Askofu Niwemugizi asikitishwa na Kauli ya Humphrey Polepole kuwafananisha Wapinzani na Corona

Askofu Niwemugizi asikitishwa na Kauli ya Humphrey Polepole kuwafananisha Wapinzani na Corona

Polepole amelewa madaraka!
"Nearly an old man can withstand adversity but if you want to test the man's character,give him power"!
Abraham Lincoln
Uko sahihi madaraka yamemlevya anafikiri ameshafika! Hakumbuki kabla yake alikuwepo aliyekalia hicho cheo cha Ukatibu uenezi.
 
Pole Pole amekuwa haraka haraka . Amekuwa kinyaaa. Hathaminiki tena ndani ya jamii. Dharau kwa binadamu aliyeumbwa kwa mfano wa Mungu, laana KUU itampata.

Sent using Jamii Forums mobile app
Taarifa zinaonyesha kwamba atakuwa mtu wa kwanza kukimbia nchini baada ya ccm kuangushwa october , atakimbilia Rwanda ,tayari amelipia nyumba
 
Polepole ni laana kwa nchi hii
View attachment 1394253

Nimesikitika sana kusoma maneno kwenye mtandao ambayo sijaamini yamesemwa kweli na mtu ambaye huko nyuma nilimheshimu sana, kwamba, tunaomba Mungu ugonjwa huu uondoke, Corona ni sawa na wapinzani nchini“.

Nikayakumbuka maneno ya Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Mheshimiwa Anna Mgwira aliyosema jana kwenye salamu zake baada ya ibada ya kumsimika Askofu Ludovic Joseph Minde kuwa Askofu wa Moshi.

Alisema kwa kurudia rudia „tusaidieni (viongozi wa dini) kuwatengeneza watu wema wanaoheshimu utu wa watu na haki za watu“. Nimejiuliza hivi kweli hiyo ni siasa safi binadamu kumwona au kumuita mwenzake ni sawa na kirusi cha Corona?

Kumwona binadamu aliyeumbwa kwa sura na mfano wa Mungu ni tusi kubwa kwa Mungu mwenyewe kwamba Yeye Mungu naye ni sawa na kirusi cha Corona, kinachopaswa kuondoka!! Halafu unamwomba huyo Mungu aondoe Corona?!

Hapo ndipo tumefika Watanzania kweli!? Hiyo ndiyo sura ya, siasa ni uadui“. Mtu mnayetofautiana mtazamo au itikadi ni adui, ila kesho akibadili mtazamo akafuata wako anabadilika na kuwa lulu nzuri, rafiki, na binadamu kama wewe.

Jamani! Nawasihi Watanzania tujitahidi kupima maneno tunayozungumza hadharani kumhusu binadamu mwingine.

Mtakatifu Yakobo anasema „Mtu asiyejikwaa katika kunena, huyo ni mtu mkamilifu, anaweza kuuzuia na mwili wake wote kama kwa lijamu“ (Yak 3:2). Na tena, ulimi ni uovu usiotulia, umejaa sumu iletayo mauti“ (3:8).

Namshauri aliyesema Corona ni sawa na wapinzani katika nchi hii kama ni muungwana aombe radhi kwa kumdhalilisha Mungu aliyemuumba binadamu kwa sura na mfano wake (Mwa 1:26-27).

Kwa namna hiyo ataepusha mauti kwa heshima yake mwenyewe na na kwa siasa za kistaarabu.

Source: FB page yake

My take:
1. CCM kutokanusha kauli hii ni sawa na kubariki, ndio tuseme ni msimamo wa chama.
2. Tahadhari wasimtingishe tena askofu na zile saga za uraia na passport

Sent from my SM-J110H using JamiiForums mobile app
 
Kuna huyu polepole and DC sabaya sijui Magufuli aliwatoa wapi, wao hujisemea lolote linalokuja kinywani bila kupima madhara yake, watawala lugha zao zimekuwa sio nzuri kwa upinzani bila kujua kuwa wapinzani pamoja na mapungufu yao bado ni watanzania na wanajenga Tanzania moja kwa mawazo tofauti.
 
View attachment 1394253

Nimesikitika sana kusoma maneno kwenye mtandao ambayo sijaamini yamesemwa kweli na mtu ambaye huko nyuma nilimheshimu sana, kwamba, tunaomba Mungu ugonjwa huu uondoke, Corona ni sawa na wapinzani nchini“.

Nikayakumbuka maneno ya Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Mheshimiwa Anna Mgwira aliyosema jana kwenye salamu zake baada ya ibada ya kumsimika Askofu Ludovic Joseph Minde kuwa Askofu wa Moshi.

Alisema kwa kurudia rudia „tusaidieni (viongozi wa dini) kuwatengeneza watu wema wanaoheshimu utu wa watu na haki za watu“. Nimejiuliza hivi kweli hiyo ni siasa safi binadamu kumwona au kumuita mwenzake ni sawa na kirusi cha Corona?

