Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 5,383
- 18,776
Askofu Mwanamapinduzi ametoa tahadhari kali kwa wale wanaojaribu kumjibu au kumshambulia Askofu Josephat Gwajima kufuatia kauli na hoja alizozitoa hivi karibuni, akisema si mtu wa kubezwa wala wa kuchukuliwa kawaida.
Katika kauli yake, Askofu Mwanamapinduzi amesema hoja alizotoa Gwajima ni nzito na hazipaswi kurukiwa bila tafakari. Amedai kuwa Gwajima ana uwezo mkubwa wa kufikiri, kufanya utafiti, na kushawishi jamii, hivyo si mtu wa kumjibu kwa pupa.
"Askofu Gwajima sio mtu mwepesi, sio mtu wa kawaida. Uwezo wake wa akili ni mkubwa, na ana ushawishi mkubwa kwa wananchi wa kawaida. Wasiwaze ametamka tu kwa bahati mbaya, wasichukulie kawaida," alisema.
Akiendelea, alionya vikali dhidi ya jaribio lolote la kutumia vyombo vya dola kumkamata au kumfungulia kesi kama njia ya kuzima hoja zake, akisema hatua kama hiyo inaweza kuibua madhara makubwa.
"Nawaonya, wakijaribu kumkamata au kumsingizia kesi badala ya kujibu hoja zake, watakuwa wameingia kwenye mzigo mkubwa. Askofu Gwajima ana wafuasi wengi nchi nzima – kila mkoa, kila wilaya – ana mtandao mpana," alisisitiza.