LGE2024 Askofu Ruwa'ichi: Kuandikisha watoto kupiga Kura ni Hatari kwa Taifa, Tunalea Wahuni na Wezi

LGE2024 Askofu Ruwa'ichi: Kuandikisha watoto kupiga Kura ni Hatari kwa Taifa, Tunalea Wahuni na Wezi

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024
Viongozi wa dini wanaotoka RC hua wamenyooka sana... Nini hua shida kwa hawa "apostoooo kuna muujiza huku...."!?!?
 
Nani anayo hayo madaftari?
Mkuu, hili nalo kweli linaweza kuwa jambo la kupotezea muda kulijadili?

Mwanzo ulikuwa "Askofu aburuzwe mahakamani", tukiamini kuwa huko ndipo kwenye haki au siyo?

Kama sote tunaamini kuwa hata huko hakuna haki; basi sioni sababu za Askofu kuburuzwa mahakamani; kwa maana tumekwisha hitimisha kuwa popote haki haitendeki, au siyo? Kama mahakama inatoa uamizi wa haki, italazimu itoe amri ya vifaa vilivyo na ushahidi huo vitolewe mahakamani. Watoto walio andikishwa wajitokeze mahakamani kama vielelezo. Kama kuna mtu hataki iwe hivyo, basi mahakama itajua la kufanya, kama inatenda haki katika maamuzi yake.

Kwa maana hiyo, serikali au yeyote yule hana haja ya kumburuza Askofu mahakamani, kwani njia mbadala zisizo za haki zipo nyingi tu za kumshughulikia.
 
Askofu Ruwaichi anaweza kuburutwa mahakamani aambiwe alete ushahidi wa hao watoto wa miaka chini ya 18 kuandikishwa
Hebu rejea alichosema; na hapa namnukuu: "........taarifa za habari na ilinisikitisha niliposikia kwamba hapa na pale imegundulika kwamba kuna mbinu za kuwaandikisha watoto ambao hawajafikisha umri wa kupiga kura, kitendo kama hicho ni kitendo cha hatari sana........"
Hapo nilipo-underline inamaanisha ni taarifa za kusikia. Habari ya kusikia hainaga mashiko mahakamani japokuwa ni kweli kuna hizo Taarifa za wanafunzi wa kidato cha kwanza huko Pwani kuandikishwa huku baadhi ya walioandikishwa wakioneshwa kuwa na umri 30yrs + (Ziliwahi kuwepo nyuzi zilizowekwa hapa jamvini - Soma LGE. 2024 zipo zaidi ya 6)
 
Askofu Ruwaichi anaweza kuburutwa mahakamani aambiwe alete ushahidi wa hao watoto wa miaka chini ya 18 kuandikishwa
Hakuna mtu wa kumpeleka Ruwaichi mahakamani wala wa kumpigia kelele.
"Roma locuta causa finita"
 
Umeanza kuelewa. Unakumbuka yaliyompata Askofu Muganyizi enzi ya Magufuli?
Nilielewa toka mwanzo, kwani njia ya mahakama siyo rafiki kwao; watakuwa wanajidhalilisha wenyewe hata kama hawawezi kuruhusu ushahidi upelekwe mahakamani. Mahakama ya umma itajuwa kinacho fanyika.
 
Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki Dar es Salaam, Askofu Jude Thaddeus Ruwa'ichi kupitia mahojiano aliyofanya na Tumaini TV amesema:

"Uchaguzi wa serikali za mitaa ni zoezi la kiraia, ni fursa ya kidemokrasia, lakini zoezi hilo ni lazima litekelezwe kwa uadilifu, kwa uzalendo na kwa uaminifu, ni Sala yetu kwamba kama zoezi la kupata viongozi wa serikali za mitaa raia wenye haki ya kupiga kura wapate fursa ya kupiga kura halali, nasema kura halali kwa sababu ilishatokea yakaweko manung'uniko kwamba umefanyika uchaguzi lakini waliochaguliwa hawakuchaguliwa kwa kura halali, hilo halitaifaa nchi yetu, jamii yetu katika maendeleo na halitasaidia katika maendeleo."

