Precious Diamond
JF-Expert Member
- Jun 9, 2023
- 593
- 1,376
Askofu wa Jimbo Katoliki Shinyanga, Mhashamu Liberatus Sangu, amewasihi wananchi wasiwapigie kura viongozi wanaotaka madaraka kwa rushwa, na kwamba wakipewa rushwa wapokee lakini wasipige kura kwa sababu wanaotoa rushwa ni wabinafsi na siyo wazalendo.
Askofu Sangu ameyasema hayo Machi 31, 2024 katika Ibada ya Pasaka Kanisa Katoliki Parokia ya Ngokolo akiwataka Watanzania kuombea amani katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024 ili upite kwa amani.
"Akikupa rushwa pokea si amekupa, lakini kwenye sanduku hakuna kumpigia kura, kuweni makini sana na watu wanaotafuta madaraka kwa rushwa siyo wazalendo, daima ni wabinafsi tuwe nao macho," amesema Askofu Sangu na kuwasihi wenye sifa kuchukua fomu za kugombe uongozi,
"Akina Mama chukue fomu Mgombea uongozi, Rais wetu ni Mwanamke, Spika wa Bunge Mwanamke na mnauwezo mkubwa wa kuongoza sababu mpo watulivu, pia na vijana tujitokezeeni kugombea kwenye hizi chaguzi," amesema Askofu Sangu.