Askofu Stephano Musomba: Wale Waliolenga Risasi ni Kina Hao, Mwanadamu sio Nguruwe Kwamba Unamuua Ili Upate Kitoweo

The Magnifico

JF-Expert Member
Joined
Jul 12, 2015
Posts
431
Reaction score
1,594
"Katika misa hii tunawaombea waliouawa. Tunasema waliuawa kwa sababu watu hawa hawakuumwa, walipigwa risasi. Tunawaombea waliojeruhi Mungu awape wepesi waweze kupona lakini pia tunaombea haki na amani katika nchi yetu"

"Wale waliolenga risasi ni nani hao? Waliouawa sisi ni ndugu zao, tunalia. Tunapowaona waliolenga risasi tunawaangaliaje?, Mwanadamu si mnyama wa kawaida kama nguruwe kwamba utasema nipate kitoweo"

"Tanzania siyo kisiwa. Taifa letu limeundwa katika misingi ya upendo. Haya yaliyotendeka yametoka wapi? Hapa Tanzania tulikuwa tunayaona kwenye movie lakini sasa tumeona risasi zinavyomiminwa. Tumekaa ndani ukitoka nje unaogopa utakutana na risasi"

"Tunaimba wimbo wa amani, amani, amani, tudumishe amani. Lakini ni maneno tu tunamtaka. Nyoyo zetu zipo mbali sana. Huwezi kujenga nyumba hewani hata siku moja. Haki na Amani. Siyo tudumishe Amani tu. Msingi wa amani ambayo itakua imara kwa Taifa lolote ni haki kwa kila mmoja. Haki katika jambo lolote."

"Upo nyumbani kwenu lakini unaishi kama mkimbizi. Hili ni tatizo. Kila mtu akisema ukweli ni kwa kadiri yangu mimi, si tunauana sisi. Tusiposoma vizuri ujumbe huu ambao tunalia na kuomboleza tutafika pabaya. Tukijidai tumeziba masikio, hatuoni, tukaegemea upande mmoja, maigizo haya yatatufikisha pabaya."

– Askofu Stephano Lameck Musomba O.S.A, Jimbo Katoliki Bagamoyo.

Credit: Jugo Media.
 
Asante Askofu, kwanza walishasema eti "mnaingilia siasa" ila sahivi wameharibu wanarudi tena eti muwasaidie ...ni wanafiki wakubwa
 
Kiukweli samuya hastahili kbs kuwa rais wa Tz, hata ukiacha matukio ya maandamano...raia hawakujitokeza kwenda kupiga kura hivyo HAKUBALIKI!.
 
Asisahau na wale waliofia kwenye kiwanda cha magodoro na ni zaidi ya 50
Maana walienda kuhamisha magodoro kila mtu na la kwake, hatujui kama walikuwa wanahamishia godauni lingine.
 
Hii nchi inahitaji ukombozi
hata kwa damu nyingine tena sio kwa ajiri yetu bali kwa vizazi vijavyo

Lazima tuheshimiane hii ni nchi yetu sote
9dec...
 
Vipi waumini wa KKKT, viongozi wenu wanaweza kuongea kama anavyoongea huyu? Au wapo busy kuongeza sadaka na kubuni miradi kwaajili ya pesa?​
 
Kiukweli kwa sisi ambao tuliyashuudia live live yale mauaji tunaumia sana tena ukiongeza na huu ukiongeza na kauli za kipuuzi za serikali sijui mara waliouawa ni raia wa kigeni mara walikuwa ni wahalifu inatia hasira sana.

Yaani mtu anatoka zake gengeni kununua mchicha tena kwa tahadhari kubwa sana unashangaa tu mara kapigwa risasi ya kifua...

....inauma mno jamani inauma sana kuona roho za watu zinateketezwa kirahisi rahisi tena na serikali yao iliyoapa kuwalinda.

Hakika kuishi kwenye hizi banana republic ni moja laana kubwa sana, maisha ya watu hayathaminiwi kabisa.

Kuna watu kibao ambao hata serikali yenyewe inajua waliuliwa bila hatia ila hakuna hata kiongozi mmoja aliyetoa tamko la pole au samahani hata kwa hao waliokufa bila hatia.
 
"Katika misa hii tunawaombea waliouawa. Tunasema waliuawa kwa sababu watu hawa hawakuumwa, walipigwa risasi. Tunawaombea waliojeruhi Mungu awape wepesi waweze kupona lakini pia tunaombea haki na amani katika nchi yetu"

"Wale waliolenga risasi ni nani hao? Waliouawa sisi ni ndugu zao, tunalia. Tunapowaona waliolenga risasi tunawaangaliaje?, Mwanadamu si mnyama wa kawaida kama nguruwe kwamba utasema nipate kitoweo"

"Tanzania siyo kisiwa. Taifa letu limeundwa katika misingi ya upendo. Haya yaliyotendeka yametoka wapi? Hapa Tanzania tulikuwa tunayaona kwenye movie lakini sasa tumeona risasi zinavyomiminwa. Tumekaa ndani ukitoka nje unaogopa utakutana na risasi"

"Tunaimba wimbo wa amani, amani, amani, tudumishe amani. Lakini ni maneno tu tunamtaka. Nyoyo zetu zipo mbali sana. Huwezi kujenga nyumba hewani hata siku moja. Haki na Amani. Siyo tudumishe Amani tu. Msingi wa amani ambayo itakua imara kwa Taifa lolote ni haki kwa kila mmoja. Haki katika jambo lolote."

"Upo nyumbani kwenu lakini unaishi kama mkimbizi. Hili ni tatizo. Kila mtu akisema ukweli ni kwa kadiri yangu mimi, si tunauana sisi. Tusiposoma vizuri ujumbe huu ambao tunalia na kuomboleza tutafika pabaya. Tukijidai tumeziba masikio, hatuoni, tukaegemea upande mmoja, maigizo haya yatatufikisha pabaya."

– Askofu Stephano Lameck Musomba O.S.A, Jimbo Katoliki Bagamoyo.
View attachment 3500205

Credit: Jugo Media.
,.,...........Mnamuonea ........
 
Back
Top Bottom