Askofu Nyaisonga avishangaa Vyama vya Upinzani kususia uchaguzi. Ahimiza waumini kujitokeza kupiga kura na kuchagua viongozi

Nimefutilia mbali michango ya mwisho wa mwaka niliyokuwa nipeleke kanisani kwangu, aidha kwa dhati ya moyo wangu najiweka kando na kanisa hilo na mambo yake yote kwakuwa "KANISA LIMETENDA DHAMBI YA MAUTI" Kanisa limejilaani na limelaanika! Siwezi kuwa sehemu ya kanisa katoliki la Tanzania lililomuelekea SHETANI! Kanisa lililofungamana na shetani likae mbali nami!
 
Hawa mapadre na maaskofu kama dhambi hii ya wazi wameifuata basi naanza kuwaelewa wale wanaowatuhumu kwa ulawiti na zinaa dhidi ya wake za watu na watoto!
 
Kwani halipo? Tuache akili za mbuni, hilo tatizo lipo, la miaka mamia na sugu.
Ungelizungumzia tena kwa juhudi kubwa wakati mwingine kabla ya tukio hili la sasa.
Kulichomekea sasa ni kuchochea moto mkubwa.
Waathirika ni dini zote.
 
Hawa mapadre na maaskofu kama dhambi hii ya wazi wameifuata basi naanza kuwaelewa wale wanaowatuhumu kwa ulawiti na zinaa dhidi ya wake za watu na watoto!

Maneno mazito haya
 
Serikali msiige ushauri uchwara huo.mkija baniwa hela na uomba ombawenu huo mtageukia kuliomba kanisa
 
Safari ni ndefu
 
You are in deep denial my friend: An unholy Union between The Church and The State has always been an epicenter of human misery from the Times An Evil Treaty of Torde-Silas was signed, going to the times of Napoleon Bonaparte up to the dawn of fascism in Europe.

Remember it was the Pope that gave a nod to Prince Henry the Navigator to institute slavery and colonialism, despicable acts which subjected an entire Africa into shackles of poverty.
 
Sasa mpaka askofu kaona haki imetendeka, na askofu ana maono na roho mtakatifu
Siyo huyu kama aliyewekewa ubongo wa bandia, KATIKA operesheni yake. Anawataka wapinzani wakae meza moja, hivi kwa akili timamu kwa muda na jinsi Jafo na team yake walivyojipanga, HILI LINAWEZEKANA?
 
Askofu amewapa somo Kazi kwao. Maaskof wameona mbali mno

ASKOFU NYAISONGA ANAYEONGOZA TEC NI MATEKA WA ITIKADI YA UBWANA-NA-UTWANA ILIYOASISIWA TANGU ENZI ZA UTUMWA WA MISRI NA BABELI NA KUBARIKIWA NA SHERIA ZA KANISA KATOLIKI ZINAZOTUNGWA NA VATICAN


Askofu Nyaisonga (pichani), ambaye ni Mwenyekiti wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), ameripotiwa na vyombo vya habari akiwahimiza Waumini Katoliki kwenda kupiga kura siku ya 24 Desemba 2019, bila kujali kwamba kuna vyama vya siasa nane ambavyo tayari vimetangaza kujitoa katika uchaguzi huu wa serikali za mitaa wa mwaka 2019.

Ametoa kauli hizi wakati ambapo, zaidi ya 99% ya wagombea wa CCM wamepitishwa bila kupingwa, baada ya wagombea wa upinzani ama kukatwa au kunyimwa fursa ya kuchukua na kurudisha fomu kwa wasimamizi wa uchaguzi. Mchakato huu unamaanisha kuwa, wananchi hawatapata fursa ya kuamua juu ya sera na viongozi wanaowataka kwa ajili ya serikali za mitaa. Wananchi wamegeuzwa watumwa ndani ya nchi yao.

Hivyo, ni wazi kuwa, kauli za Askofu Nyaisonga juu ya uchaguzi zinamweka kundi moja na watu wanaoongozwa na mtazamo wa dunia wenye msingi wake katika itikadi ya ubwana-na-utwana (master-slave ideology). Mtazamo huu unapatikana katika Sheria za Kanisa Katoliki (1983) fungu la 536(2). Tunasoma:

"A pastoral council possesses a consultative vote only and is governed by the norms established by the diocesan bishop."

Kanuni hii imefafanuliwa katika ibara ya 5.2 ya waraka wa Vatican (1997) uitwao “Instruction on certain questions regarding the collaboration of the non-ordained faithful in the sacred ministry of priest,” kama ifuatavyo:

"Diocesan and parochial Pastoral Councils and Parochial Finance Councils, of which non-ordained faithful are members, enjoy a consultative vote only and cannot in any way become deliberative structures.”"

Hivyo, kwa mujibu wa fungu hili walei ni watumwa wa makleri. Yaani, fundisho kwamba, walei wanayo kura yenye nguvu ya ushauri pekee ("consultative vote only") wakati makleri wanayo kura yenye nguvu ya uamuzi (deliberative vote) pia.

Na kifalsafa, mtumwa ni mtu asiye na uamuzi, mtu asiye na kauli. Anaelekezwa na kutekeleza na mtu mwingine aliye juu yake ama kama mkoloni au mmiliki wake.

Bahati mbaya itikadi ya ubwana na utwana imepitwa na wakati. Enzi za utumwa zimepita, hata kama bado Biblia inaongelea "mtumwa mwema" na "mtumwa mwenye faida."

