Askofu Mwamakula: Usalama wa maisha ya Peter Madeleka uko hatarini Gerezani kisongo, Arusha!

Askofu Mwamakula: Usalama wa maisha ya Peter Madeleka uko hatarini Gerezani kisongo, Arusha!

Bandari haiuzwi,wazalendo wapo kila kina hadi Magereza,watapike hela za mwarabu tu ndio pona yao.

"Sisi Askofu Mwamakula" ana maanisha nini,mara kadhaa naiona hii?

Mwenye ufahamu anijulishe
"Sisi Askofu Mwamakula" maana yake ni taasisi na si mtu.
Wa ovyo hawa jamaa
 
Huyu askofu huwa nina mashaka naye maana nahisi analaaana fulani hivi kutoka kwa Mwenyezi Mungu,ndio maana ameacha kazi ya utumishi wa Mungu na kubaki mpiga Ramli ,mchochezi na mtu asiyefaa kuitwa mtumishi wa Mungu.sasa anajifanya anajificha kwenye koti la uaskofu wa kujipa,. Serikali inatakiwa iwachukulie hatua kali sana watu wa aina hii maana ni hatari kwa usalama wa Taifa kutokana na kuleta sintofahamu na mitafaruko isiyo na ukweli wala msingi katika jamii.
MAGUFULI: Ni kichaa peke yake anayeweza kuushabikia mkataba huu wa Kimangungo. IBARA 4 (2) ya mkataba huu inasema, Tanzania inapotaka kuweka mwekezaji mwingine maeneo mengine ya bandari inatakiwa iende Dubai kuomba ridhaa, Dubai wakikataa kutoa idhini ndio basi. Yaani nchi huru ikaombe ridhaa Dubai, kwa Mali zake? Huu uwendawazimu uko CCM ukishabikiwa na Wasira na Waitara.
 
Bandari haiuzwi,wazalendo wapo kila kona hadi Magereza,watapike hela za mwarabu tu ndio pona yao.

"Sisi Askofu Mwamakula" ana maanisha nini,mara kadhaa naiona hii?

Mwenye ufahamu anijulishe
Uaskofu ni Taasisi.
 
Madeleka akitoka poa tutasema kelele zimesaidia atoke poa au kelele ni uzushi tu?
 
Hata wafanyaje

Hoja kuu zinazohitaji majibu ni hizi hapa

1.) Tofauti ya ‘Makubaliano’ na ‘Mkataba’ ni ipi hasa kiasi mseme ule sio mkataba, kwamba ni makubaliano tu ya awali, na je Mkataba huo (makubaliano hayo) ni wa miaka mingapi? (UKOMO)

2.) Ni kwa faida ya nani kwamba DPW anapewa haki ya bandari zote za Tanganyika, kwamba hakuna mwekezaji mwingine yeyote anaweza kuja kufanya uwekezaji kwenye bandari za Tanganyika bila udalali wa DPW, je, ukiritimba huu ni kwa faida ya nani?

3.) Ni kwa faida ya nani, DPW apewe haki ya kudai kipande chochote cha ardhi yenye ukubwa wowote anaoutaka yeye ndani ya ‘Territory’ ya Tanganyika na sisi tumpe ardhi hiyo kwa kuondoa watu na miradi yote ndani ya eneo alilolitaka, na tumpatie bire kabisa kwa gharama zetu sisi, hata fidia tulipe sisi ili kuondoa watu kumpisha, huu uwendawazimu ni kwa faida ya nani?

4.) Ni kwa faida ya nani, kwamba sisi tuliowekeza matrillion ya mikopo kuendeleza bandari na tukiwa kama wamiliki wa rasimali ya bandari, tupate 0% ya faida itakayotokana na uendeshaji wa huduma za kibandari, yaani ni kana kwamba yeye kawekeza 100% na hivyo achukue 100%? Uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?

5.) Ni kwa faida ya nani, kwamba mkataba unahusisha bandari za Tanganyika tu na sio za Zanzibar, ilihali bandari ni suala la Muungano? Je, Zanzibar haitaki kunufaika au yenyewe haitaki matunda ya mkataba huu? Ukizingatia walioongia huu mkataba wote ni waZanzibari, kuanzia Samiah Suluhu Hassan, Makame Mbarawah, Hamza Johari na wenzao, kwamba hawataki Zanzibar yao ipate matunda mazuri ya mkataba huu?!

