ATCL Kaa Mbali na Ushirikiano na KQ

ATCL Kaa Mbali na Ushirikiano na KQ

Huihui2

JF-Expert Member
Joined
Jan 5, 2012
Posts
7,021
Reaction score
11,475
Kwenye habari za Channel 10 ya Saa 1:00 jioni leo tarehe 19/ 04/ 23, kuna habari inayosema ATCL ina mpango wa kushirikiana na Shirika la Ndege la Kenya maarufu kama KQ.

Kama habari hii ni ya kweli, nashauri Watanzania tukemee mipango hii kwa vile uzoefu unaonyesha ushirikiano hauna tija Kama ifuatavyo;

1. Alliance Air ikihusisha SAA na Uganda Airways ilishirikiana na Air Tanzania kwenye 1994 hadi 2002 na matokeo yake tulifilisika vibaya

2. Kenya Airways ilishirikiana na Precision Air kwenye miaka ya 2000, na baada ya hapo Precison ilidhoofu vibaya

3. Kwenye miaka ya 2001 hadi 2006 ATC ikawa washirika wa SAA na tukafa moja kwa moja

Nashauri tukatae ubia wowote na mashirika ya Africa. Labda kama kuna haja tutafute ushirika na mashirika ya Ulaya au Middle East
IMG-20230419-WA0008.jpg
 
Naunga mkono hoja 100% Wakenya ni mbwa sana linapokuja suala la ushirikiano, wana tamaa sn na sio waaminifu, katika nchi ambazo hatutakiwi kuungana nao kwa lolote basi ni Kenya, hata EAC chanzo cha kufa kilitokea Kenya labda serikali ijisahaulishe, nashauri Wakenya tushirikiane nao kwenye chakula pekee tuwe tunapiga pesa kwa kuwapelekea chakula, hiyo ndiyo sekta pekee tunapaswa kushirikiana nao mana kwenye njaa hawana ujanja, ni wavivu kulima na wazembe lkn co sekta zingine. Kwanza unashirikiana vipi na shirika linaloleta hasara kubwa kila mwaka kama KQ? Si uchizi huo?
 
Kwenye habari za Channel 10 ya Saa 1:00 jioni leo tarehe 19/ 04/ 23, kuna habari inayosema ATCL ina mpango wa kushirikiana na Shirika la Ndege la Kenya maarufu kama KQ.

Kama habari hii ni ya kweli, nashauri Watanzania tukemee mipango hii kwa vile uzoefu unaonyesha ushirikiano hauna tija Kama ifuatavyo;

1. Alliance Air ikihusisha SAA na Uganda Airways ilishirikiana na Air Tanzania kwenye 1994 hadi 2002 na matokeo yake tulifilisika vibaya

2. Kenya Airways ilishirikiana na Precision Air kwenye miaka ya 2000, na baada ya hapo Precison ilidhoofu vibaya

3. Kwenye miaka ya 2001 hadi 2006 ATC ikawa washirika wa SAA na tukafa moja kwa moja

Nashauri tukatae ubia wowote na mashirika ya Africa. Labda kama kuna haja tutafute ushirika na mashirika ya Ulaya au Middle EastView attachment 2593219
Kama kuna ukweli basi huo ni ukoma haupaswi kusogelewa!
 
Kwa taarifa yako Precision wanashirikiana na KQ na hii and imeokoa PWD wasife. Inapaswa ATCL washirikiane na PW .
 
Naunga mkono hoja 100% Wakenya ni mbwa sana linapokuja suala la ushirikiano, wana tamaa sn na sio waaminifu, katika nchi ambazo hatutakiwi kuungana nao kwa lolote basi ni Kenya, hata EAC chanzo cha kufa kilitokea Kenya labda serikali ijisahaulishe, nashauri Wakenya tushirikiane nao kwenye chakula pekee tuwe tunapiga pesa kwa kuwapelekea chakula, hiyo ndiyo sekta pekee tunapaswa kushirikiana nao mana kwenye njaa hawana ujanja, ni wavivu kulima na wazembe lkn co sekta zingine. Kwanza unashirikiana vipi na shirika linaloleta hasara kubwa kila mwaka kama KQ? Si uchizi huo?
Kweli kabisa unachosema. Kenya ni jirani anayetuangalia kwa jicho la husda, urafiki wetu ni wa mashaka. Ukisinzia kidogo inakula kwako.

Nafuu ATC ijifie yenyewe kuliko kuja kufa kwa kuambukizwa na KQ. Kwa sasa ATC kwa mtaji uliowekwa na Serikali na sawa na "binti kigori aliyetoka kuvunja ungo", ana mvuto. KQ ni kama Sugar daddy aliyekubuhu ambayo ana magonjwa hatari kama UKIMWI. Hivyo basi huyu ATC akikubali kujichanganya na KQ ni lazima atakufa tu muda si mrefu.

Tuseme HAPANA kwa ubia huu
 
ATCL imeshindwa tayari acha washirikiane na KQ.watanzania tunawaogopa sana wakenya hasa kwenye swala la mambo ya uchumi!
 
