Askofu Niwemugizi asikitishwa na Kauli ya Humphrey Polepole kuwafananisha Wapinzani na Corona

Askofu Niwemugizi asikitishwa na Kauli ya Humphrey Polepole kuwafananisha Wapinzani na Corona

Corona = Chadema?

Itakuwa alikuwa anatania..hapa hakuna utani kwenye siasa?
Eeenh Heee,

Siku hizi unatandikwa hata risasi huku jamaa akicheka; unaambiwa ni "utani tu"!

Watani, mmoja anamchakaza mwenzie kwa maumivu. Anayechakazwa, yeye ajisikie maumivu yake ni utani. Na hana hata njia ya kuujibu huo utani, hata kwa kulalamika tu!
 
Usiwe serious sana, kuna mwanachema mmoja humu alikuwa anaomba corona ije Tanzania..na bado alijetetea na lengo lake au mawazo yake ilikuwa CCM iathilike, kwa hiyo na huyu kuwafananisha CDM na corona hana tofauti na yule...au mm sijaelewa? Wote hawa wanafanya mzaha na Corona
Polepole kiongozi you zwazwa
 
Naongea Leo hii tarehe 20 mwezi March mwaka 2020, Kwa kauli hii ya dhihaka na kejeli aliyoitoa Polepole, kipindi ambacho virusi vya Corona vitafutika kwenye Ardhi hii ndicho kipindi Polepole atafutika pamoja navyo.

MWENYEZI MUNGU HADHIHAKIWI

Sent using Jamii Forums mobile app
Kizzy Wizzy
Kwa kufanya utani wa dizaini hii kwa kusema kuwa kama tunavyolaani ugonjwa wa korona nchi hi na kuombea utoweke ndani ya nchi yetu...........

Kwa hiyo jinsi tunavyojitahidi kuomba ugonjwa huu wa korona utoweke nchini, vivyo hivyo tunaonba Chadema nayo ifutike ndani ya ardhi ya Tanzania!

Hakika kwa maombi hayo kwa Mungu, majibu yake yatakuja vice versa. Siyo chama cha Chadema kitakachofutika, Bali ni yeye Polepole na Chama chake cha CCM ndivyo vitakavyofutika ndani ya ardhi hii ya Tanzania na kuibakiza Chadema ikipaa katika viwango vingine kabisa
 
Hyo kauli ya polepole Ni ya kijinga Na ya kulaaniwa Na kila mtanzania mpenda umoja Na mshikamano Wa taifa letu...
 
Ukitamzama sana Polepole kuna kitu amepungukiwa. Amekosa hata chembe ya hekima.
Toka lini mtu mpumbavu akawa na hekima?
Huyu jamaa ni takataka,kwani kuwa mpinzani ni tatizo? Mbona hata ndani ya CCM kuna wapinzani...
Halafu akiongea anafikiri anaongea vitu vya maana kumbe ni ujinga mtupu...kwanza hana shule..
Personally siwezi kusikiliza nonsense..basically he has nothing upstairs..

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Nimesikitika sana kusoma maneno kwenye mtandao ambayo sijaamini yamesemwa kweli na mtu ambaye huko nyuma nilimheshimu sana, kwamba, tunaomba Mungu ugonjwa huu uondoke, Corona ni sawa na wapinzani nchini“.

Nikayakumbuka maneno ya Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Mheshimiwa Anna Mgwira aliyosema jana kwenye salamu zake baada ya ibada ya kumsimika Askofu Ludovic Joseph Minde kuwa Askofu wa Moshi.

Alisema kwa kurudia rudia „tusaidieni (viongozi wa dini) kuwatengeneza watu wema wanaoheshimu utu wa watu na haki za watu“. Nimejiuliza hivi kweli hiyo ni siasa safi binadamu kumwona au kumuita mwenzake ni sawa na kirusi cha Corona?

Kumwona binadamu aliyeumbwa kwa sura na mfano wa Mungu ni tusi kubwa kwa Mungu mwenyewe kwamba Yeye Mungu naye ni sawa na kirusi cha Corona, kinachopaswa kuondoka!! Halafu unamwomba huyo Mungu aondoe Corona?!

Hapo ndipo tumefika Watanzania kweli!? Hiyo ndiyo sura ya, siasa ni uadui“. Mtu mnayetofautiana mtazamo au itikadi ni adui, ila kesho akibadili mtazamo akafuata wako anabadilika na kuwa lulu nzuri, rafiki, na binadamu kama wewe.

Jamani! Nawasihi Watanzania tujitahidi kupima maneno tunayozungumza hadharani kumhusu binadamu mwingine.

Mtakatifu Yakobo anasema „Mtu asiyejikwaa katika kunena, huyo ni mtu mkamilifu, anaweza kuuzuia na mwili wake wote kama kwa lijamu“ (Yak 3:2). Na tena, ulimi ni uovu usiotulia, umejaa sumu iletayo mauti“ (3:8).

Namshauri aliyesema Corona ni sawa na wapinzani katika nchi hii kama ni muungwana aombe radhi kwa kumdhalilisha Mungu aliyemuumba binadamu kwa sura na mfano wake (Mwa 1:26-27).

