Mwita Maranya
JF-Expert Member
- Jul 1, 2008
- 10,565
- 7,984
Kweli mkuu ningeweza shinda mimi au wewe wapo wengine wangekuja kubisha kama wewe tukubali matokeo na kukomaa kiJF
Kukataa matokeo ni tatizo la kimataifa, mwanzoni nilidhani ni afrika tu lakini kadri siku zinavyokwenda ninagundua kwamba hili ni tatizo la kidunia, kwahiyo nchi zote duniani zinahitaji kuzitathmini upya tume zao za uchaguzi pamoja na sheria za uchaguzi, kwani kuna baadhi ya taratibu nzuri na pia kuna baadhi ni mbaya katika uendeshaji wa uchaguzi.
Lililo muhimu ni kuzidi kuboresha utaratibu mzima wa kujipatia washindi, nadhani tujadiliane hapo baade na tuambizane wapi tunadhani panastahili kurekebishwa.
Lakini la muhimu zaidi kabla ya kutupa lawama kwa wasimamizi wa uchaguzi tujiangalie sisi wenyewe tumeshiriki kiasi gani kuufanya uteuzi na hatimaye uchaguzi kuwa wa haki? kama hatushiriki kufanya nominations, hatushiriki kupiga kura, tunapata wapi nguvu za kupinga matokeo??