Askofu Nyaisonga avishangaa Vyama vya Upinzani kususia uchaguzi. Ahimiza waumini kujitokeza kupiga kura na kuchagua viongozi

Mwezi February kanisa katoliki lilitoa waraka watu wajiandikishe uchaguzi.

Mbona hili kanisa halikujitokeza kuhamasisha waumini wakajiandikishe kupiga kura?!

Leo wanawahamasisha wakapige kura vipi ikiwa hawakujiandikisha?!

Kura wanapiga za nini ikiwa mgombea ni mmoja?!
 
Kasome historia ya vita za Yerusalemu,dark ages na mauaji ya wakristo ulaya,uongozi wa madikteta ka Musolini na Hitler,mauaji ya wayahudi Ujerumani,Rwandan genocide,Ireland crisis,utawaelewa vizuri viongozi wa kikatoliki.Ni watu very controversial yanapokuja mambo ya aina hii na mara nyingi husimama na upande wenye nguvu.Ni wanafiki na nyoka wabaya.Pole kwa waumini wao.
 
Kabisa, usisahau mambo mema kama kumuunga mkono kuchinja na kupora mali za Wayahudi zaidi ya elfu nane na kuwapeleka Borgo San Dalmazzo Camp na Fossoli ili Kanisa lipewe mji wa Vatican.
Ninafikiri Kanisa Katoliki liliunga mkono mambo mema pekee.

Hata leo, kuna mambo hayaendi sawa katika awamu tuliyonayo. Lakini haimaanishi kuwa hakuna mambo mema mengi yanayotendeka.

Kwa mtazamo wangu; busara ni kuunga mkono hayo mema na kutumia njia nzuri kukosoa mapungufu. Ukosoaji huu sio lazima uwe public.

Tufanye kususia uchaguzi; what will be our next plan?
 
Vipi kuhusu DRC na Kabila?
 
Kuna tatizo hapo.
Na ukiona hivyo tunaelekea kubaya sana.
Kama kuna waumini humu wa Kanisa hilo wamwambie kabisa huyo askofu wao kuwa amebariki dhulma katika Taifa hili.
Dhulma siku zote unaishia kwenye vurugu,ghasia na mwishowe vifo vingi.

Siku zote nilikua sijaelewa kuwa ni kwa nini Viongozi wa Dini hasa wa kanisa Katoliki wamekua wakihusishwa na vita za kimbari sasa nimepata jibu .
Askofu anaposimama upande wa Mdhulumaji mwenye nguvu zote kama Mabunduki ,majeshi na kila aina ya mabavu na kumwacha mlalamikaji asiye na nguvu basi amebariki ugandamizaji.Matokeo yake mlalamikaji dhaifu hata akijaribu kuandamana ataishia kupigwa risasi na hata kumwagiwa kemikali za sumu na kufa kama Panya. Mwishowe mlalamikaji mnyinge ataamua kujitetea dhudi ya binadamu mwenzake anayeamua kumuua na kumwona kama sisimizi.Hapo vita inaingia ya kimbari na wenyewe kwa wenyewe . Chanzo ni viongozi wa dini waliosimama upande wa Wenye nguvu dhidi ya wanyongo na dhaifu.

Lakini kama askofu angesimama na wanyonge angeepusha vurugu na kuuawa kwa wanyonge mana wenye nguvu wangejichunguza na kuona makosa yao na kuwatendea haki wanyonge.

Waafrika tumeamua kutumia kila mbinu za kikoloni kutawaliana kimabavu kwa faida ya watawala na dini viongozi wa dini za kikoloni.
Ubeberu umehamia kwa watawala.

Nadhani watakua wanapata migao ya mafungu ya dhulma yanayopatikana nje ya bajeti.

Lakini tuwalaumu viongozi dhaifu wa upinzani wasio na weledi na Elimu ya siasa kama alivyodai.

