Askofu Shoo, Wabunge Timotheo Mzava wa Korogwe na Dkt. Pallangyo wa Arumeru wanalichafua kanisa au wanachafuliwa?

Kama Anna na Mzava waliishi kama mume na mke Kwa zaidi ya miaka miwili, hapo Kuna presumption of marriage.

Anna ana pingamizi halali, asikilizwe.
Lkn kama walikuwa waliishi kama wazinzi na kupata watotot , wanafungwa na pingamizi gani?
TOBA ya mtu si tu lazima ifanywe mbele za kanisa, japo ni kweli kuwa lazima aonesha badiliko kulingana na Toba yake.

Huwezi kulazimisha kuoa au kuolewa na mtu mliyekuwa manazini naye.

Mungu asichanganywe na uhuni wa wanadamu kama watu wanaishi kinyume na taratibu za Ndoa iliyo takatifu watengwe na Kanisa na ndicho ambacho hawa walisitahili kabla ya kuja kuleta hitaji la kufunga ndoa
 
Ujanjaujanja Kwenye Dini Nadhani Kote
kweli kabisa, ni dalili za siku za mwisho.
Makanisa ya kipentekoste[walio-okoka] ndio kabisa, watoto wa wachungaji ni kujipia vitoto bikra watakavyo, wanazaa nje ya ndoa[bila ndoa ] na hawatengwi ila wewe kajamba nane jaribu tu , ushatengwa.
 
kweli kabisa, ni dalili za siku za mwisho.
Makanisa ya kipentekoste[walio-okoka] ndio kabisa, watoto wa wachungaji ni kujipia vitoto bikra watakavyo, wanazaa nje ya ndoa[bila ndoa ] na hawatengwi ila wewe kajamba nane jaribu tu , ushatengwa.
Shida Sana Ndugu Zangu
 
Labda nikuulize wakili msomi,ina maana Ndoa ya kiserekali haitambuliki na ni dhambi kwa wake waumimi wa katoliki?
Kikanisa haitambuliki ndio maana watu walioanza kufunga huko wakitaka wafunguliwe huduma za kikanisa kama sakramenti ni lazima fuate upya taratibu za kanisa na kuja kubarikiwa kanisani

Kanisa lina aina moja tu ambayo ni monogamous ya mke mmoja mme mmoja mpaka kifo kiwatenganishe lakini ya kiserikali inakubali zote monogamy na polygamy ambayo ni haramu kikanisa

Na ikitokea mwanume mkatoliki akawa amefunga ndoa ya kiserikali na akachagua pale mke zaidi ya mmoja na akawa nao akitaka kwenda kufunga ndoa ya kanisa lazima amkane mmoja ili amchague mmoja wapo afunge naye ndoa takatifu isiyokuwa na kipengele cha talaka
 
Brodher, hiyo sio ndoa ni uhawara siibkidini na wala kwa mujibu wa sheria ya ndoa labda maneno ya DEFACTO na DE JURE niliyoyatumia huyajui, labda hujui kitu gani kilisababisha tuende kukopa hicho kifungu kuyoka KENYA kwenye tume ya judge fray labda hujui kesi za akina BI HAWA MOHAMED
 
Hivi lile la Tangazo la Siku 21 kukaribisha endapokuna pingamizi no kwa mujibu wa Sheria ya Serikali au Kanisa!???
Hata hivyo maadam wahusika ni Wabunge wa CCM Acha wapambane na hali yao!
Kama alikuwa hajafunga ndoa nyingine yoyote iwe ya kimila ama ya kiserikali hata akipeleka hilo pingamizi haliwezi kuwa kizuizi cha ndoa
 
Huo ni mtazamo wa kiimani ambao sipingani nao.

Ila Sheria inatambua watu waliokaa pamoja Kwa miaka miwili na zaidi kama mume na mke.

Nimesema huyo mama ana hoja kwakua anazo haki zifuatazo.

1. Matunzo ya mtoto.

2. Machumo ya ndoa.

Sasa Kwa hoja hizo mbili ipo haja ya kumsikiliza kwani mapingamizi yake ni halali.

Busara tu zitumike.
 
Hivi lile la Tangazo la Siku 21 kukaribisha endapokuna pingamizi no kwa mujibu wa Sheria ya Serikali au Kanisa!???
Hata hivyo maadam wahusika ni Wabunge wa CCM Acha wapambane na hali yao!

