Askofu Rweyongeza: Ujinga umelifikisha taifa letu kubaya sana

Askofu Rweyongeza: Ujinga umelifikisha taifa letu kubaya sana

The Watchman

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2023
Posts
2,186
Reaction score
4,940
Mhashamu Almachius Vincent Rweyongeza, Askofu wa Jimbo Katoliki la Kayanga, ametoa onyo kali dhidi ya kile alichokiita "ujinga na maigizo" ya baadhi ya viongozi wanaojaribu kuingiza siasa ndani ya Kanisa Katoliki.

Akizungumza kwa ukali kuhusu taratibu za kikanisa, Askofu Rweyongeza amewashangaa watu wanaoruka ngazi za uongozi na kwenda kumshtaki Askofu au Baraza la Maaskofu moja kwa moja kwa Baba Mtakatifu (Papa) bila kufuata utaratibu.

Askofu ameeleza kuwa Kanisa lina mifumo madhubuti ya kisheria na kikanisa ambayo haiongozwi kwa kukurupuka au shinikizo la kisiasa. Amebainisha kuwa Kanisa Katoliki ni taasisi kongwe ambayo imehimili dhoruba za kihistoria kwa zaidi ya miaka elfu mbili, na hakuna jitihada za kibinadamu zinazoweza kuliangusha.


 
Unauwa watu unateka viongozi wa dini unazuia watu wasiabudu halafu wewe mualifu unaenda kushtaki
Hii serikali imedekezwa sana wanajiona kila wanachowafanyia watanganyika basi wako juu ya sheria ya dunia
 
Back
Top Bottom