"Ili tuendelee kama raia wa Tanzania tunahitaji kufanya mambo kwa namna ambayo ni ya haki, uadilifu, safi na ni sahihi, nilipokuwa Roma (Italia) nilikuwa nafuatilia taarifa za habari na ilinisikitisha niliposikia kwamba hapa na pale imegundulika kwamba kuna mbinu za kuwaandikisha watoto ambao hawajafikisha umri wa kupiga kura, kitendo kama hicho ni kitendo cha hatari sana kwa sababu ni kuwafundisha watoto kuwa wezi, ni kuwafundisha watoto kuwa waongo, ni kuwafundisha watoto kuwa wahuni, sasa tukilea watoto wetu kuwa waongo, kuwa wezi, kuwa wahuni, maana yake tunatia mbegu ya mahangaiko yetu wenyewe, tupende kufanya vitu kwa usahihi na ukweli na namna hiyo ya kufanya vitu itujenge."
Pongezi kubwa kwa kusimama upande wa haki.
 
Hahaha, CCM hawana namna, mimi nasubiri siku ya kupiga kura tuwaone hao watoto wakiwa kwenye mstari kwenda kupiga kura. Au CCM watapiga kura kwa niaba ya watoto?
Kukomesha wizi huo tubadilishe mfumo wa kupiga kura. Badala ya makaratasi wapiga kura wasimame nyuma ya mgombea wanayemtaka badala ya makaratasi kwa kuwa hata TAKUKURU licha ya lawama zinazotolewa wamekaa kimya kana kwamba hakuna kinachotokea. Au na wao wanasubiri wapelekewe majina au wanapaswa kuchunguza na kubaini ukweli kisha kuchukua hatua stahiki?
Hahaha, CCM hawana namna, mimi nasubiri siku ya kupiga kura tuwaone hao watoto wakiwa kwenye mstari kwenda kupiga kura. Au CCM watapiga kura kwa niaba ya watoto?
 
Demokrasia imeshindikana 🐼
Ukija ukasoma maoni ya wanafalsafa wakongwr kama Plato unagundua kwamba Democracy sio mfumo mzuri wa uongozi, sababu tu ya risk ya wajinga kuwa wengi na kuamua kwenye demokrasia ya wengi wape! Wajinga Hawa sasa Ndio wanaoenda kuchagua Rais ambaye anajiona Mungu mtu na kujiongezea Kinga dhidi ya mashtaka na wanaomzunguka!
 
Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki Dar es Salaam, Askofu Jude Thaddeus Ruwa'ichi kupitia mahojiano aliyofanya na Tumaini TV amesema:

"Uchaguzi wa serikali za mitaa ni zoezi la kiraia, ni fursa ya kidemokrasia, lakini zoezi hilo ni lazima litekelezwe kwa uadilifu, kwa uzalendo na kwa uaminifu, ni Sala yetu kwamba kama zoezi la kupata viongozi wa serikali za mitaa raia wenye haki ya kupiga kura wapate fursa ya kupiga kura halali, nasema kura halali kwa sababu ilishatokea yakaweko manung'uniko kwamba umefanyika uchaguzi lakini waliochaguliwa hawakuchaguliwa kwa kura halali, hilo halitaifaa nchi yetu, jamii yetu katika maendeleo na halitasaidia katika maendeleo."

"Ili tuendelee kama raia wa Tanzania tunahitaji kufanya mambo kwa namna ambayo ni ya haki, uadilifu, safi na ni sahihi, nilipokuwa Roma (Italia) nilikuwa nafuatilia taarifa za habari na ilinisikitisha niliposikia kwamba hapa na pale imegundulika kwamba kuna mbinu za kuwaandikisha watoto ambao hawajafikisha umri wa kupiga kura, kitendo kama hicho ni kitendo cha hatari sana kwa sababu ni kuwafundisha watoto kuwa wezi, ni kuwafundisha watoto kuwa waongo, ni kuwafundisha watoto kuwa wahuni, sasa tukilea watoto wetu kuwa waongo, kuwa wezi, kuwa wahuni, maana yake tunatia mbegu ya mahangaiko yetu wenyewe, tupende kufanya vitu kwa usahihi na ukweli na namna hiyo ya kufanya vitu itujenge."
Hivi huyu askofu alistahili kweli kuwa askofu wa jiji kubwa na lenye ushawishi kama Dar kweli. Mbona ni zero brain na hana ushawishi kabisa. Hata homilia zake mi huwa nataka kanisani mana huwa ziko shallow. Hatakuja kutokea kama Pengo yule bwana alikuwa akiongea mpaka serikali inatetemeka. Sasa kadinali tuliyechaguliwa mdo kilaza haswaa. Siju rugambwa au nani kwnza hata kuongea hajui
 
Back
Top Bottom