Askofu Nyaisonga avishangaa Vyama vya Upinzani kususia uchaguzi. Ahimiza waumini kujitokeza kupiga kura na kuchagua viongozi

Shukrani barafu kwa bandiko hili.

Binafsi naona huyo askofu ana matatizo ya kiakili, kama sio kwamba anachanganya dini na siasa.

Uchaguzi huu sio wa jumuiya za kikatoliki, ni uchaguzi wa serikali za mitaa. Na hata ingekuwa wa jumuiya za kikatoliki, sidhani kwamba ni lazima kila mkatoliki ashiriki.

Vyama vilivyo jitoa kushiriki uchaguzi huu ni vichache kuliko idadi ya vyama vya siasa vilivyoko kwenye daftari la msajiri wa vyama vya siasa.

Tumeshuhudia chaguzi nyingi sana lakini siyo vyama vyote vilishiriki, sasa kwanini huu uwe tofauti?!

Ni uchaguzi upi vyama vyooote vyenye usajili vilishiriki?!

Vyama vilivyojitoa havifiki 10, idadi ya vyama vya siasa ni zaidi ya 25, ikiwa vilivyobaki vinashiriki uchaguzi tatizo liko wapi?!

Kwanini wanaumia vyama kujitoa, mbona tumeshuhudia chaguzi ndogo kadhaa mshiriki akiwa ni ccm pekee na matokeo yamekubalika?! Mfano kule jimbo alilotoka Tundu Lisu na hata kule alikotoka Nasari. Walishiriki ccm peke yao na hakukuwa na tatizo, kwanini sasa ionekane ni tatizo?!

Kabla ya vyama vingi ccm waliendesha chaguzi hizi na hakukuwa na shida, kwanini wasifanye vivyo hivyo na wakaendelea na maisha yao ya siasa?!

Nahisi walitengeneza hili tatizo kwa makusudi fulani, sasa makusudio yao yameshindwa kutimia wanatafuta sababu nyingine ili kutimiza adhima yao.
 
Kuna nchi fulani kanisa lilitoa matamko wakati wa watu kudai demokrasia Mkuu wa Kanisa aliingia matatani huko The Hague sasa na ninyi endeleeni msiseme hatukuwaambia.
Mnabariki dhuluma ukatili kwa kumwabudu na kumsifia mwanadamu mwenzenu mwenye mapungufu mengi kiroho sijui mtamwambia nini Mungu mkifika kwake!
 
Wanashindwa kutambua ni kuwa wanachi wenyewe wanajiongoza kwa migomo pasipokumsikiliza yeyote labda niseme nisawa na kumsukuma mlevi.
 

Mkuu hili ulilolosema liko wazi na ni ukweli mtupu. Wangalau KKKT ndio wamebaki upande wa haki, hao RC wameamua kusimamia upande wa uovu ili kupata faida binafsi. Nadhani huko makanisani kuna mabox ya maoni, ni vyema hiyo kauli ikapigwa kwa nguvu zote na waumini.
 
Huyo siyo mtumishi wa Mungu aliye hai, Bali anslitumikia tumbo lake

Kwa kuwa Mungu ninayemwamii Mimi anahubiri kutenda haki.....

Hivi kweli katika huu UCHAFUZI unaotegemewa kufanyika tarehe 24 mwezi huu, hivi kweli hata nafsi zenu haziwasuti mnaojiita watumishi wa Mungu??
 
Yeyote mwenye akili timamu atashangaa!
 
Mbona hili kanisa halikujitokeza kuhamasisha waumini wakajiandikishe kupiga kura?!

Leo wanawahamasisha wakapige kura vipi ikiwa hawakujiandikisha?!

Kura wanapiga za nini ikiwa mgombea ni mmoja?!
 
Siamini kama kanisa langu ndilo lililoamua hivyo.ina maana kanisa halikuona kabisa jinsi wagombea wa upinzani walivyoenguliwa?Kwa nini halikuishauri serikali kutumia busara wakati huo?ingelikua enzi za mkwele sasa hivi ungeshatoka waraka wa kichungaji na kila jumapili mahubiri yangekua ni serikali kuharibu uchaguzi Mkuu.
 
Kumbuka Askofu Ruwaichi alitumiwa ndege kumchumkua huko KCMC Hospital na kumleta hapa Dar kupata matibabu kwa maelekezo ya rais. Katika mazingira hayo unategemea kanisa la Roma liwe upande wa haki au la wanaowalinda viongozi wake?

Wote ruwa na nyai ni watu wa tiaisies!!
 
Huyo askofu kada Mbona akutoa neno juu ya maagizo ya watendaji kuzikimbia ofisi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…