chazachaza
JF-Expert Member
- Feb 21, 2018
- 2,829
- 3,835
Imani ilijaa kwake,pale alipotutoka kwa huzuni mwendazake.
viatu alikiri vikubwa kwake,lakini tukamsihi akaze vyema gidamu zake.
njia ilikuwa nyeupe kwake,kwani iliwekwa lami na mwendazake.
japo sote tulimsihi ,njiani umakini auweke,wapo wahuni ambao hapo mwanzo tuliwapiga mateke.
tukamsihi asivutwe na zao hila, pale watakapompiga ukope!!
sijui nn kilimkuta ,mbona ameunga tela na wapiga ukope!!?
wanatukaririsha eti hekalu ni maskini,wanahekalu sio tena mabwege,ukweli uliwekwa wazi na mwendazake!
usipoteze nguvu kumtetea ,atavuna anachokipanda kwa mikono yake!
chaguo ni lake,aambatane na wapiga kope,au airudie njia aliyoichonga mwendazake!!