Kumwona binadamu aliyeumbwa kwa sura na mfano wa Mungu ni tusi kubwa kwa Mungu mwenyewe kwamba Yeye Mungu naye ni sawa na kirusi cha Corona, kinachopaswa kuondoka!! Halafu unamwomba huyo Mungu aondoe Corona?!

Hapo ndipo tumefika Watanzania kweli!? Hiyo ndiyo sura ya, siasa ni uadui“. Mtu mnayetofautiana mtazamo au itikadi ni adui, ila kesho akibadili mtazamo akafuata wako anabadilika na kuwa lulu nzuri, rafiki, na binadamu kama wewe.

Jamani! Nawasihi Watanzania tujitahidi kupima maneno tunayozungumza hadharani kumhusu binadamu mwingine.

Mtakatifu Yakobo anasema „Mtu asiyejikwaa katika kunena, huyo ni mtu mkamilifu, anaweza kuuzuia na mwili wake wote kama kwa lijamu“ (Yak 3:2). Na tena, ulimi ni uovu usiotulia, umejaa sumu iletayo mauti“ (3:8).

Namshauri aliyesema Corona ni sawa na wapinzani katika nchi hii kama ni muungwana aombe radhi kwa kumdhalilisha Mungu aliyemuumba binadamu kwa sura na mfano wake (Mwa 1:26-27).

Kwa namna hiyo ataepusha mauti kwa heshima yake mwenyewe na na kwa siasa za kistaarabu.

Source: FB page yake

My take:
1. CCM kutokanusha kauli hii ni sawa na kubariki, ndio tuseme ni msimamo wa chama.
2. Tahadhari wasimtingishe tena askofu na zile saga za uraia na passport
tatizo hawa makada wa MATAGA wanaitikia kibwagizo cha wimbo aliouanzisha bosi wao (mwenyekiti wa chama chetu)..... wimbo wa kusema mbofumbofu hadharani bila mshipa wa aibu.

aibu naona mimi sasa!
 
Naongea Leo hii tarehe 20 mwezi March mwaka 2020, Kwa kauli hii ya dhihaka na kejeli aliyoitoa Polepole, kipindi ambacho virusi vya Corona vitafutika kwenye Ardhi hii ndicho kipindi Polepole atafutika pamoja navyo.

MWENYEZI MUNGU HADHIHAKIWI

Sent using Jamii Forums mobile app
Hawa walevi akina Pole Pole ni wasahaulifu Sana. Wamesahau alichosema Komba kwamba zikiruhusiwa serikali tatu nchini kwenye Katiba Mpya, yeye Komba ataenda msituni, na kweli alienda kwenye msitu asikoweza kurudi asilani. Mungu hadhihakiwi?
Au amuulize Komandoo Salmin alivyoapa kutomwona Seif Sharif akimwita Hizbu kwa macho akiingia Ikulu ya Zanzibar. Kilichofuatia Ni kupofuka Kisha Seif akawa Makamu wa Rais wa Zanzibar na Juma Duni Haji akawa ndiye anamwandikia ruhusa ya matibabu
Mungu hadhihakiwi. Kina Polepole watakiona, Acha wacheze mdundiko dhidi ya Mwenye viumbe vyake!!
 
Usiwe serious sana, kuna mwanachema mmoja humu alikuwa anaomba corona ije Tanzania..na bado alijetetea na lengo lake au mawazo yake ilikuwa CCM iathilike, kwa hiyo na huyu kuwafananisha CDM na corona hana tofauti na yule...au mm sijaelewa? Wote hawa wanafanya mzaha na Corona
Nakumbuka yule si ni chadema na watu humu walimsapoti Sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Naongea Leo hii tarehe 20 mwezi March mwaka 2020, Kwa kauli hii ya dhihaka na kejeli aliyoitoa Polepole, kipindi ambacho virusi vya Corona vitafutika kwenye Ardhi hii ndicho kipindi Polepole atafutika pamoja navyo.

MWENYEZI MUNGU HADHIHAKIWI

Sent using Jamii Forums mobile app

Hata wewe huna tofauti na corona


Sent from my iPhone using Tapatalk
 
Ufafanuzi hapo kwenye bold.
Tuachane na spelling ni typing error na hiyo auto correction ya kiingereza kwenye kiswahili.Wali tuambia wamejipanga tusiwe na wasiwasi,huyo alioji nchi kama USA n.k umesha ingia inakuwaje Ummy kujiamini sana na baada ya siku chache sana tuna ambiwa ugonjwa umeingia TZ.Nini kosa lake?
 
Kama taifa wakati huu tuna matatizo mengi sana, Polepole ni moja ya matatizo tuliyo nayo.

Nape pamoja na kuitwa vuvuzela lakini hakuwa kituko na wala hakukifanya chama kionekane kichekesho.
​
 
Back
Top Bottom