Hivyo, ni walei wachache sana bado wanaikubali itikadi ya "consultation-deliberation dualism" inayokumbatiwa na sheria za Kanisa Katoliki.

Hivyo, uasi unaotokea Parokia ya mt. Mikaeli Kawe dhidi ya kina Padre Kundy na Parokia ya Kijitonyama jijini Dar ni ushahidi tosha kwamba Waumini Katoliki sasa wanataka ukombozi dhidi ya ukoloni unaotekelezwa kupitia mfumo wa hiarakia ya Kanisa Katoliki.

Uasi huo utaendelea kuwatikisa makleri mpaka hapo watakapokubali kuheshimu hadhi ya ubinadamu tuliyo nayo kwa usawa.

Kwa mujibu wa ibara ya 536 ya Sheria za Kanisa Katoiliki, ndani ya Kanisa hilo kuna "consultative democracy" na hakuna "deliberative democracy."

Chini ya "consultative democracy" ndani ya Kanisa Katoliki, kuanzia kwenye Jumuiya Ndogo Ndogo, wapiga kura wanaishia kwenye ngazi ya "kura ya maoni" na kusubiri "kura ya uamuzi" kufanywa katika ngazi za juu, kama vile parokiani, au Jimboni, au huko Vatikani.

Lakini, chini ya "deliberative democracy," inayotamkwa katika katiba ya Tanzania ya 1977, wapiga kura hushiriki, sio katika "kura ya maoni" pekee, bali katika "kura ya uamuzi" pia.

Uamuzi wao ni wa mwisho, na hauwezi kutenguliwa na mtu mwingine yeyote kwa mujibu wa sheria. Hii maana yake ni kwamba, kwa mujibu wa sheria za nchi yetu, wananchi wanayo haki juu ya kitu ambacho katika political philosophy kinaitwa "the right to deliberative justification of policies and leadership."

Sheria za Kanisa Katoliki hazitambui kitu hiki. Hivyo, Askofu Nyaisonga hana msaada mkubwa katika hatua hii ya uchaguzi inayohusu "kura ya uamuzi" katika uendeshaji wa nchi-dola inayoitwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Nchini mwetu, kimekuwa na ukiukwaji mkubwa sana wa "procedural rights" katika mchakato wa uchaguzi wa sasa. Na kwa sababu hiyo hatuwezi kutegemea kwamba, huko mbeleni "substantive rights" zitabaki salama.

Ma-DC, ma-DED, ma-WEO na ma-VEO ndio wanapindisha haki hizi ninazoziita "procedural rights." Wamekuwa wanafanya hivyo kwa miaka minne sasa. Wakaona hata "watu wa Mungu" wako kimya, na kwa sababu hiyo sasa wame-overdo!

Just imagine, katika wilaya kama Karagwe, ndani ya vijiji 78, wagombea wa upizani katika ngazi ya uenyeviti wa kijiji wamekatwa isipokuwa wanne tu. Na katika ngazi ya vitongoji, kati ya nafasi 630, wote wamekatwa isipokuwa 18 pekee.

Halafu, kina Nyaisonga wanapanua vinywa vyao na kuwambia wananchi wa Karagwe wasonge mbele na uchaguzi ifikapo 24 Novemba 2019.

Ni uchaguzi gani huu wakati ma-CCM yamekwishajichagua na kujaza nafasi zaidi ya 90%? Hapo kuna deliberative democracy kweli? Watu wanaweza kupata fursa ya kuhoji kwa ufanisi sera na wagombea wanaozinadi sera hizo? Hapana!

Hivyo, ni lazima tuseme "BIG NO" kwa tamko la TEC kupitia kwa Askofu Nyaisonga na wenzake.

Askofu Nyaisonga arudi darasani kujifunza juu ya demokrasia ya vyama vingi katika nchi ambayo ni Jamhuri ya kidemokrasia kama ilivyo Tanzania. Muda wa kuishi katika dola zinazoendeshwa kitemi, kichifu na kinyemela zimepita.
 
Ajitokeze yeye na familia yake, Shenzii sana🏃🏻🏃🏻🏃🏻
 
Mahtma Gandhi once said "I love the God of Christians but i hate Christians"
 
Ni aibu kanisa(viongozi wa kanisa) limesaliti waumini wake, ila nina uhakika msimamo wa uongozi wa kanisa na msimamo wa waumini si lazima viwe sawa.
Hawa si kama wale waumini wa Gwajiboy, Kakobe and the likes, they think, reason and decide independently.
 

Fvck him!
 
Wanadamu viumbe wa ajabu sana. Akihimiza watu/wananchi wakapige kura kwenu ni sawa,huyo huyo kesho akiwakemea mtasema ooh asichanganye siasa na dini.
Tatizo waafrika tuna ubinafsi mwingi maslahi binafsi na unafiki mwingi.
 
Nimesikiliza mahubiri ya Askofu Mkuu na Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tz,Mhashamu Askofu Nyaisonga,
Hayo bado ni Mahubiri tu tusubiri Tamko la baraza hivyo tujiandae kwa yanayo kuja
 
Fungu hili linasema kuwa walei ni watumw wa makleri.



Bahati mbaya itikadi hii imepitwa na wakati.

Ni walei wachache sana bado wanaikubali.

Uasi unaotokea parokia ya mt. Mikaeli kawe na parokia ya kijitonyama jijini dar ni ushahidi tosha.

Mkuu itakuwa umechanganya mgogoro wa Parokia ya Mt.Mikaeli haitokani na sababu ulioanisha hapo juu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…