Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ask Mwamakula: "Tunaitoa taarifa hii Kwa kiapo maalum Cha Uaskofu"Nimesoma hii post ya Askofu wa CHADEMA ndugu Mwamakula na kusikitishwa na huu uchochezi wa kipuuzi. Askofu Mwamakula atanufaika vipi na machafuko anayotaka yatokee kwenye jamii? Ninawasihi vyombo vya usalama visimchekee wala kumwonea huruma Askofu kama huyu mchochezi. Soma hapo chini taarifa yake ya kichochezi
USALAMA WA MAISHA YA PETER MADELEKA UKO HATARINI GEREZANI KISONGO, ARUSHA!
Ndugu Watanzania!
Sisi Askofu Mwamakula tumejulishwa juu ya njama zinazopangwa kutaka kuondoa uhai wa Peter Madeleka. Taarifa hizi zimevujishwa na mmoja wa Askari Magereza kutoka Gereza la Kisongo alikowekwa mahabusu wakili msomi Peter Madeleka aliye miongoni mwa mawakili waliopiga kelele kupinga Mkataba wa Bandari.
Sisi Askofu Mwamakula tunatoa tahadhari hii kuwa taarifa hizo zimevuja na hivyo wahusika waache mara moja mpango wa kutaka kumpa sumu Peter Madeleka. Tunaitoa taarifa hii kwa kiapo maalum cha Uaskofu. Tunashukuru sana kwa uzalendo huo kwa upande wa Askari huyo.
Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!
Askofu Emmaus Bandekile Mwamakula
Dar es Salaam, 29 Julai 2023; 13:45 pm
Usiwe na wasiwasi na huyu kichaa anayejiita askofu. Kwanza, uliishawahi kumuona siku yoyote anaendesha ibada? Sasa ataletaje machafuko huyu mwehu?Nimesoma hii post ya Askofu Mwamakula na kusikitishwa na huu uchochezi. Askofu Mwamakula atanufaika vipi na machafuko anayotaka yatokee kwenye jamii? Ninawasihi vyombo vya usalama visimchekee wala kumwonea huruma Askofu kama huyu mchochezi. Soma hapo chini taarifa yake ya kichochezi
USALAMA WA MAISHA YA PETER MADELEKA UKO HATARINI GEREZANI KISONGO, ARUSHA!
Ndugu Watanzania!
Sisi Askofu Mwamakula tumejulishwa juu ya njama zinazopangwa kutaka kuondoa uhai wa Peter Madeleka. Taarifa hizi zimevujishwa na mmoja wa Askari Magereza kutoka Gereza la Kisongo alikowekwa mahabusu wakili msomi Peter Madeleka aliye miongoni mwa mawakili waliopiga kelele kupinga Mkataba wa Bandari.
Sisi Askofu Mwamakula tunatoa tahadhari hii kuwa taarifa hizo zimevuja na hivyo wahusika waache mara moja mpango wa kutaka kumpa sumu Peter Madeleka. Tunaitoa taarifa hii kwa kiapo maalum cha Uaskofu. Tunashukuru sana kwa uzalendo huo kwa upande wa Askari huyo.
Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!
Askofu Emmaus Bandekile Mwamakula
Dar es Salaam, 29 Julai 2023; 13:45 pm
Nondo juu ya nondoHata wafanyaje
Hoja kuu zinazohitaji majibu ni hizi hapa
1.) Tofauti ya ‘Makubaliano’ na ‘Mkataba’ ni ipi hasa kiasi mseme ule sio mkataba, kwamba ni makubaliano tu ya awali, na je Mkataba huo (makubaliano hayo) ni wa miaka mingapi? (UKOMO)
2.) Ni kwa faida ya nani kwamba DPW anapewa haki ya bandari zote za Tanganyika, kwamba hakuna mwekezaji mwingine yeyote anaweza kuja kufanya uwekezaji kwenye bandari za Tanganyika bila udalali wa DPW, je, ukiritimba huu ni kwa faida ya nani?