Kama linatangaziwa kanisani basi la kanisa na kama kwenye mabango ya halmashauri basi la serikali
 
 
Hizo haja ni SAHIHI. Ni za kisheria, ana Haki yake itaipata tu.
Lakini kwa Kanisa ni hoja tofauti ,
 
KANISA HALITAMBUI NDOA ZA KIMILA WALA ZA KISERIKALI ILA LINAZIHESHIMU.

Naomba nikujibu duku duku lako kama ifuatavyo

Kwanza ,Nikufahamishe tu kuwa Kanisa huwa halitambui ndoa zilizofungwa nje ya utaratibu wa kanisa ila huwa linaziheshimu.

Pili, Kuzaa na mwanamke au mwanaume hata ungezaa watoto ishirini bado hiyo siyo ndoa bali mlikuwa mnafanya uasherati.Hiyo haiwezi kuitwa ndoa na kanisa lolote lile.
Ukiwa unaishi na mwanamke au mwanaume bila kwenda kufunga ndoa madhabahuni kwa upande wa kanisa haliwatambui kama mke na mume.

Tatu, Kwenye hilo sakata mshauri huyo ndugu yako kama alifungishwa ndoa ya kanisani achukue cheti chake atoe kopi aende kwenye kanisa inapotaka kufungiwa ndoa hiyo amuone mchungaji kiongozi wa kanisa la mahali hapo akiwa na cheti cha ndoa cha KANISA na siyo kingine chochote ataandikishwq maelezo ya kuweka pingamizi.Na litakubalika

Nne,Kama aliishi maisha ya bila ndoa ya KIKANISA na hana cheti cha ndoa ya kanisani basi walikuwa wanafanya uasherati kama mtu mwingine yeyote yule ambaye hajafunga ndoa.HIVYO KANISA HALIWEZI KUSIMAMISHA KUFUNGWA KWA HIYO NDOA KAMA HANA CHETI CHA NDOA YA KANISANI.

Tano, Kwa kukusaidia au kumsaidia huyo ndugu yako ili ndoa isifungwe siku hiyo anapaswa kufanya yafuatayo.

Kwanza,Hatua ya kwanza aende mahakamani kuomba kuzuia hiyo ndoa ambapo mahakama itampa COURT ORDER ya kuzuiwa kufunga ndoa hiyo.

Pili,Hatua ya pili, Aichukue hiyo COURT ORDER aupeleke kwa Mchungaji kiongozi linalotakiwa kufungiwa ndoa amkabidhi mchungaji hiyo COURT ORDER na lazima asaini kitabu cha wageni na makabidhiano hayo ya COURT ORDER kwa maandishi.Akumbuke kutoa kopi na yeye awe na nakala.
Jambo hili linapaswa lifanyike kabla ya siku ya ndoa.Afanye mapema iwezekanavyo.Kinyume na hapo ndoa hiyo itafungwa kama kawaida na itakula kwake.

Suala hilo wala halipo ngazi ya Askofu.Hilo lipo chini ya Mchungaji kiongozi wa Shemu inayofungwa ndoa.Mshauri huyo ndugu yako afuate utaratibu aache kupatika ovyo kwenye vyombo vya habari huko hawezi kupata misaada wowote.

Mwambie apeleke cheti cha ndoa kama hana cheti cha ndoa aende mahakamani kuomba COURT ORDER ya kusimamisha hiyo ndoa ili isifungwe kisha aupeleke kwa mchungaji wa eneo hilo mapema iwezekanavyo.

Nawatakia kila la heri

Mwisho nitoe wito kwenu wakina dada.Muache kuishi maisha ya uchumba sugu.Kama mmeshazaa na watoto au mtoto kwanini usiende kanisani kubariki ndoa yako? Leo angekuwa amebariki ndoa hiyo taabu yote asingeipata.

Hata huyo mchumba wake kamwe asingethubutu kutangaza ndoa nyingine ya kanisani labda abadili dini.

Mwisho usiwe mtu wa kutuhumiwa kanisa.Acha.Kanisa siyo Shemu ya siasa.Kanisa linamiongozo yake.Halibadiliki ipo kama ilivyo.

Nawatakia kila la heri.
Nawasilisha.
 
KANISA HALITAMBUI NDOA ZILIZOFUNGWA NJE YA UTARATIBU WA KANISA ILA LINAZIHESHIMU

Kama waliishi bila ndoa ya kanisani hao walikuwa wanafanya uasherati na hivyo mwenzake kaamua kuachana na uasherati na kuhongwa madhabahuni kufunga ndoa rasmi ya kanisani.

