Askofu Niwemugizi: Rais Magufuli aliagiza nirejeshewe Passport yangu na alisema 'Wewe ni Askofu wangu utanizika'

Askofu Niwemugizi: Rais Magufuli aliagiza nirejeshewe Passport yangu na alisema 'Wewe ni Askofu wangu utanizika'

Hapa kuna chai kidogo kwa hiyo alijuaje kwamba yeye atatangulia kufa amuache Askofu kiasi kwamba amwambie yeye ndo atamzika?
Hayo maneno ama kayasema Magu akiwa hoi, au Askofu kapewa ujumbe wa Magu kumbe Magu mwenyewe keshavuta. Ni watu waliandaa mazingira ya mazishi, ili Askofu amwage maombi bila kinyongo
 
Atuambie pia tukio hilo lilimkumbusha nini juu ya kuwa yeye ni kiongozi wa kiroho, jamii na urai na kuhusu uzakendo wa Taifa lake.
Huyo Askofu mbona yuko vizuri sana? Aliweka msimamo hadi Magu karudisha Passport. Huyu siyo Kakobe aliyeubga mkono juhudi ndio wakarudishwa Passport
 
Huyo Askofu mbona yuko vizuri sana? Aliweka msimamo hadi Magu karudisha Passport. Huyu siyo Kakobe aliyeubga mkono juhudi ndio wakarudishwa Passport

Yule aliyesaidiwa kwenye matibabu yake ni yupi?
 
Hapa kuna chai kidogo kwa hiyo alijuaje kwamba yeye atatangulia kufa amuache Askofu kiasi kwamba amwambie yeye ndo atamzika?
Nadhani concept inafahamika mapadri na Wachungaji uongoza ibada za mazishi ndio maana akasema atamzika.
 
Aisee!
Sema mzee baba si ndo vile tena, hata ukimpa makavu hakusikii.

[emoji444][emoji445][emoji444]Nyumba yangu leo, ni chini udongoni
Hakuna mlango,
Hakuna madirisha
Kitanda changu, nalo blangeti langu,
Wameninyang'anya hata senti moja.
[emoji444][emoji445][emoji445][emoji445]
Tuishi kwa upendo.
"Hapa we msafiri"
 
Unatengeneza tatizo halafu unalitatua chap.
Teuzi za kusifu na kuabudu zitakuwepo? Unamsifia kisha anakupa cheo
Pole sana mnyonge, raisi wa wanyonge hayupo tena
kwa hiyo Askofu Niwemugizi anataka ahongwe Passport ili amuzike Magufuli au? Mla rushwa mkubwa
 
Askofu wa Kanisa Katoliki jimbo la Rulenge Ngara, Severine Niwemugizi amesema aliyekuwa Rais wa Tanzania marehemu, John Magufuli aliagiza arejeshewe hati yake ya kusafiria na alimtamkia mara mbili kuwa kiongozi huyo wa kiroho ndiye atakayemzika.

Akizungumza leo Alhamisi Machi 25, 2021 katika Kanisa Katoliki la Bikira Maria Parokia ya Chato, Askofu Niwemugizi ambaye hakutaja muda maalum wa agizo la kurejeshewa hati hiyo, amesema Magufuli aliagiza idara ya uhamiaji kumrejeshea.

"Kwa kweli niwaambie mara mbili, Magufuli aliniambia, ‘wewe ni Askofu wangu utanizika. Mwaka ule 2015 akaniambia hivyo, mara ya pili akamwagiza Kamishna Jenerali wa Uhamiaji anirudishie passport akaniambia wewe ni Askofu wangu utanizika.”

Wasalaamaidi, soma: Askofu Niwemugizi wa Kanisa Katoliki aitwa Uhamiaji kuhojiwa juu ya uraia wake
KWA NINI TUFIKE HUKU KOTE
 
Upepo umevuma kwenda upande mwingine..."Askofu wa Makamanda" leo wamemgeuka!
 
Back
Top Bottom