Askofu Nyaisonga avishangaa Vyama vya Upinzani kususia uchaguzi. Ahimiza waumini kujitokeza kupiga kura na kuchagua viongozi

Huku nikutudhalilisha wakatoliki

Yaani nasikia aibu sana mimi kuitwa mkatoliki

Hawa viongozi hovyo sana.

Badala ya kukemea maovu, wanakumbatia waovu

Wakapige wao mapadre mimi nafamilia yangu marufuku
lazima atakuwa raia wa nchi jirani kwahiyo anataka kuchomoa betri
 
Hakuna cha intelijensia wala upuuzi mwingine wowote. Huyu amesukumwa na urafiki wake binafsi na mtawala. Na hili tamko kwa vyovyote ni lake yeye binafsi na syndicate yake.

Huyu Askofu, analinajisi Kanisa Katoliki.
 
Huyu askofu anaonekana ni mtu wa system, na mimi kama mkatoliki asilia napingana naye na nitachochea uasi dhidi ya maaskofu vibaraka kama pengo nk. Sitatoa hela yangu tena kama Dhaka, mavuno nk ila siwezi kuhama kanisa sababu najua kanisa ni safi ila kwa sasa linaongozwa na viongozi wabovu
 
Nitaendelea kusali kanisa katoliki. Sadaka na zaka yangu nitaitoa kwa watu maskini wasiojiweza.
 
Kumbuka Askofu Ruwaichi alitumiwa ndege kumchumkua huko KCMC Hospital na kumleta hapa Dar kupata matibabu kwa maelekezo ya rais. Katika mazingira hayo unategemea kanisa la Roma liwe upande wa haki au la wanaowalinda viongozi wake?
.... unataka kusema kanisa katoliki halikuwa na uwezo wa kumsafirisha Ruwaichi?!, au kuna mtu mwingine alietumia hilo gap kwa manufaa yake?, kama tulivyooneshwa kwa mussolini, au hujasoma story yote!
 
....nimekusoma vizuri sana na nimekuelewa, mimi pia ni Mkatoliki 100 percent, jamaa sometimes wanatufanya watoto hatuna akili, yaani wanakera sana kwa kukurupuka kwao kusikokuwa na maana, ili iweje, umfurahishe huyo ili iweje?, hawa watu wanatuboa sana waumini wao.
 
Safisana askofu hakika uliyoyasema ni mfano wa kuigwa kwa viongozi wa vyama vya siasa!kuliko kususa wangekaa meza moja na serikali! Ubarikiwe Sana baba askofu
 
Waraka mmeusahau?
 
Hakuna cha intelijensia wala upuuzi mwingine wowote. Huyu amesukumwa na urafiki wake binafsi na mtawala. Na hili tamko kwa vyovyote ni lake yeye binafsi na syndicate yake.

Huyu Askofu, analinajisi Kanisa Katoliki.
Haya ni maoni yako na mimi ninayo yangu, si wote tunapigania demokrasia itakayo tupa uhuru wa maoni n.k?
 
... hope this is the case, then be it!, but not otherwise..
 
Acha wivu ulitaka askofu asemeje tatizo mnapenda hii nchi tuingie vitani !mbona Kama kiongozi wa kiimani ameongea vizuri kabisa
 
Kwa kweli Kanisa Katoliki, viongozi wetu wanatuabisha. Inakuwaje kwa kanisa lenye waumini mamilioni, kenye maaskofu lukuki, wafikie kumchagua Rais wa TEC kwa kuangalia ushahiba wake na mtawala?

Hiyo inaonyesha kwa sasa kanisa la RC limepoteza mwelekeo na ndio maana waumini wake wanazidi kwenda kwenye makanisa ya kiroho, wamechoka kuona mapadre na maaskofu wakiwa na familia huku mitaani wakati wanajifanya hawaoi. Kwa ujumla hilo kanisa kwa sasa linapaswa kujitafakari kwani limegeuka kuwa kanisa la mtaani. Sasa ngoja waone idadi ya watu itakavyokuwa ndogo ndio wajue hata hilo kanisa limepuuzwa.
 
Acha wivu ulitaka askofu asemeje tatizo mnapenda hii nchi tuingie vitani !mbona Kama kiongozi wa kiimani ameongea vizuri kabisa

Huyo kiongozi wa kiimani hajaongea vizuri, bali ameamua kushiriki uovu.
 
.... unataka kusema kanisa katoliki halikuwa na uwezo wa kumsafirisha Ruwaichi?!, au kuna mtu mwingine alietumia hilo gap kwa manufaa yake?, kama tulivyooneshwa kwa mussolini, au hujasoma story yote!

Nimemaanisha huyo aliyemsafirisha alitumia hiyo fursa ili kulifumba macho kanisa, na sasa kanisa linalipa fadhila.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…