Aslay na Nandy kupelekwa Mahakamani

Aslay na Nandy kupelekwa Mahakamani

Asijali boss ruge yupo atawalipia kila kitu mahakamani,unaambiwa ruge ni genius sana huwa hashinfwi kwanza hata wao enzi zao itakua walisimamiwa na ruge.
 
Sasa mbona Walizipokeaa????? Matahiraa sana haoo.. Baada ya kuona wimbo umekuwa Hit song wanaanza ubashitee waoo
Ishu iko hivi Mkuu, Hawa walikubaliana na wenye wimbo hawakuwa na cha kupoteza (kwa uwezo wao wa kufikiri) wakadaka 800,000/- sasa baada ya ngoma kuwa hit song wajanja wa mjini wakawarudia tena wenye wimbo kuwa imekuwaje walikubali laki nane wakati wenzao wanapiga mamilioni...hadi mawakili wamewatafutia kudadadeki?? Mjini shule
 
Wasanii wa siku hizi makajanja sana hawana vipaji basi tu kulazimisha fani kwa migongo ya wasanii wa zamani. Nyimbo zao wakitynga zinadumu wiki moja au mbili ishaisha utamu
Mie huwa najiwazia kwani ni lazima kurudia wimbo wa mtu ambao ulishaimbwa sababu mwisho wa siku ndio hizi seke seke zinatokea.

Yetu macho na masikio wacha tuone mwisho ni nini.
 
Ishu iko hivi Mkuu, Hawa walikubaliana na wenye wimbo hawakuwa na cha kupoteza (kwa uwezo wao wa kufikiri) wakadaka 800,000/- sasa baada ya ngoma kuwa hit song wajanja wa mjini wakawarudia tena wenye wimbo kuwa imekuwaje walikubali laki nane wakati wenzao wanapiga mamilioni...hadi mawakili wamewatafutia kudadadeki?? Mjini shule
Si ndo hapooo... Ilaa watafelii tuu!! Maana walishakubaliana hiyo laki 8 .
 
upload_2018-2-12_14-30-56.png

Wasanii wa kizazi kipya Aslay na Nandy hatiani kupelekwa mahakamani kwa tuhuma za kufanyia kazi wimbo ujulikanao kama ”Subalkheri” ulioimbwa na kikundi cha Taarabu Asilia visiwani Zanzibar (Culture Music Club) bila ridhaa toka kwa kikundi hiko.

Hayo yameibuka mara baada wasanii hao kutuhumiwa kutoa kiasi kidogo cha fedha laki nane, 800,000 na kuwalipa baadhi ya wasanii katika kundi kama namna ya kufidia kazi hiyo kitendo ambacho ni ukiukaji wa katiba ya kikundi hicho.

Hivyo imedaiwa kuwa wamevunja katiba ya kikundi ibara ya Sita (6) inayosema kuwa nyimbo zote zilizoimbwa na kikundi ni mali ya kikundi na kwamba muimbaji, mtunzi na muweka sauti watakuwa na haki zao kupitia kikundi hicho kwa kuwalipa baadhi ya waimbaji wa wimbo huo.

“Walichokifanya Aslay na Nandy kwenda kwa waimbaji wetu na kuwapa kiwango hicho cha fedha kwetu tunaona hakikubaliki na wametoa kama zawadi tu kwa sababu thamani ya wimbo wetu haulingani na kiwango hicho. Kwa mujibu wa katiba ya kikundi chetu, ibara ya sita inaeleza nyimbo zote zilizoimbwa na kikundi ni mali ya kikundi na kwamba muimbaji, mtunzi na muweka sauti watakuwa na haki zao kupitia kikundi hicho”, amesema Twaha.

Hata hivyo Katibu Mtendaji wa Kikundi hicho Taimur Rukuni Twaha amesema kitendo cha wasanii hao kuimba wimbo huo Subalkheri bila ridhaa sio sawa na ilitakiwa wasanii hao kuonana na uongozi ili kufanya makubaliano.

Hivyo kama kikundi hawazitambui pesa hizo kwani hazijitoshelezi kufidia thamani ya wimbo huo na wamejipanga kulifikisha swala hilo mbele ya mahakama ili waweze kupata haki yao.

Kwa upande mwingine, Twaha amesema msimamo wao utabaki pale pale wa kuwafikisha Mahakamani wasanii hao endapo watashindwa kutimiza masharti waliyopewa na uongozi wa kikundi hicho.
 
Washtakiwe tu hakuna namna.Hawa madogo kila siku wanadai haki miliki lakini wao hawazifuati.Wanaanzaje kuimba wimbo wa watu bila idhini ya wenyewe? Washitakiwe tu iwe mfano.
Wachawi wanaanzaga hivi hivi
 
Back
Top Bottom