Elias Msuya
Platinum Member
- Dec 23, 2011
- 267
- 1,014
Singida. Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Wilaya ya Itilima mkoani Simiyu Askofu Maximilian Machumu Kadutu maarufu Mwanamapinduzi amekutwa na kesi ya kujibu katika kesi ya uchochezi inayomkabili katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Singida mkoani Singida.
Hatua hiyo imekuja baada ya kuhitimishwa kwa ushahidi, ambapo mashahidi wanne walitoa ushahidi wao katika mahakama hiyo kwa Agosti 6 na 7, 2025.
Taarifa kutoka mahakamani hapo zinasema, baada ya ushahidi huo, mahakama alitoa uamuzi mdogo ulioonyesha kuwa mtuhumiwa ana kesi ya kujibu.
Baada ya uamuzi huo, mshitakiwa Mwanamapinduzi alijitetea mbele ya Mahakama na hivyo kufunga ushahidi na ndipo upande wa Jamhuri umetakiwa kuandaa hoja za mwisho zitakazotolewa 21, Agosti,2025 na ndiyo siku ambayo kesi hiyo itatajwa mahakamani hapo kwa mara nyingine tena.
Awali wakati ilipoanza upande wa Jamhuri walisema ya kwamba wana mashahidi wapatao 13 lakini mpaka ushahidi ulipofungwa siku ya jana kwa upande wa Jamhuri wameweza kupeleka mashahidi saba tu.
Askofu Mwanamapinduzi anakabiliwa na kesi uchochezi katika maneno yake aliyoyatamka mwaka jana katika mkutano wa hadhara wa CHADEMA ulioongozwa na Mwenyekiti wa chama hicho, Tundu Lissu katika Mkoa wa Singida.
Maneno yanayolalalamikiwa katika kesi hiyo ni "wakiwananihii muwananihii."
Mwanzo wa kesi hiyo, Askofu Mwananpinduzi alikuwa akiwakilishwa na Lissu, lakini kwa sasa anawakilishwa na Hemed Kulungu.