Mbunge wa Korogwe Vijijini Timotheo Mzava anatarajiwa kufunga ndoa na Binti wa Mbunge wa Arumeru Mashariki Dr. Jonh Pallangyo. Ndoa hii inalalamikiwa na mtu anayetambulika kwa jina la Anna na wachungaji huko Arusha na Tanga wanafahamu upo mgogoro. Mgogoro huu nimeusoma kwenye gazeti kwamba Mzava ameishi na mwanamke kinyumba kwa miaka mitatu na amezaa naye mtoto Kisha akamwacha na kuanza mahusiano na mtoto wa Mbunge mwenzie.
Mimi sina shida na mahusiano mapya ila kwa mujibu wa Taarifa zilizotolewa na Raia Mwema na nikiwa Kama muumini wa kikristo nimeona Kama kanisa halifanyi kazi yake Kama linavyopaswa kufanya. Kanisa linachafuka kwa kuandikwa vibaya kwenye magazeti lakini pia skendo ikihusisha watu wenye vyeo na fedha kwenye jamii.
Tunapoona haya yanaandikwa kwenye vyombo vya habari na kwa kuwa yanagusa imani zetu za dini pamoja na nyumba za ibada, tunalazimika kuwaomba viongozi wa dini watoke adharani kukana tuhuma hizi zilizoelekezwa kwao au kuzikubali na kuzirekebisha kwa kuzingatia maandiko na Katiba ya kanisa.
Utaratibu wa kanisa upo wazi, kabla ya kufunga ndoa lazima ndoa itangazwe siku 21 na likitokea pingamizi Basi lipatiwe ufumbuzi na TAASISI husika, je inakuwaje Kuna pingamizi na taratibu za kufunga ndoa next week kwa mujibu wa gazeti zinaendelea.
Endapo muumini atabainika kufanya uzinzi na ushahidi kuwepo (kwa mazingira haya ushahidi ni mtoto wa mzava na Anna) muumini lazima asimame mbele ya kanisa na kutubu Kisha kurejeshwa kundini ndipo taratibu za ndoa ziendelee, huyu Mzava hajawahi kufanya haya.
Panapowekwa pingamizi mweka pingamizi uitwa na suluhu upatikana, kwenye hili hakuna hiyo suluhu. Je, siku ya ndoa Anna akisimama akasema anapingamizi ndoa itafungwa? Kanisa halina walinzi, je siku hiyo familia hizi mbili zitakuja na walinzi kanisani kwa sababu Wana nafasi serikalini na Wana fedha? Kwanini Mkuu wa KKKT usubiri hadi Hali ichafuke kwenye hekalu wakati una nafasi yakusimama imara na kuzitetea nguzo za imani?
Nikuombe wewe na viongozi wa kanisa msiruhusu mambo haya kufanyika sirini, tokeni adharani msafishe kanisa kwenye tuhuma hizi za wanasiasa kutumia madara na pesa kupindisha utaratibu wa kanisa.
Tendeni haki, Kama Mzava na Pallangyo Wana haki tokeni adharani tuelezeni kwa haki yao ni ipi, na Kama huyo mwanamke Anna ana haki na mtoto wake kuweka pingamizi sikilizeni pingamizi ilo. Msipowatendea wenye fedha na madaraka Kama mnavyowatendea watu wa chini dhambi hii italipasua kanisa. Wapo waumini wametengwa kwa zinaa, Wapo waumini ndugu zao wamezikwa bila kanisa kushiriki kisa tu alikuwa ajarudishwa kundini, Wapo watu wametengwa na huduma za kanisa baada ya kubainika Wana vimada au mke zaidi ya mmoja lakini watu hao wote kwa miaka ya hivi karibuni wamekuwa na waumini wa Hali ya chini.
Matajiri na wenye nyadhifa hakuna sehemu mmewatenga Wala kukataa kuwazika. Simamieni misingi ya kanisa acheni kuwaona waumini flani Wana haki kuliko wengine.
