Askofu Mwamakula: Tusilale usingizi pasipo kujua Moses Lijenje yupo wapi na ana hali gani

Askofu Mwamakula: Tusilale usingizi pasipo kujua Moses Lijenje yupo wapi na ana hali gani

Mwamakula anataffuta kick
Baada ya kuona watu wamempuuza na umaarufu wake kwisha
Acha upumbavu wako,hapa issue sio ya askofu, hapa ni maisha ya binadamu mwenzetu,mtanzania mwenzetu aliyekua na familia kama mimi na wewe, yaani bila hizi ID fake mtu kama wewe ningekutambua ningekuzomea kila wakati unapokwenda kwenye nyumba za ibada, maana wewe ni katili wa roho.
 
Aisee......
Kwa kweli tulifikia pabaya. Hebu fikiria mtu anapata wapi ujasiri wa kuomba tenda kutoka kwa Rais wa Tanzania ya kumuua Mtanzania na kui-post humu JF. Tulioisoma hiyo post tulipigwa butwaa!

Baadaye post hiyo inaonekana ilifutwa baada ya kuchangiwa na wazalendo wengi tu wakiulizia huu ujasiri unatoka wapi? Kwa shetani mwenyewe? Mashahidi wa hili ni wale wana JF wote walioisoma.

Hadi leo hii mtu huyo anayejiita YEHODAYA, bado anao uthubutu wa kuandika humu akimkebehi Askofu Mwamakula kwa kuhoji alipo Moses Lijenje! Yaani hadi leo haya makatili bado yapo yanadunda tu!

Kwa hakika inafikirisha sana!
 
Shahidi (mtuhumiwa) huyo ameieleza Mahakama kuwa alipokuwa akiteswa, alitishwa na mmoja wa wasulubu (Polisi) wake huku akigusishwa bastola kichwani kuwa na yeye angelitupwa kama alivyotupwa Moses Lijenje bila kutaja alitupwaje na alitupwa wapi na kwa sababu gani. Kwa maneno mengine, wasulubu (Polisi) hao ndio 'walimtupa Moses Lijenje'!
Kumekucha !
 
TUSILALE USINGIZI PASIPO KUJUA MOSES LIJENJE YUKO WAPI NA ANA HALI GANI!

View attachment 2391595

Kamanda Kingai na Afande Mahita katika nyakati tofauti kila mmoja akiwa chini ya kiapo, walitoa ushahidi Mahakamani kuwa walikuwa wakimtafuta mtuhumiwa Moses Lijenje kule Moshi. Lakini mmoja wa watuhumiwa hao (aliyesadikiwa kuwa pamoja na Moses Lijenje katika program ya VIP Protection ya Mbowe); akiongozwa na Mawakili wa Utetezi, ameieleza Mahakama mara kadhaa juu ya Moses Lijenje.

Shahidi (mtuhumiwa) huyo ameieleza Mahakama kuwa alipokuwa akiteswa, alitishwa na mmoja wa wasulubu (Polisi) wake huku akigusishwa bastola kichwani kuwa na yeye angelitupwa kama alivyotupwa Moses Lijenje bila kutaja alitupwaje na alitupwa wapi na kwa sababu gani. Kwa maneno mengine, wasulubu (Polisi) hao ndio 'walimtupa Moses Lijenje'!

Mambo mengine ni ya Jaji na Mahakama, sisi watetezi wa haki tuna jambo letu. Kama watetezi wa haki ni lazima tutake kujua Moses Lijenje yuko wapi na hali yake ikoje huko aliko. Kama kweli ametupwa, ametupwa na nani na kwa sababu gani na ametupwa wapi na hali yake ikoje huko aliko? Kutupwa huko kuna maana gani? Kesi hiyo inaweza kuchukua muda mrefu kuisha, lakini hiyo haituzuii sisi watetezi wa haki kutafuta kujua wapi aliko mtu anayeitwa Moses Lijenje na hali yake ikoje.

Kwa sababu hiyo, sisi Askofu Mwamakula tunatoa wito wa kila Mtanzania kufanya 'manhunt' yaani kuanza kumtafuta mtu aitwaye Moses Lijenje kuanzia muda huu. Jeshi la Polisi linao wajibu wa kuuambia umma ni wapi alipo ndugu Moses Lijenje! Paza sauti yako kwa kusema, kuandika na kusambaza ujumbe hadi uwafikie walio karibu na Lijenje, wanaomhifadhi, alikokimbilia au waliomtupa!

Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!
Askofu Emmaus Bandekile Mwamakula
RIP commando!!
 
Mwamakula anataffuta kick
Baada ya kuona watu wamempuuza na umaarufu wake kwisha
Lazima una matatizo ya akili. Hapa tunaongelea juu ya uhai wa mtu, wewe u unaleta maneno ya kipuuzi kabisa.

Kama unafahamu mlikomtupa au mlikomweka, utuambie.
 
Mwamakula anataffuta kick
Baada ya kuona watu wamempuuza na umaarufu wake kwisha
acha ujinga wako bhana. kama jambo huna maslahi nalo kaa kimya? hivi leo mtu akihoji
zilipo pesa za pre bagaining anatafuta kiki?
mtu akihoji ni kina nani walimpiga lisu risasi ni kutafuta kiki?
kuhoji aliko Ben sanane ni kutafuta kiki?
yupo wapi anzory gwanda?
ujinga, ushamba na roho mbaya yako peleka lumumba mkuu
 
Back
Top Bottom