Kwa namna hiyo ataepusha mauti kwa heshima yake mwenyewe na na kwa siasa za kistaarabu.

Source: FB page yake

My take:
1. CCM kutokanusha kauli hii ni sawa na kubariki, ndio tuseme ni msimamo wa chama.
2. Tahadhari wasimtingishe tena askofu na zile saga za uraia na passport
Baba Askofu amesahau maana ya siasa
 
Polepole ni mshenzi tu.Muda si mrefu ARV zitamrukisha ukichaa.Pumbaaaaavu sana yule ndezi.

Sent from my TA-1024 using Tapatalk
 
Askofu anakosea kumuhusisha Mwenyezi Mungu na ujinga wa binaadamu. Nikweli polepole kakosea sana na hatasisi tulimtaka aombe msamaha kuonesha uungwana lkn tusiingize imani humo. Watu huitwa wapumbafu,wachawi,wabaya,malofa,wanangwengwe lkn hatusemi kwakuwa wao ni mfano wake basi naye kaitwa hivyo NO. Mengine yote namuunga mkono Askofu.
 
Polepole mpumbavu aliyelewa madaraka na kudhalilisha wengine.ajitafakari.vyeo vinapita
 
Tazama nchi za wenzetu particularly Italy..namuomba Mwenyezi Mungu awasaidie sana hawa binadamu wenzetu ...pamoja na nchi nyingine zote zinazoteseka na tatizo hili hali ni mbaya sana na haijulikani mwisho wake ni nini ...uchumi wa dunia upo mahali ambapo ni ngumu kupaelezea eti leo anaibuka tu mtu kutoka sijui wapi analeta maneno yasiyo na kichwa wala miguu halafu eti anaitwa kiongozi...hii ni aibu kwa nchi mbele ya dunia nzima...Nimemdharau sana pamoja viongozi wenzake wote...
Naomba niishie hapa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Remote,
Huyo Polepole anayafanya yote hayo kwa kumpendezesha bosi wao ambaye ni "sadist" mkubwa

Kama bosi wake hapendi siasa hizo za chuki, basi tutarajie akemee vikali


Siyo akemee tu, bali amwambie MPUMBAVU NA AMFUKUZE MAKAO MAKUU YA CHAMA.

ASIPOFANYA HIVYO,

AMEMTUMA.
 

Nimesikitika sana kusoma maneno kwenye mtandao ambayo sijaamini yamesemwa kweli na mtu ambaye huko nyuma nilimheshimu sana, kwamba, tunaomba Mungu ugonjwa huu uondoke, Corona ni sawa na wapinzani nchini“.

Nikayakumbuka maneno ya Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Mheshimiwa Anna Mgwira aliyosema jana kwenye salamu zake baada ya ibada ya kumsimika Askofu Ludovic Joseph Minde kuwa Askofu wa Moshi.

Alisema kwa kurudia rudia „tusaidieni (viongozi wa dini) kuwatengeneza watu wema wanaoheshimu utu wa watu na haki za watu“. Nimejiuliza hivi kweli hiyo ni siasa safi binadamu kumwona au kumuita mwenzake ni sawa na kirusi cha Corona?

Kumwona binadamu aliyeumbwa kwa sura na mfano wa Mungu ni tusi kubwa kwa Mungu mwenyewe kwamba Yeye Mungu naye ni sawa na kirusi cha Corona, kinachopaswa kuondoka!! Halafu unamwomba huyo Mungu aondoe Corona?!

Hapo ndipo tumefika Watanzania kweli!? Hiyo ndiyo sura ya, siasa ni uadui“. Mtu mnayetofautiana mtazamo au itikadi ni adui, ila kesho akibadili mtazamo akafuata wako anabadilika na kuwa lulu nzuri, rafiki, na binadamu kama wewe.

Jamani! Nawasihi Watanzania tujitahidi kupima maneno tunayozungumza hadharani kumhusu binadamu mwingine.

Mtakatifu Yakobo anasema „Mtu asiyejikwaa katika kunena, huyo ni mtu mkamilifu, anaweza kuuzuia na mwili wake wote kama kwa lijamu“ (Yak 3:2). Na tena, ulimi ni uovu usiotulia, umejaa sumu iletayo mauti“ (3:8).

Namshauri aliyesema Corona ni sawa na wapinzani katika nchi hii kama ni muungwana aombe radhi kwa kumdhalilisha Mungu aliyemuumba binadamu kwa sura na mfano wake (Mwa 1:26-27).

Kwa namna hiyo ataepusha mauti kwa heshima yake mwenyewe na na kwa siasa za kistaarabu.

Source: FB page yake

My take:
1. CCM kutokanusha kauli hii ni sawa na kubariki, ndio tuseme ni msimamo wa chama.
2. Tahadhari wasimtingishe tena askofu na zile saga za uraia na passport
Kwa kumpa nafasi ya ukatibu mwenezi taifa pole pole, tulichemsha kabisa badala ya kuunganisha chama na wananchi yeye amejipa kazi ya kukitenga chama na wananchi. Hopeless kabisa.
 
Back
Top Bottom