GE2025 Askofu Shoo: Ni makosa kuacha kujitokeza kushiriki kupiga kura

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Hizi dini ni utaoeli mtupu sipotezagi muda kufatilia
 
Askofu wa Dayosisi ya Kaskazini ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dk. Frederick Shoo, amesema ni makosa kuacha kujitokeza kushiriki kupiga kura, huku akiwataka Watanzania wasikubali mtu yeyote awaondolee haki na wajibu wao wa kuchagua kiongozi wanayemtaka.

Akizungumza leo katika Mkutano Mkuu wa 17 wa Jimbo la Kilimanjaro Kati la Dayosisi hiyo uliofanyika Majengo, Moshi, mkoani Kilimanjaro, amesema hoja inayoendelea ya watu kuacha kuona umuhimu wa kushiriki mchakato wa uchaguzi, hayo ni makosa.

"Wito wetu wote tunapoingia katika uchaguzi mkuu, tuombee mchakato mzima. Na sisi tumewahamasisha watu washiriki na kujitokeza kikamilifu katika kupiga kura.

Sisi tutambue tunao wajibu wa kuchagua, tena wajibu wa kikatiba. Tusikubali mtu yeyote atuondolee haki yetu na wajibu wetu, tusikubali. Mungu anataka tushiriki, tufanye uchaguzi, tusimame kama raia na wananchi tukachague viongozi tunaowataka.
Mk wake
 
Nenda wewe baba Askofu, si LAZIMA na si KOSA kikatiba na kisheria mtu kutopiga kura.
Ambao hawatakwenda wana sababu zao za msingi kutofanya hivyo, heshimuni maamuzi yao.
 
Back
Top Bottom