Habari za ijumaa wakuu
Moja kwa moja niende kwenye mada kama kichwa kinavyojieleza hapo juu
Kumekuwa na promo nyingi sana kumhusu aslay na nandy , kutoa nyimbo mbalimbali pamoja, kufanya shoo pamoja, kuingia mikataba mbalimbali pamoja ikiwemo mikataba ya kuitangaza tatu mzuka. Lakini pia kurudia baadhi ya nyimbo za askay pamoja.
Sasa jamani mimi naona hiki kitu ni kizuri ila hakitafika mbali na kitamuacha aslay pabaya. Watu wengi wanaompenda aslay na kumsapoti kwenye ngoma zake alizokuwa anazifululiza mwanzo nadhani kwa sasa wanasita kumsapoti kwa hii kiki mpya anayopewa na hawa CLOUDS ambao wote mnawatambua vizuri sina haja ya kuelezea hapa.
Jamani mimi nachoona ni kwamba siku si nyingi aslay atafyonzwa kama mua na hatakuwa na utamu tena na watantupilia mbali.
Ushauri wangu kwa kijana aslay ni aendelee na ule utaratibu wake wa mwanzo na aachane kabisa na hawa watu wa sasa
Ni hayo tu nawasilisha