MK254
JF-Expert Member
- May 11, 2013
- 32,408
- 50,809
Kuna video inasambaa kwenye mitandao inayomuonyesha RC wa Tanzania akimtukana rais wa Kenya na Wakenya, binafsi sijahangaika kuitazama maana nawafahamu Watanzania ndivyo walivyo, kwao hakuna tofauti ya malofa wa vijiweni na viongozi wa ngazi ya juu, kila mmoja huropokwa bila kuzingatia diplomasia au utaalam.
Muhimu sana asitokee kiongozi wa Kenya hata kwenye level ya mbunge kujishusha hadhi na kumjibu huyo mkuu wa mkoa, au kama vipi yule mbunge anaitwa Jaguar ndiye ajibu, maana yeye akiongea hujadiliwa na Tanzania yote hadi bungeni hadi na waziri mkuu.
Watanzania lazima waelewe kwetu hapa afya ya Wakenya lazima ilindwe kwa nguvu zote, wao kama viongozi wameamua kuwarubuni wananchi kisa umaskini wa nchi, na kuachia watu wajifie kwa corona eti hawataki kuchukua tahadhari maana nchi itaadhirika kiuchumi, sisi hapa lazima kila mtu anayeingia ndani ya nchi apimwe, apimwe apimwe na apimwe....haijalishi watatulilia kwa kiasi gani, lazima wapimwe.
Hizo hasira zao ni cha mtoto sana na haziwezi kusababisha tubadilishe sera, huku tunapima hata wanaosafiri baina ya majimbo au gatuzi iwe kajamba kutoka nje ya nchi ndiye aruhusiwe kutuletea corona. Mambo ya hasira na mizuka ndio zetu tunafahamika Afrika, hivyo hamna jipya hapo, kumtukana rais wetu au Wakenya ni kitu kidogo sana.
Hayo mahindi mnakuja kutuuzia huku na malori tunanunua kwa hela yetu, hivyo haiwezekani tutumie hela zetu kununua corona pia, jeuri ya pesa inatuwezesha kununua mahindi popote tunataka, wewe unatuletea mahindi hakikisha unatii sheria na masharti yetu. Fika mpakani ufanye aidha mojawapo wa haya
- Upimwe corona na kuruhusiwa kupita au
- Upokeze lori lako kwa dereva wa huku ikiwemo hata kuwapa Watanzania walio huku, na lipulizwe kabisa na mtupiane funguo
Madereva wetu wasiruhusiwe kuingia Tanzania maana wakienda kule lazima wageuze na corona.
Inashangaza sana wataalam wa Tanzania wote chali, hakuna anayesema wala kushauri nchi, wameachia wanasiasa waseme vitu vya ajabu ajabu ambavyo haviendani na elimu yoyote ya sayansi.
Hii imesababisha Tanzania itengwe na majirani wote kuanzia SADC hadi EAC.
Mkulu wa Tanzania nilimsikia akisema dereva aliyejiendeshea lori kilomita 1,000km hana haja ya kupimwa, hiyo kuendesha gari kwa umbali ni ishara tosha kwamba ni mzima.