Chadema ndicho chama tegemeo la Watanzania lakini Mbowe amevuruga Chama hakina dira wala uongozi mpaka sasa.
Chama hakina Intelijensia ya kutosha.
Chama hakitumii fedha kujenga Chama ngazi za chini zaidi ya kumlinda Mbowe na maslahi yake.
Wasomi ndani ya Chadema wamejitenga na Chama na wamekaa kimya.
Hata Lisu ameamua kukaa kimya mana anaona anahatarisha maisha yake kwa manufaa ya Mtu Mmoja Mbowe na Mali zake .
Akili kubwa kama Komu inawekwa pembeni kwa sababu ya akili ndogo.
Komu ni kati ya wasomi wenye uwezo mkubwa sana kiakili na anauwezo wa kupambanua mambo na uwezo wa kubadili mwelekeo wa siasa za Tanzania kwa kuja na mbinu mpya.

Kubenea amewekwa kapuni ,MTU mwenye historia ya kuichachafya serikali mpaka akataka kupoteza maisha yake. Akisema tunaletewa hadithi za Mbowe amepoteza Mali zake wakati anapewa stahiki yake ya kukwepa Kodi . Ufisadi wa Mbowe wa kukwepa kodi umekigharimu chama. Na hawezi kuachia uongozi mana anaishi kwa ruzuku za Chama ili afidie hasara alizopata kupitia siasa.
Wenzake wamenusurika kuuawa kwa akili ya Chama lakini wanatumikia Chama nje ya madaraka lakini Mbowe ameguswa kwenye kodi na ufisadi wake analia lia na kusema akiondoka chama kitakufa wakati anakiua mana chama kinakosa dira.

Wapo watu jasiri wasio hofia mali zao wala maisha yao kama alivyo Lema, Heche,Juma Mwalimu, Msigwa ,Esta Matiku n.k Lakini bado tu Chama kina mkumbatia Mbowe na usanii wake.
Hapo kweli Chama hiki kitategemea Kauli toka kwa Kanisa Katoliki.?? Kweli ??? Are serious ???
Komu amesoma na Mapadri wengi na walikua wanamheshimu kwa Uwezo wake aliokua nao Darasani. Hata Mkuu Fulani wa taasisi nyeti anamfahami vilivyo Komu alivyokua anawachachafya kule Seminary. Leo anakimbizwa na wawekezaji wa kisiasa.

Hata hivyo siungi mkono kauli ya Askofu kwa sababu hata kama wapinzani wangeshiriki uchaguzi hali ingekua ni hiyo hiyo mana CCM wangekata rufaa na kuwaengua wote hata kama wangeshinda mana wameshaelekezwa kosa lilipo kuwa ni majina ya Vyama na kwa mtego hawakusema kuwa form zijazwe upya Bali waruhusiwe kugombea. Mtego ulikua hapo bado.

Lakini pia ukimfumania mpishi anataka kukuwekea sumu kwenye chakula huwezi kukubali kuendelea kupikiwa chakula na mpishi huyo huyo eti kwa sababu chakula kimemwagwa.

Wapinzani wajichunguze.
Serikali ijichunguze.
CCM ijichunguze.
Wananchi wajichunguze.
Kanisa Katoliki lijichunguze kama limesimama katika haki au upande wenye dhulma na nguvu ya fedha na mabavu?
 
Kabla ya yote lazima ujiulize katika viongozi wa vyama vya upinzani walioazimia kususia uchaguzi umemwona MTU mwenye uwezo wa kutoa hoja ya kulishawishi kanisa Katoliki . Kanisa lililofungamana serikali tangu enzi na enzi.
Lazika pawe na mtu anayejua filosofia ya Kanisa na mtizomo wake ili aweze kutoa hoja zenye kuweza kulishawishi kanisa hilo kwa mapana yake.
Vyama vyenye nguvu vijifunze kupata viongozi wanye maono mapana yanayoweza kujichimbia mpaka ndani ya kanisa Katoliki na sio kubaki kulia lia tu wakati wanajua wazi kuwa kanisa hilo tangu ukoloni lina ndimi mbili.
 

