Jamal Akbar
JF-Expert Member
- Oct 9, 2014
- 413
- 471
Viongozi wa dini wamemsifu Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuifungua nchi kibiashara kwa kuwajengea wote wenye nia ya biashara kuingia kufanya hivyo, huku akiondoa vikwazo vinavyonyima fursa.
Akizungumza kwa niaba ya viongozi wenzake, Mwenyekiti wa Kamati ya Kitaifa ya Maaskofu na Masheikh ya Maadili, Amani na Haki za Binadamu, Askofu William Mwamalanga alimpongeza Rais Samia kwa kuunganisha tena Watanzania hasa wafanyabiashara wa ndani na mataifa mengine.
"Ni wakati wenu kuunganisha nguvu zenu za mitaji ili kuwekeza kwenye miradi mikubwa ya kilimo, madini na hata katika baadhi ya maeneo ya bandari zetu nyingi tulizotengeneza. baada ya kujaliwa bahari na maziwa mengi.
"Tusiogope kuwekeza kwenye taifa letu...kuweni wajanja kuchungulia ile miradi inayochunguliwa na wageni na sisi tuingie haraka kuwekeza ...hivi kweli tunashindwa kuendesha biashara na kazi kama za usafi wa miji yetu, kupanda miti ili kukuza misitu, kushirikiana kujenga viwanda vya mbolea mikoani badala ya kuvilundika Dar es Salaam, au kuendeleza fukwe za bahari," alisema Askofu Mwamalanga.
Akizungumzia serikali, Askofu Mwamalanga ali-isifu kwa hatua ilizochukua na akaiomba wizara yenye dhamana ya uwekezaji kuendelea kuzitangaza fursa za maeneo ya uwekezail kwa wafanyabiashara wandani kabla ya kuzitangaza hizo fursa nje pekee yake.
"Ni vyema serikali kila mwezi ilipe muda wa kuwapa Watanzania fursa za kuwekeza kwa lengo la kuwakuza wawekezaji wa ndani. Lakini nanyi Watanzania hebu kuweni wathubutu basi bila kuogopa kuingia kwenye sekta.za uwekezaji. Ingieni kwenye biashara na uwekezaji, tukuze uchumi, tuzalishe na kuuza bidhaa nje ya nchi na kupandisha thamani ya shilingi yetu dhidi ya sarafu za kigeni," alihimiza Askofu Mwamalanga.
Akiwa ameongozana na baadhi ya viongozi wa kamati yake, Askofu Mwamalanga aliwahimiza viongozi wa dini kuwasaidia vijana kuchukua ukurasa mpya kwa maendeleo badala ya kubakia kwenye biashara za bodaboda. tu.
"Ni wajibu wa viongozi wa dini nchini kushiriki kwenye fursa za maendeleo kwa kuwafundisha waumini kuchukua nafasi hizo badala ya kubakia kwenye utazamaji na ugeni wa fursa hizo, hii ni njia muhimu ya kulinda amani ya taifa letu, alihitimisha.