Aslay ana tatizo gani, mbona simuelewi?

Aslay ana tatizo gani, mbona simuelewi?

Naanza kumuelewa Vanesaa Mdee wasanii wanapitia makubwa. Ndo maana weengine wanakua mateja
 
Yeah!
Ruge Alijaribu kumbeba beba wakapiga colabo na Nandy wakafanya na-show, mapromo clouds yalikua kama yotee.. nyimbo zake zilikua zinapigwa clouds kama dozi vile kutwa mara tatu!
Ila ndo Ivo Rg kachomoka, CMG Naona kama wamemtema hiviii
Jamaa kabaki Anapambana mwenyewe!

Bado anafanya vizuri sana ndugu
 
Hivi mnamuelewa Aslay, labda nianze kuwauliza ndugu zangu, maana nilishafikiria Sana mpaka nimeona niwasharikishe na nyinyi.

Aslay ni Moja ya Wasanii Wazuri Sana Bongo na wanakipaji cha Hali ya juu Sana, na waswahili wa Mtaani wanamuelewa sanasana nadhani Kwa sababu wanamjua Mswahili mwenzao kama ambavyo Mimi nilipata bahati ya kusoma naye pale Tandika Sekondari (Hapo nimejipa minyama mngejuaje sasa kama nimesoma na Star [emoji3] ).

Tuachane na hayo Kwanini nasema simuelewi Aslay naona kama bado anajitafuta wakati nadhani kuna hatua Fulani ambayo alikuwa kashaifikia kwenye muziki kiasi Kwamba alikuwa namba 3 yaani ukimtoa Mondi na Kiba anayefuata ni yeye, sijui hapa Kati ikawaje lakini nikaona graph yake ikiwa imestack na sielewi anachofanya kwenye muziki.

Nimefuatilia nimegundua tangu Mwaka huu uanze nadhani anatoa Ngoma kila mwezi ambapo kwa sasa anangoma karibia 5 Kwa 2020 sio mbaya kwa sababu hata Harmonize naye anafanya hasa baada ya kutoa Album ya Afro East.

Siikumbuki mara ya mwisho nimesikia interview yake kwenye Radio, TV, Blog ukitacha wakati alipotoa Ngoma yake na Alikiba ya Bembea na alipofanya Homa TVE.

Ngoma ya mwisho kutoa Aslay ilikua mchepuko ni Kali lakini ilipita kimya kimya sio hiyo tu ni nyingi ambazo akishatoa mnaweza msisikie chochote. Moyo Kiburi Mateka Kilanga Komo Rudi Darasani Mchepuko

Sijui tatizo ni nini kama nilivyosema simuelewi Japo nilijaribu kuwauliza baadhi ya wadau wa muziki walinijibu Kwamba Mwana anadai amekuwa Mkubwa hafanyi Interview na media yeyote na Ngoma wazifuate YouTube, kama ni kweli nadhani Aslay bado anaamini yeye ni namba 3 kwenye muziki

Kama anaamini hivyo anakosea sana Kwa sababu zamani nilikuwa nikisikia Sana Ngoma zake kwenye Bodaboda, vibanda vya simu Ila now sizisikii tena na hata huko YouTube anapotegemea mara nyingi huwa hazikai Trending Kwa muda mrefu, pia akumbuke game hapakati imechange sana kuna mtu anaitwa Konde Boy Mjeshi MARIOO wanahasira sana wanapiga interview hata na sisimizi, na wanafanya poa kila Kona.

Nadhani Aslay anahitaji kunielewesha kwenye hili bila hivyo, siuoni Ubora wake tena kwenye muziki au labda kama ameamua kubadilisha biashara na si muziki tena.

Insta : FB : Twit : Sangu Joseph

Mtoa maada ni aslay tu umemwona au ndie unamfahamu

List ya wasanii Tanzania inaanzia dsm mpaka kigoma
 
Anabaniwa tu, we hujui muziki ni vita murA
 
i
Yanga march 8 alitoa wimbo mpaka sasa una kimbiza mtu alipewa cha nguruwe bado kinamuendesha mpaka leo.
Nye bhana na wajinga sana,ni kama kwenye maisha yenu march 8 ndo mliwahi kushinda,mnafunguwa na droo kila siku ,tunaelekea mwezi wa 7 mnakosa ubingwa na kuperfom vizuri kwa ajili ya ujinga kama huo,utopolo mmekuwa wajinga sana,hamtafuti mafanikio mechi ya tar 8 ni kama mmechukua kombe,baada ya kifocus kwenye mechi zijazo mnafocus kwenye march 8,na azam conf mtaikosa hivi hivi
 
Nye bhana na wajinga sana,ni kama kwenye maisha yenu march 8 ndo mliwahi kushinda,mnafunguwa na droo kila siku ,tunaelekea mwezi wa 7 mnakosa ubingwa na kuperfom vizuri kwa ajili ya ujinga kama huo,utopolo mmekuwa wajinga sana,hamtafuti mafanikio mechi ya tar 8 ni kama mmechukua kombe,baada ya kifocus kwenye mechi zijazo mnafocus kwenye march 8,na azam conf mtaikosa hivi hivi
hahahahaha potelea mbali sisi mechi tulimaliza tar. 8 machi sa ivi tuko kwenye mabonanza tu

ila kumpiga nyau kuna raha yake yaani unatamba mwaka mzima
 
hahahahaha potelea mbali sisi mechi tulimaliza tar. 8 machi sa ivi tuko kwenye mabonanza tu

ila kumpiga nyau kuna raha yake yaani unatamba mwaka mzima
Kauli za wakosaji
 
Kauli za wakosaji
unasema vp Yanga kakosa wakati ki rekodi anakuzidi kila kitu ww umemzidi kuwa na washabiki ma mbumbumbu.

vp lakini ule msumari wa march 8
 
Lawama watapewa WCB mng,lkn mwanzo alivyokuwa anang'aa sifa alikuwa anapewa meneja Maneno.Aslay Kafeli kwenye management huwezi kutoa hit song 14 ndani ya mwaka mmoja,kama angekuwa anatoa tatu kali na mbili za kawaida kila mwaka Aslay mpaka sasa angekuwa bado wa moto.

Wenzake wana rekodi nyimbo nyingi alafu unachanganya kali na za kawaida wakati wa kutoa.
Hizo kali ndo zip kweli? [emoji16][emoji16][emoji16]
 
Aisee we shemeji goti nipe samaki akijua wengine tatu halafu Tanga rivasi Jumatano
 
Back
Top Bottom