Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 2,060
- 5,648
Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki Dar es Salaam, Askofu Jude Thaddeus Ruwa'ichi kupitia mahojiano aliyofanya na Tumaini TV amesema:
"Uchaguzi wa serikali za mitaa ni zoezi la kiraia, ni fursa ya kidemokrasia, lakini zoezi hilo ni lazima litekelezwe kwa uadilifu, kwa uzalendo na kwa uaminifu, ni Sala yetu kwamba kama zoezi la kupata viongozi wa serikali za mitaa raia wenye haki ya kupiga kura wapate fursa ya kupiga kura halali, nasema kura halali kwa sababu ilishatokea yakaweko manung'uniko kwamba umefanyika uchaguzi lakini waliochaguliwa hawakuchaguliwa kwa kura halali, hilo halitaifaa nchi yetu, jamii yetu katika maendeleo na halitasaidia katika maendeleo."
"Ili tuendelee kama raia wa Tanzania tunahitaji kufanya mambo kwa namna ambayo ni ya haki, uadilifu, safi na ni sahihi, nilipokuwa Roma (Italia) nilikuwa nafuatilia taarifa za habari na ilinisikitisha niliposikia kwamba hapa na pale imegundulika kwamba kuna mbinu za kuwaandikisha watoto ambao hawajafikisha umri wa kupiga kura, kitendo kama hicho ni kitendo cha hatari sana kwa sababu ni kuwafundisha watoto kuwa wezi, ni kuwafundisha watoto kuwa waongo, ni kuwafundisha watoto kuwa wahuni, sasa tukilea watoto wetu kuwa waongo, kuwa wezi, kuwa wahuni, maana yake tunatia mbegu ya mahangaiko yetu wenyewe, tupende kufanya vitu kwa usahihi na ukweli na namna hiyo ya kufanya vitu itujenge."