Kwenye habari za Channel 10 ya Saa 1:00 jioni leo tarehe 19/ 04/ 23, kuna habari inayosema ATCL ina mpango wa kushirikiana na Shirika la Ndege la Kenya maarufu kama KQ.

Kama habari hii ni ya kweli, nashauri Watanzania tukemee mipango hii kwa vile uzoefu unaonyesha ushirikiano hauna tija Kama ifuatavyo;

1. Alliance Air ikihusisha SAA na Uganda Airways ilishirikiana na Air Tanzania kwenye 1994 hadi 2002 na matokeo yake tulifilisika vibaya

2. Kenya Airways ilishirikiana na Precision Air kwenye miaka ya 2000, na baada ya hapo Precison ilidhoofu vibaya

3. Kwenye miaka ya 2001 hadi 2006 ATC ikawa washirika wa SAA na tukafa moja kwa moja

Nashauri tukatae ubia wowote na mashirika ya Africa. Labda kama kuna haja tutafute ushirika na mashirika ya Ulaya au Middle EastView attachment 2593219
Kwanza Kenya wenyewe Shirika lao la KQ limewashinda wanataka kuuza hisa zake. Tunatakiwa tuwe makini katika jambo hilo tusiingie kichwa kichwa tutajuta mbeleni.
Screenshot_20230419_221504_Gallery.jpg
 
Kwenye habari za Channel 10 ya Saa 1:00 jioni leo tarehe 19/ 04/ 23, kuna habari inayosema ATCL ina mpango wa kushirikiana na Shirika la Ndege la Kenya maarufu kama KQ.

Kama habari hii ni ya kweli, nashauri Watanzania tukemee mipango hii kwa vile uzoefu unaonyesha ushirikiano hauna tija Kama ifuatavyo;

1. Alliance Air ikihusisha SAA na Uganda Airways ilishirikiana na Air Tanzania kwenye 1994 hadi 2002 na matokeo yake tulifilisika vibaya

2. Kenya Airways ilishirikiana na Precision Air kwenye miaka ya 2000, na baada ya hapo Precison ilidhoofu vibaya

3. Kwenye miaka ya 2001 hadi 2006 ATC ikawa washirika wa SAA na tukafa moja kwa moja

Nashauri tukatae ubia wowote na mashirika ya Africa. Labda kama kuna haja tutafute ushirika na mashirika ya Ulaya au Middle EastView attachment 2593219
Kwanini sisi ndo tufilisike alafu wao wapete?? Je, tatizo ni watu wetu au mifumo yetu??
 
Sijui ni nini Rais wetu ameona kwa wakenya , ana waamini sana.
 
Washirikiane na PW yenye ndege 4?
Rasilimali (assets) kuu za shirika/kampuni ya ndege ni njia/masafa (traffic rights), sio ndege. Ukiwa na njia zenye biashara nzuri kubwa na business plan ya maana, ni collateral tosha kukopeshwa au kuazimwa ndege ukalipa kadiri unavyopata faida. Ndege bila biashara ya maana ni mzigo tu.

KQ wanazitaka njia zetu za anga zinazoingiza pesa wazifaidi wao, sio ndege zetu ambazo ni gharama tu kuzitunza.
 
Chukulia we ndio ATCL unaweza kwenda China au India directly mara tatu kwa week na kujaza ndege kwa abiria wa Tanzania tu.

Hata hayo mashirika makubwa kama KLM ayawezi kujaza ndege kuja popote Afrika kutoka Amsterdam pekee. Ili kujaza kuna vindege vyao vidogo au strategic partners wanao waletea abiria kutoka nchi ambazo ni masaa mawili au limoja mpaka Amsterdam ili kujaza ndege.

Kwa ivyo watu U.K., Germany, France, Ireland na nchi EU. Kuja Africa na KLM watabebwa na videge vya masafa mafupi mpaka Amsterdam halafu mnapakiwa kwenye Dreamliner kama lile alilonunua mwamba Magufuli ndio mnaletwa E.A. Likitua E.A mara nyingi Kenya na kwenyewe Kenya airways inawasambaza Uganda, Tanzania, Rwanda na Burundi that’s how routes maximise number of passengers.

Huo ndio msingi wa strategic alliances ili ATCL iweze beba abiria wa Uganda, Rwanda, Burundi na Kenya; inahitaji shirika la ndege linalo ruka maeneo hayo frequently.

Kwa muungano huo ATCL inaweza chukua abiria wa nchi hizo kutoka nje ya nchi ikitua Kenya abiria wakapata connection ya kwenda nchi zingine za EA kirahisi kwa sababu Kenya airways inaruka frequently nchi hizo.

Kuliko wakija Tanzania na ATCL ambapo inaweza bidi walale siku kadhaa ndio wapate connection za kwenda mwisho wa safari yao. Huko ni kupoteza wateja kwa sababu mashirika mengine yenye strategic partnership na Kenya airways itawabeba.
 
Back
Top Bottom