Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 28,297
- 68,017
Kwema wakuu!
Kila nikijitahidi kumtetea naona inakataa. Kila nikijaribu kuona Kama itawezekana naona haiwezekani.
Anaweza fanya mazuri kuliko waliopita lakini jicho langu kutoka nyota ya Tibeli halimuoni kama atakubalika na wacheza Amapiano.
Sapoti ni Kama itaanza kuyeyuka Sirius kuanzia 2023, mivurugano mikali na mafarakano yapo waziwazi.
Lango litakuwa wazi lakini litakuwa na mitego mingi mibaya. Ataingia lakini atajikuta yupo nje. Atasema lakini ataona anajifokea mwenyewe. Atajipamba lakini atajiona dhalili. Sijui kwakweli!
Kama atakuwa mjanja ataaga na kuacha lango Kwa wategaji lakini wapiga Amapiano nao watavurugana na watega mitego. Hapa kazi ipo.
Sisi tutaangalia tuu.
Labda akinambia nimshauri; anaweza zichanga karata zake na Makuhani wavaa majoho huko madhabahuni ingawaje jicho langu linawaona makuhani mwakani 2022 wakitema dhabihu na kuchoma uvumba, akiwawahi mapema hawezitema nyongo, na hiyo inaweza kuwa Dalili nzuri.
Akiwashika Mkono maliwali, makadhi, maakida na jemadari huenda ikawa Kheri kwake lakini asichelewe Sana.
Hofu yangu ipo Kwa watega mitego, na wacheza Amapiano ambao wanataka kutrend Kwa kila Ngoma wanaoiachia hawa wanataka mpaka 2025 wawe wamekubalika.
Niishie hapa tuu
Kumbuka 2022 ni mwaka wa Makuhani kutema nyongo na kufukiza uvumba. Bahati sio mbali ni wiki moja ijayo.
Wasalamu!