Askofu Nyaisonga avishangaa Vyama vya Upinzani kususia uchaguzi. Ahimiza waumini kujitokeza kupiga kura na kuchagua viongozi

barafu nataka nikuhakikishie tu kanisa katoliki lina intelijensia yake yenye ufanisi wa hali ya juu.
Kanisa linajaribu kupunguza athari za tatizo badala ya kumwagia mafuta kwenye moto.

Wameona kilicho nyuma ya pazia juu ya kosa hili kubwa la kuvuruga uchaguzi kizembe kwa wale wenye dhamana, na jinsi upande wa pili wa wapinzani wa wenye dhamana walivyo itumia vizuri fursa hii kutaka kupitisha ajenda ya kulivuruga taifa.

Hatuwavui lawama waliovuruga uchaguzi, lori linakata breki mteremkoni.
Lakini tuwe makini waliomuondoa Ghadaf, walio umizwa na kuzuiwa kupora rasilimali zetu, walio zuiwa ulaji wameiona vizuri fursa waliyopewa na watu wenye dhamana kwenye sahani ya fedha.

It doesn't take Solomon's wisdom to know The Trojans (In this case The Authority) are wrong, and they have pulled a wooden Horse from the Greeks into their city.
What scares me is how the opposition takes it as blessings, without knowing they are tracing the footprints of the Libyan revolutionists..

Kudhania kuvuruga uchaguzi wa serikali za mitaa ni ushindi kwa wapanga mikakati, na ile kujitoa uchaguzi wapinzani ni kama kupewa zawadi ya ushindi na wapinzani dhaifu ni kujidanganya, hiki ni kisa cha TROJAN HORSE.
God forbid ....
NAIPENDA NCHI YANGU NAWAKOSOA KWA HESHIMA, ADUI NI YULE ANAE NYAMAZA ANASUBIRI MAJANGA ASEME "NILIJUA HAYA KABLA" BAADA YA MABAYA KUTOKEA.
Tumkumbuke Nyerere katika ujumbe wake wa tujisahihishe.
 
Uzuri ni kuwa watanzania wote si wafuasi wa huyo corrupt "afkoti"
 
Mahusiano na mafungamano yangu na Kanisa Katoliki Tanzania yamesimamishwa rasmi kuanzia hivi sasa. Kanisa Katoliki halikuwahi kutoa kauli za hovyo na zisizo na mashiko kwa kiasi hiki.
Wanaongelea upinzani kukaa na serikali utadhani hawaini kinachoendelea nchini? Serikali yenyewe imeshindwa kukaa pamoja, upinzani utawezaje wakati unachukiwa na kuonekana kama vile ni waasi na mbaya zaidi wamepigwa marufuku kufanya shughuli zao za kisiasa??
Nilitaraji wangekua na hoja za maana katika tamko lao, wameokoteza mtu tepwete kabisa eti ndiyo awe rais wa baraza ili tu kufanya na kutenda yale watawala wanayoyataka?. Pumbavu kabisa!
Alikuwa wapi huyo Ask8fu kutoa kauli wakati wapinzani wanaengulia kwa fitina na sababu zisizo na mashiko?? Yaani kasubiri wapinzani wamechukua hatua zao tena kwa amani tu eti anaanza kuwashambulia!,
 
Huyo askofu kweli ana akili timamu??

Hivi chama chako kinaenguliwa wagombea wako zaidi ya asilimia 95 na wapinzani wako CCM wagombea wake wote asilimia 100 wanaonekana kuwa ndiyo waliojaza sahihi hizo fomu!

Hivi huyo askofu anakuwa na ujasiri kweli wa kuvilaumu vyama vya upinzani kwa kususia huo UCHAFUZI??

Hakika katika awamu hii ya utawala, hata hao wanaojiita watumishi wa Mungu wamewekwa mfukoni!
 
Ubarikiwe sana kwa andiko hili. Wakati wa ibada kubwa kule Brazil iliyoendeshwa na Papa mwenyewe, Papa alisema, siku zote Kanisa linatakiwa kusimama na watu wa kawaida, watu maskini na siyo na watawala au matajiri. Yeye mwenyewe kwa kuonesha mfano, hata ibada yenyewe alifanyia kwenye viunga vya watu maskini, maeneo ambayo yaliaminika ni maeneo machafu, maeneno yaliyojaa uovu, maeneo ya wavuta bangi na watumiaji wa madawa ya kulevya.

