Lax
JF-Expert Member
- Feb 10, 2022
- 4,740
- 7,179
Mkuu nina swali mfano magu alikua raisi wa awamu ya tano je 2020 lissu angechukua uraisi angeitwa raisi wa awamu ya ngapi?Je, awumu ya Tano iliisha lini mpaka tunafika awamu ya sita.?
Je, awamu ni mtu au ni mfumo wa serikali baada ya wananchi kumchagua Rais na serikali yake kwa Kura .?
Je, sio awamu ya tano iliyomweka Mh. Samia kwenye nafsi ya kuweza kuendeleza kijiti baada bila kukabidhiwa na mtu wala wananchi kumchagua ili akamilishe awamu aliyokua nayo na aliyokua anaitumikia na kuifahamu vizuri.
Hii ya kuita awamu ya sita ni janja tu ya machawa ila awamu yake itaanza 2025 endapo atagombea na kushinda.
Huyu ni rais wa kujaza nafasi ya Rais aliyefia madarakani na endapo naye atafia pale (Mungu epushia mbali)basi atakua ni Mpango . Je ,mpango kwa miezi kumi au sita iliyobaki ataitwa rais wa awamu ya saba mfano imebaki miezi saba ataitwa rais wa awamu ya saba . Na mwezi wa kumi uchaguzi awe anaingia awamu ya pili. Katiba ya CCM na serikali yake ni katiba ya wahuni na watu wasiojali maslahi ya nchi zaidi ya matumbo yao.
Awamu moja ina muda wa miaka kumi na sio nane . Ikikamilishwa na miaka mitano mitano na sio mitatu.
Samia hana awamu yake ya sita bali ni ya tano na ameipata kwa utaratibu wa kuendeleza awamu aliyoitumikia kwa sifa ya umakamu wa Wa rais aliyefariki na sio kwa mamlaka ya kura za wananchi .
Awamu yake ya sita itaanza 2025 endapo atapita na hiyo ndiyo itakua awamu ya sita.
Hii ni awamu ya tano .
Bakita waeleze awamu maana yake ni nini