Parabolic
JF-Expert Member
- Dec 3, 2013
- 2,922
- 3,252
Leo Septemba 29, 2025, Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Singida imemuachia huru Askofu Maximilian Machumu Kadutu (Mwanamapinduzi), Mwenyekiti wa CHADEMA Wilaya ya Itilima, Mkoa wa Simiyu, na Naibu Katibu Mkuu wa Kanisa la Glory of Christ Tanzania (GCTC) Maarufu kama Kanisa la Ufufuo na Uzima linaloongozwa na Askofu Mkuu Dkt. Josephat Gwajima.
Askofu Mwanamapinduzi alikuwa anakabiliwa na kesi ya uchochezi namba 19525/2024 tangu Juni 3, 2024. Katika hukumu iliyotolewa leo, Mahakama imebainisha kuwa, kwa mujibu wa ushahidi uliotolewa na mashahidi 10 wa upande wa Jamhuri, haikupatikana misingi ya kisheria ya kumtia hatiani, Hivyo basi Mahakama imemuachia huru Askofu Mwanamapinduzi.
Soma Pia: Askofu Mwanamapinduzi akutwa na kesi ya kujibu kesi ya uchochezi
Ikumbukwe kuwa kesi hiyo, ambayo ilivuta hisia za wengi kitaifa, awali ilisimamiwa na Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Mheshimiwa Wakili Tundu Lissu, na baadaye kuchukuliwa na Wakili Hemedi Kulungu pamoja na Wakili Hekima Mwasipu, ambao wameshikilia keshi hiyo mpaka mwisho.
Chanzo: Askofu Mwanamapinduzi