Lakini kama watu wenye imani, tunatakiwa kufahamu kuwa shetani ana nguvu, na yupo kwenye ngazi zote. Shetani anaweza kutenda kazi kupitia Papa (kuna wakati Kanisa katoliki liliongozwa na mapapa wa ajabu, na mwingine aliwahi kuuawa na waumini altareni kwa kukabwa koo), Makadinali, Maaskofu, Mapadre, wachungaji, n.k. Tuyaangalie matendo na maneno yao, kisha tujiulize, ananena yaliyo ya Mungu au ya shetani? Tusiangamie kwa kukosa maarifa. Tukigundua anayonena kadinali, Askofu au Padre au Mchungaji ni ya shetani, lazima tujitenge naye. Mungu wa kweli hana ushirika na shetani.

Kwa wale wakatoliki, baadhi wanafahamu zile siri za Fatima. Hasa ile iliyotolewa mwaka 1980. Siri ile inasema, kuanzia mwaka 1980, shetani atatenda kazi zaidi kupitia kwa viongozi wa dini. Watu wengi wataangamia kwa vile watayatekeleza wanayoambiwa na viongozi wao, wakiamini ni ya Mungu, kumbe ni ya shetani.

Kwa waumini, chungeni sana imani zenu, msiwe mbumbumbu wa kusaidiki na kuamini na kutenda kila mnachoambiwa na viongozi wa dini. Tafakarini, pimeni, chambueni na ombeni msaada wa Mungu ili kutambua kuwa mnayoambiwa yanatoka kwake, yana baraka zake au watu wanalitumia jina lake kufanikisha mipango ya shetani.
 
Well said. Ni vigumu kuamini kuwa hili ni lile Kanisa lililosimama na wananchì kudai katiba ya wananchì na kutangaza hadharani kuikataa katiba pendekezwa. Kwa msimamo huu wa Kanisa kwanini baadhi ya watu wasiendelee kuamini kwambà JK alipata upinzani kutokana na dini yake? Mwana JF mmoja majuzi aliandika kuhusu ukimya wa Kanisa katika kadhia hii ya uchaguzi wa serikali za Mitaa. Alidai kuwa kuna tetesi kuwa rais wa TEC wa sasa amechaguliwa mahsusi kuwa kiungo Kati ya Kanisa na utawala ambao unaonekana kuwa tofauti (erratic?) na nyingine zote zilizotangulia. Sikuamini kuwa madai hayo yana ukweli kutokana na misimamo ya Kanisa katoliki katika mambo ya msingi kuhusu jamii ya miaka ya hivi karibuni. Hata hivyo inaelekea madai hayo yana ukweli kwani kwa hili la uchaguzi wa Serikali za Mitaa tumedhihirishiwa bila shaka yoyote kuwa nia ya serikali yetu ya sasa ni ovu sana na haitaki kabisa demokrasia.
 
Je namba moja angekuwa "ostaz" unadhani RC wangetoa tamko la namna hii? Thubutuu.
 
Kanisa katoliki lifunge mdomo. Kule Rwanda walihusika na mauaji ya kimbari kwa 100% hadi pope wao aliomba msamaha. Wasitake kugombanisha watazania kwa sababu za siasa. Wao wahubiri dini na wawaache wanasiasa wahubiri siasa. Baba Askofu tunakuheshimu sana. Tafadhali rudi madhabahuni. Kama unataka siasa vua joho tujue moja
 
Huku nikutudhalilisha wakatoliki

Yaani nasikia aibu sana mimi kuitwa mkatoliki

Hawa viongozi hovyo sana.

Badala ya kukemea maovu, wanakumbatia waovu

Wakapige wao mapadre mimi nafamilia yangu marufuku
Kwa kweli Kanisa Katoliki, viongozi wetu wanatuabisha. Inakuwaje kwa kanisa lenye waumini mamilioni, kenye maaskofu lukuki, wafikie kumchagua Rais wa TEC kwa kuangalia ushahiba wake na mtawala?
 
Mimi naamini Mungu yupo ila sio kupitia makanisa au misikiti

Hivyo Nyaisonga wala hanipi shida kuunga mkono udhalimu
 
Naunga mkono 100% kauli ya baba Askofu Nyaisonga!
Ndio maana niliacha kuhudhuria kanisani baada ya kutambua hawa maaskofu uchwara wapo pale ili kujipendekeza kwa sirikali na kunenepesha mitumbo yao. Pumbafuuuuu kabisa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…