Mkalukungone Mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 3,141
- 7,205
Naibu Katibu Mkuu wa Makanisa ya Ufufuo na Uzima (GCTC), Askofu Maximilian Machumu Kadutu maarufu kama Mwanamapinduzi, ameibua maswali kuhusu hatua ya Serikali kufungia makanisa yote ya Ufufuo na Uzima nchini akisema waumini wa makanisa hayo sasa wanaishi kama ‘wakimbizi wa kiroho’.
Akizungumza siku ya Jumapili Agosti 03, 2025 mara baada ya ibada iliyofanyika kwenye ukumbi wa kukodi mkoani Dar es Salaam, Askofu Kadutu amesema tangu kufungwa kwa makanisa hayo yaliyo chini ya Askofu Josephat Gwajima, waumini wamekuwa wakitangatanga pasipo sehemu rasmi ya kusali huku wengi wakikumbwa na sintofahamu ya kiimani.
“Ukweli ni kwamba watu hawa wamekuwa kama wakimbizi wa kiroho. Kuna wakimbizi wanaokimbilia katika nchi mbalimbali kutafuta hifadhi baada ya kuziacha nchi zao. Sasa waumini hawa ni wakimbizi wa kiroho,” amesema Kadutu.
Ameeleza kuwa uamuzi wa serikali kufungia makanisa yote ya Ufufuo na Uzima kwa madai ya kuchanganya dini na siasa, hauwezi kueleweka kwa kuwa hakuna ushahidi wa kauli za kisiasa kutolewa kwenye makanisa yote nchini.
Kadutu amesema waumini sasa wanalazimika kusali kwenye maeneo ya muda au kumbi za kukodi bila kuwa na utulivu wa kiroho huku wakijitahidi kutovunja sheria.