3.) Ni kwa faida ya nani, DPW apewe haki ya kudai kipande chochote cha ardhi yenye ukubwa wowote anaoutaka yeye ndani ya ‘Territory’ ya Tanganyika na sisi tumpe ardhi hiyo kwa kuondoa watu na miradi yote ndani ya eneo alilolitaka, na tumpatie bire kabisa kwa gharama zetu sisi, hata fidia tulipe sisi ili kuondoa watu kumpisha, huu uwendawazimu ni kwa faida ya nani?
4.) Ni kwa faida ya nani, kwamba sisi tuliowekeza matrillion ya mikopo kuendeleza bandari na tukiwa kama wamiliki wa rasimali ya bandari, tupate 0% ya faida itakayotokana na uendeshaji wa huduma za kibandari, yaani ni kana kwamba yeye kawekeza 100% na hivyo achukue 100%? Uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?
5.) Ni kwa faida ya nani, kwamba mkataba unahusisha bandari za Tanganyika tu na sio za Zanzibar, ilihali bandari ni suala la Muungano? Je, Zanzibar haitaki kunufaika au yenyewe haitaki matunda ya mkataba huu? Ukizingatia walioongia huu mkataba wote ni waZanzibari, kuanzia Samiah Suluhu Hassan, Makame Mbarawah, Hamza Johari na wenzao, kwamba hawataki Zanzibar yao ipate matunda mazuri ya mkataba huu?!
6.) Ni kwa faida ya nani kusema kwamba, hata DPW akavunja mkataba na kukiuka kanuni na taratibu zote zinazotambulika kimataifa, bado hatutaweza kuvunja , kuusema vibaya au kujitoa kwenye mkataba, milele! Uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?
7.) Ni kwa faida ya nani kwamba pamoja na kuwa DPW watachukua 100% ya faida, bado tena faida hiyo watapewa Msamaha wa kodi kwa 100%, yaani hata hicho wanachovuna nacho hatuchukui kodi, na wakti huo huo tunakamuliwa kodi za miamala, uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?
Kwani ni dhambi?Haka kaaskofu kanapenda sana siasa
Mwamakula naye amepinda tu kama mateja yanayovuta unga. Yeye Hana kanisa wala waumini popote japo anaitwa Askofu wa Moravian Uamsho
Emmanuel Bandekile Mwamakula ni Tapeli tu kama tapeli yeyote unayomfahamu. Wenzie wa Moravian Mbeya walimtimua walipoona ni mdokozi wa sadaka
Hivyo walivyo rekebisha na kuiweka Mods ndiyoo inatakiwa iwe hivyo, sivyo utakavyo wewe.Nimeamua kuufuta uzi kwasababu Mods wa JF wameubadilisha kuuweka jinsi wanavyotaka wao. Kichwa cha habari kilikuwa kinasema ASKOFU MWAMAKULA ACHA UCHOCHEZI wameamua kubadili na kuweka wanavyoona wao. Na baadhi ya comments zimefutwa bila sababu. Tafadhalini JF kama mmeamua JF iwe sehemu huru ya kutoa maoni basi acheni iwe huru. Naomba ufafanuzi kama kuna kosa lolote kwenye kichwa cha habari nilichokuwa nimeweka. Pia kwanini comments zingine mzifute.
Uasikofu ni taasisi kama ilivyo urais, anaposema sisi askofu ... , anamaanisha yeye pamoja na jopo lake.Bandari haiuzwi,wazalendo wapo kila kina hadi Magereza,watapike hela za mwarabu tu ndio pona yao.
"Sisi Askofu Mwamakula" ana maanisha nini,mara kadhaa naiona hii?
Mwenye ufahamu anijulishe
Mtakatifu Luka hujapost Pambio leo ?Huyu askofu huwa nina mashaka naye maana nahisi analaaana fulani hivi kutoka kwa Mwenyezi Mungu,ndio maana ameacha kazi ya utumishi wa Mungu na kubaki mpiga Ramli ,mchochezi na mtu asiyefaa kuitwa mtumishi wa Mungu.sasa anajifanya anajificha kwenye koti la uaskofu wa kujipa,. Serikali inatakiwa iwachukulie hatua kali sana watu wa aina hii maana ni hatari kwa usalama wa Taifa kutokana na kuleta sintofahamu na mitafaruko isiyo na ukweli wala msingi katika jamii.