Natumai utamwomba Mwenyenzi Mungu akusaidie kuliponya kanisa pale ambapo walio chini yako wamekuwa wakipotoka. Nakupenda nakutakia tafakuri njema huku ukilinda imani na kanisa ulilokabidhiwa.
KANISA HALITAMBUI NDOA ZA KIMILA WALA ZA KISERIKALI ILA LINAZIHESHIMU.
Naomba nikujibu duku duku lako kama ifuatavyo
Kwanza ,Nikufahamishe tu kuwa Kanisa huwa halitambui ndoa zilizofungwa nje ya utaratibu wa kanisa ila huwa linaziheshimu.
Pili, Kuzaa na mwanamke au mwanaume hata ungezaa watoto ishirini bado hiyo siyo ndoa bali mlikuwa mnafanya uasherati.Hiyo haiwezi kuitwa ndoa na kanisa lolote lile.
Ukiwa unaishi na mwanamke au mwanaume bila kwenda kufunga ndoa madhabahuni kwa upande wa kanisa haliwatambui kama mke na mume.
Tatu, Kwenye hilo sakata mshauri huyo ndugu yako kama alifungishwa ndoa ya kanisani achukue cheti chake atoe kopi aende kwenye kanisa inapotaka kufungiwa ndoa hiyo amuone mchungaji kiongozi wa kanisa la mahali hapo akiwa na cheti cha ndoa cha KANISA na siyo kingine chochote ataandikishwq maelezo ya kuweka pingamizi.Na litakubalika
Nne,Kama aliishi maisha ya bila ndoa ya KIKANISA na hana cheti cha ndoa ya kanisani basi walikuwa wanafanya uasherati kama mtu mwingine yeyote yule ambaye hajafunga ndoa.HIVYO KANISA HALIWEZI KUSIMAMISHA KUFUNGWA KWA HIYO NDOA KAMA HANA CHETI CHA NDOA YA KANISANI.
Tano, Kwa kukusaidia au kumsaidia huyo ndugu yako ili ndoa isifungwe siku hiyo anapaswa kufanya yafuatayo.
Kwanza,Hatua ya kwanza aende mahakamani kuomba kuzuia hiyo ndoa ambapo mahakama itampa COURT ORDER ya kuzuiwa kufunga ndoa hiyo.
Pili,Hatua ya pili, Aichukue hiyo COURT ORDER aupeleke kwa Mchungaji kiongozi linalotakiwa kufungiwa ndoa amkabidhi mchungaji hiyo COURT ORDER na lazima asaini kitabu cha wageni na makabidhiano hayo ya COURT ORDER kwa maandishi.Akumbuke kutoa kopi na yeye awe na nakala.
Jambo hili linapaswa lifanyike kabla ya siku ya ndoa.Afanye mapema iwezekanavyo.Kinyume na hapo ndoa hiyo itafungwa kama kawaida na itakula kwake.
Suala hilo wala halipo ngazi ya Askofu.Hilo lipo chini ya Mchungaji kiongozi wa Shemu inayofungwa ndoa.Mshauri huyo ndugu yako afuate utaratibu aache kupatika ovyo kwenye vyombo vya habari huko hawezi kupata misaada wowote.
Mwambie apeleke cheti cha ndoa kama hana cheti cha ndoa aende mahakamani kuomba COURT ORDER ya kusimamisha hiyo ndoa ili isifungwe kisha aupeleke kwa mchungaji wa eneo hilo mapema iwezekanavyo.
Nawatakia kila la heri
Mwisho nitoe wito kwenu wakina dada.Muache kuishi maisha ya uchumba sugu.Kama mmeshazaa na watoto au mtoto kwanini usiende kanisani kubariki ndoa yako? Leo angekuwa amebariki ndoa hiyo taabu yote asingeipata.
Hata huyo mchumba wake kamwe asingethubutu kutangaza ndoa nyingine ya kanisani labda abadili dini.
Mwisho usiwe mtu wa kutuhumiwa kanisa.Acha.Kanisa siyo Shemu ya siasa.Kanisa linamiongozo yake.Halibadiliki ipo kama ilivyo.
Nawatakia kila la heri.
Nawasilisha.