6.) Ni kwa faida ya nani kusema kwamba, hata DPW akavunja mkataba na kukiuka kanuni na taratibu zote zinazotambulika kimataifa, bado hatutaweza kuvunja , kuusema vibaya au kujitoa kwenye mkataba, milele! Uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?

7.) Ni kwa faida ya nani kwamba pamoja na kuwa DPW watachukua 100% ya faida, bado tena faida hiyo watapewa Msamaha wa kodi kwa 100%, yaani hata hicho wanachovuna nacho hatuchukui kodi, na wakti huo huo tunakamuliwa kodi za miamala, uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?
Safi sana! Hakuna kuyumbishwa na propaganda za UDINI au ushenzi mwingine! warudishe mchongo wa watu mali zetu hazigawiwi kama njugu -----CC FaizaFoxy
 
Nimeamua kuufuta uzi kwasababu Mods wa JF wameubadilisha kuuweka jinsi wanavyotaka wao. Kichwa cha habari kilikuwa kinasema ASKOFU MWAMAKULA ACHA UCHOCHEZI wameamua kubadili na kuweka wanavyoona wao. Na baadhi ya comments zimefutwa bila sababu. Tafadhalini JF kama mmeamua JF iwe sehemu huru ya kutoa maoni basi acheni iwe huru. Naomba ufafanuzi kama kuna kosa lolote kwenye kichwa cha habari nilichokuwa nimeweka. Pia kwanini comments zingine mzifute.
sasa wewe unasema aache uchochez, wakati mtajwa kweli yupo hatarini! Hapo nani mchochezi? yeye au wewe utakaye yeye naye ashughurikiwe
 
Bandari haiuzwi,wazalendo wapo kila kona hadi Magereza,watapike hela za mwarabu tu ndio pona yao.

"Sisi Askofu Mwamakula" ana maanisha nini,mara kadhaa naiona hii?

Mwenye ufahamu anijulishe
Hii inaitwa "the royal "we"" au "majestic plural". Hutumika na viongozi ambao hata kiongozi akisema neno, neno hilo si lake yeye tu, linawakilisha maoni ya uongozi mzima, huwa linatumika sana na Wafalme.

Mfano, Mfalme Haile Selassie I, Negus Nagast, alikuwa mara nyingi anatumia "sisi" badala ya "mimi" kwa maana yeye anawakilisha watu wote, sio tu wanaoishi, bali pia waliofariki, waliopo na watakaokuja kuzaliwa.

Askofu Mwamakula inaonekana anatumia mfumo huu kuwakilisha maoni ya maaskofu, si maoni yake binafsi.

Asante Kwa elimu hii
 
Nimeamua kuufuta uzi kwasababu Mods wa JF wameubadilisha kuuweka jinsi wanavyotaka wao. Kichwa cha habari kilikuwa kinasema ASKOFU MWAMAKULA ACHA UCHOCHEZI wameamua kubadili na kuweka wanavyoona wao. Na baadhi ya comments zimefutwa bila sababu. Tafadhalini JF kama mmeamua JF iwe sehemu huru ya kutoa maoni basi acheni iwe huru. Naomba ufafanuzi kama kuna kosa lolote kwenye kichwa cha habari nilichokuwa nimeweka. Pia kwanini comments zingine mzifute.
JF=CHADEMA na CHADEMA= JF
 
Haka kaaskofu ni kachonganishi sana. Sasa mbona huyo Madeleka bado hajafa huko Kisongo?
 
Mwamakula naye amepinda tu kama mateja yanayovuta unga. Yeye Hana kanisa wala waumini popote japo anaitwa Askofu wa Moravian Uamsho

Emmanuel Bandekile Mwamakula ni Tapeli tu kama tapeli yeyote unayomfahamu. Wenzie wa Moravian Mbeya walimtimua walipoona ni mdokozi wa sadaka
Una uhakika wewe MATAGA?
 
Bandari haiuzwi,wazalendo wapo kila kona hadi Magereza,watapike hela za mwarabu tu ndio pona yao.

"Sisi Askofu Mwamakula" ana maanisha nini,mara kadhaa naiona hii?

Mwenye ufahamu anijulishe
Kwani nani alikuwa anauza bandari?
 
Back
Top Bottom