Aisee!
Ngoja nimtafute The Boss aje aniandikie speech ya shukrani. Wengine kuandika maneno mengi ya shukrani ungwini umetupitia pembeni. Yangekuwa makalkulesheni hapa ingekuwa afazali.
Anyway Ngoja nijaribu:
Kwa niaba ya mai dia waifu yaani bibi yenu (Hongera na nakutakia heri ya siku yako na wanawake wenzako)
Kwa niaba ya vibinti vyangu Mamshanga na ze griit Matesha (Someni kwa bidii laaleki, mje muwe member JF lol)
Kwa niaba ya kampeni Meneja wangu Kongosho asali ya ODM
Kwa niaba ya mratibu wa kampeni mai felo tablet klorokwini
Kwa niaba ya mababu wenzangu Dark City na Mtambuzi
Kwa niaba ya mwenyekiti wa JEC mheshimiwa Superman (ungechakachua kura yangu ungenikoma)
Kwa niaba ya wapwa, mabinamu, wajukuuz, mashemeji na hommies wote
Kwa niaba ya mabingwa EMT na BAK
Na kwa niaba yangu binafsi na viungo vyangu vyote mwilini...
Mimi ODM wa wajukuu nawashukuruni nyote kwa mpigo. Mlionipigia kura na msionipigia. Mlioninominate na msioninominate...yaani wote wa majukwaa yote (la wakubwa liheshimiwe zaidi lol). Yaani ahsanteni sana. Yaani dah! Yani tulihuzunika pamoja, tukafurahia pamoja na tutaendelea kuwa pamoja sana. Yaani nyie watu nyie. Yaani laaleki walahi. Yaani...
Sasa basi: Mimi nisiyestahili kupewa heshima kubwa namna hii kwa moyo wa upendo na wa dhati kabisa. Naudediketi ufalme huu kwa BAK na EMT. Tuuagawane sawa kwa sawa (Isipokuwa zawadi. Hii inawahusu Kongosho na klorokwini lol)
Baada ya kusema hayo..... Napiga magoti kuwaombeeni nyote msamehewe dhambi zenu zote na kuwasihi msirudie tena kutenda dhambi.
Mungu ibariki JF, Mungu wabariki madaktari, Mungu ibariki siku ya wanawake.
Ahsanteni kwa kunisikiliza.
Wasalaam; Asprin a.k.a Babu wa them Jukuuz, ODM.
Kaunta ya Juu
Kingstar Bar
Boko Basihaya.