Kwa Jicho La Kibiashara:
700 M hata mtu kama Diamond ni nyingi sana na hivyo hawezi kukataa mchongo kama huo! Hapo cjamtaja Kiba.
SWALI: Sasa nini kitawafanya Tatu Mzuka wawekeze mkwanja wote huo kwa watu ambao hata total social media following kwa pamoja haifiki hata nusu ya mtu kama Diamond ambae; pamoja na mambo mengine, pia ana loyal fans base na digital influence ya kutosha kuzidi hao wawili combined!
Anyway, unless huo mkataba uwe mrefu kweli kweli ingawaje uzoefu unaonesha michezo ya kubahatisha ni ya msimu! Itafika wakati wapenda vya bwelele wote watajikuta wameshapigwa sana na hapo unakuwa ndio mwisho wa 3 Mzuka na wenzake