Kama huyo ndugu yako anacheti cha ndoa alivyowahi kufunga ndoa na huyo mwanaume anayedai ni wake apeleke hicho cheti kwa mchungaji kiongozi wa kanisa hilo.

Kama hana cheti cha ndoa ya kanisani ,Kanisa haliwezi kusimamisha kufungisha ndoa hiyo.

Ila akitaka ndoa hiyo isifungwe basi aende mahakamani kuomba COURT ORDER YA KUZUIA NDOA HIYO ISIFUNGWE kisha amri hiyo ya mahakama aupeleke kwa mchungaji kiongozi wa eneo husika mapema iwezekanavyo kisha amsainishe kwenye dispatch book.

Baada ya kanisa kupokea amri hiyo ya mahakama ,Kanisa litawaita walalamikiwa na kuwajulisha amri hiyo ya mahakama ya kuitwa kwa ndoa yao hivyo kanisa litawasilishwa rasmi kwa maandishi likiambatanisha na nakala ya amri hiyo ya mahakama ya kuzuiwa kwa ndoa yao na hivyo kanisa litawaelekeza waende mahakamani wakamalize kesi yao hiyo ya msingi ndipo warudi kuendelea na utaratibu wa ndoa yao kulingana na hukumu ya kesi yao.

Ni kusihi kuacha kutoa maneno ya uzushi na yasiyo na afya kwa Kanisa.

Kanisa siyo Shemu ya kupiga siasa.
 
Mkuu kuishi miaka miwili au zaidi ni kigezo pekee? Have they aquired the reputation of being husband and wife!? Na ukumbuke hiyo presumption of marriage is rebuttable.
Asomeje tena wakati amesoma na kuwasilisha alichosoma! Labda ungesema asome case laws
 
Kama Anna na Mzava waliishi kama mume na mke Kwa zaidi ya miaka miwili, hapo Kuna presumption of marriage.

Anna ana pingamizi halali, asikilizwe.
Nope, presumption huwa inakuwa invoked mahakamani kwa ajili ya kumsaidia mwanamke apate mgawanyo wa mali kwa mchango aliotoa walipokuwa wanaishi pamoja.

Ina fact Sheria haitambui hiyo kwamba ni marriage but inakuwa presumed tu for purposes of mgawanyo wa mali na custody ya mtoto/ watoto.

Ina other way hiyo ni concubinage tu (umalaya) na huwezi hata kwenda kanisani kusema uliishi nae sababu kabisa haliruhusu umalaya. Hii Ina maana ya kwamba kanisa halina Mamlaka ya kusikiliza malalamiko hayo Bali huyo mhusika anapaswa aende mahakamani kuomba apewe mgawanyo wa mali na custody ya watoto kama itaonekana kweli aliishi na kupata status ya kuwa mke kwa kutambulika na majirani pamoja na kuishi na mwanaume kwa miaka mitatu mfululizo basi Mahakama huinvoke presumption of marriage ONLY for purposes za kumgawia mali tu.
 
Kweli kabisa hii ni kutaka kuchafua kabisa kwa mambo ya kijinga na uzudhi. Huyo mwanamke aende mahakamani sio kanisani, pingamizi huwa sustained kanisani kama walioana ndoa ya kanisani au serikali kwa maana Wana cheti Cha ndoa .

Huwezi kufunga valid marriage halafu uoe Tena kwa valid marriage kanisani, hiyo ya pili huwa void ab initio.

Huyu mleta mada inaonekana ndio aliyeachwa sasa anamlazimisha ndoa, akapambane kupata mali aanze maisha mapya mbunge ana hela huyo ampukutishe
 
Kama Anna na Mzava waliishi kama mume na mke Kwa zaidi ya miaka miwili, hapo Kuna presumption of marriage.

Anna ana pingamizi halali, asikilizwe.
Kanisa la Kikristo la wapi mkuu maana naona kama vile unachanganya serikali na sheria zake kwa upande mmoja na dini yenu hiyo ya mapokeo-ANYWAY vyote vya kuja tu mtajijua
 

Sasa kama kanisa halina mamlaka ya kusikiliza hoja zake,

Kwanini Huwa wanaruhusu nafasi ya kupokea mapingamizi.

Hayo ndio mapingamizi yenyewe na lazima wayatolee uamuzi.

Wakimruhusu aende mahakamani hiyo ndoa itafungwa kweli??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…