Nimeumwa ghafla. Sijui nikapime kipimo gani. Siendi tena kanisani. Mitabaki na machozi ya ndugu zangu yeye na ulatili aliousifia ataukuta jehanamu. Shetani andaa kuni au mkaa wa kutosha. Ikiwezekana weka gesi ya kutosha.
 
'ujiulize katika viongozi wa vyama vya upinzani walioazimia kususia uchaguzi umemwona MTU mwenye uwezo wa kutoa hoja ya kulishawishi kanisa Katoliki'.

Uzuri wananchi wanajionea figisu zinazofanywa na watawala so hakuna hata haja ya wapinzani kutoa hoja zozote za kulishawishi kanisa katoliki.
 
Mimi niliyasikia haya wakati wa kipindi cha kumpata Rais mpya wa TEC. Jambo la kujiuliza, hivi hizi dini zetu zipo kwaajili ya imani au maslahi fulani? Ni dini au watu fulani ndio wanaozifanya dini kuwa syndicate ya matakwa binafsi ya watu fulani?
Mkuu kwa nini unajipa jakamoyo?hamia mito ya baraka au mlima moto,yesu ni yule yule tu
 
Wapinzani wamenusa tu kushindwa suala la kususa ni geresha
Eti UPDP nao wamesusa,sijui hata kama wana kiti hata kimoja katika mitaa yote nchi nzima
 

Mm sio msemaji lakini kwa kauli hii ya huyu askofu tutawaumbua. Hawezi kutetea watu wanne wakati mamilioni wanateseka. Niko tayari kufa na kuteseka jamani. Baba mtakatifu tunakuita nenda Tanzania kaangalie vilio vya watoto wako.
Na mimi ni mkatoliki lakini maweza kuwa na ushawishi duuu!!!!!!!. Jiwe kila mahali anarushiwa stone hata duniani na mbinguni hafai.

Baba nyoosha mkono wako (Il tuo lemani beneffici signore) sisi baba bado tunakupenda ndio maombi yetu.
 
haki ni ku support unachokitaka wewe?
Kumbuka Askofu Ruwaichi alitumiwa ndege kumchumkua huko KCMC Hospital na kumleta hapa Dar kupata matibabu kwa maelekezo ya rais. Katika mazingira hayo unategemea kanisa la Roma liwe upande wa haki au la wanaowalinda viongozi wake?
 
Anza kwa Ngwajima patakufaa..
Usisumbuke kuona aibu. tuko powa
Huku nikutudhalilisha wakatoliki

Yaani nasikia aibu sana mimi kuitwa mkatoliki

Hawa viongozi hovyo sana.

Badala ya kukemea maovu, wanakumbatia waovu

Wakapige wao mapadre mimi nafamilia yangu marufuku
 
Unawalilia RC. utadhani ni chama cha siasa.
Subiri kanisa la wachaga KKKT li support kila wanachotaka chadema..
 
Ahsante kwa andiko hili lenye funzo mhimu, mkuu 'Barafu'.

Linalojitokeza kwa msimamo waliochukua hawa wenye dini yao, ni kwamba waumini wataanza kuhoji. Hili ni jambo jema watu wakianza kuhoji.
Hawa viongozi wa dini, kiukweli sio wenye kanisa; kanisa ni waumini. Waumini wanapoanza kuhoji yanayofanywa au kusimamiwa na viongozi wa dini zao, wanajikomboa na kujitoa kwenye ujinga wa kufuata kila kitu wasemacho viongozi wa dini kama makondoo. Kwa hiyo hili ni jambo zuri kabisa wanalofanya hawa viongozi wa dini.

Ningejua namna ya kumfikishia ujumbe wa bandiko lako hili huyo askofu ningemfikishia, au hata kumtumia kitabu chenyewe ulichotaja hapa ili na yeye ajisomee.
Na kwa bahati mbaya sana, dini zote watu/viongozi kama hawa wamo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…