Leo Septemba 29, 2025, Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Singida imemuachia huru Askofu Maximilian Machumu Kadutu (Mwanamapinduzi), Mwenyekiti wa CHADEMA Wilaya ya Itilima, Mkoa wa Simiyu, na Naibu Katibu Mkuu wa Kanisa la Glory of Christ Tanzania (GCTC) Maarufu kama Kanisa la Ufufuo na Uzima linaloongozwa na Askofu Mkuu Dkt. Josephat Gwajima.
Askofu Mwanamapinduzi alikuwa anakabiliwa na kesi ya uchochezi namba 19525/2024 tangu Juni 3, 2024. Katika hukumu iliyotolewa leo, Mahakama imebainisha kuwa, kwa mujibu wa ushahidi uliotolewa na mashahidi 10 wa upande wa Jamhuri, haikupatikana misingi ya kisheria ya kumtia hatiani, Hivyo basi Mahakama imemuachia huru Askofu Mwanamapinduzi.
Ikumbukwe kuwa kesi hiyo, ambayo ilivuta hisia za wengi kitaifa, awali ilisimamiwa na Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Mheshimiwa Wakili Tundu Lissu, na baadaye kuchukuliwa na Wakili Hemedi Kulungu pamoja na Wakili Hekima Mwasipu, ambao wameshikilia keshi hiyo mpaka mwisho.
Hii taarifa rasmi imetolewa na Askofu Emaus Mwamakula.
Nimewawekea hapa chini tamko lake soon hapa (kwa njia ya video). Ameelezea kwa kina kilichomsibu na hata kutishiwa maisha.
Hii taarifa rasmi imetolewa na Askofu Emaus Mwamakula.
Nimewawekea hapa chini tamko lake soon hapa (kwa njia ya video). Ameelezea kwa kina kilichomsibu na hata kutishiwa maisha.
Maana yake ni ile ile wanayo itumia sasa hivi kwa Tundu Lissu; wamwachie, "aondoke nchini"!
Naona miaka hii mitano endapo huyu jambazi atanyang'anya atawale, Tanzania itazalisha wakimbizi wengi wa kisiasa, kama wameamua hii ndiyo iwe njia ya kuwaziba watu midomo.
Naam , ni tishio kwa amani feki ambayo ndio comfort ya mafisadi.
Hii amani tunayoambiwa ipo ni turufu kubwa na inapendwa na mafisadi maana wanaendelea kujipimia kwa urefu wa kamba zao bila ya kuwa na wasiwasi ni kizazi hadi kizazi.
Naona miaka hii mitano endapo huyu jambazi atanyang'anya atawale, Tanzania itazalisha wakimbizi wengi wa kisiasa, kama wameamua hii ndiyo iwe njia ya kuwaziba watu midomo.
Napenda sana kuamini hivyo; lakini....
Endapo waTanzania wataipoteza nafasi nzuri na adimu kabisa ya kuondoa uchafu huu Oktoba 29; taifa hili litalipa gharama kubwa sana katika miaka hiyo mitano au zaidi ya hawa waovu kuendelea kuwa watawala.
WaTanzania watashindwa vipi kulielewa jambo hili jepesi namna hii?
Napenda sana kuamini hivyo; lakini....
Endapo waTanzania wataipoteza nafasi nzuri na adimu kabisa ya kuondoa uchafu huu Oktoba 29; taifa hili litalipa gharama kubwa sana katika miaka hiyo mitano au zaidi ya hawa waovu kuendelea kuwa watawala.
Kweli unaamini ni CCM ndiyo inayofanya haya ya sasa?
Hilo jina la CCM, na miundo mbinu zake ndizo zinazo tumika sasa hivi; chama hakipo tena.
Ukiona Kikwete na Samia ndio wanampitisha mgombea wa chama; hiyo ni ishara tosha kuu ya kukuonyesha kwamba chama hakipo tena. Hakuna chama kinacho amua chochote. Ni kundi la watu waovu ndio wameshika jina la chama na kulitumia wanavyo taka wenyewe.
Naona inawawia vigumu watu wengi kuelewa hili jambo; sijui kwa nini hawataki kulielewa.