ATCL Kaa Mbali na Ushirikiano na KQ

ATCL Kaa Mbali na Ushirikiano na KQ

Kwenye habari za Channel 10 ya Saa 1:00 jioni leo tarehe 19/ 04/ 23, kuna habari inayosema ATCL ina mpango wa kushirikiana na Shirika la Ndege la Kenya maarufu kama KQ.

Kama habari hii ni ya kweli, nashauri Watanzania tukemee mipango hii kwa vile uzoefu unaonyesha ushirikiano hauna tija Kama ifuatavyo;

1. Alliance Air ikihusisha SAA na Uganda Airways ilishirikiana na Air Tanzania kwenye 1994 hadi 2002 na matokeo yake tulifilisika vibaya

2. Kenya Airways ilishirikiana na Precision Air kwenye miaka ya 2000, na baada ya hapo Precison ilidhoofu vibaya

3. Kwenye miaka ya 2001 hadi 2006 ATC ikawa washirika wa SAA na tukafa moja kwa moja

Nashauri tukatae ubia wowote na mashirika ya Africa. Labda kama kuna haja tutafute ushirika na mashirika ya Ulaya au Middle EastView attachment 2593219
ATCL inatakiwa kujiimarisha kwanza kufikia level moja na KQ ndipo waanze kushirikiana...lakin kwa ss wasipoangalia watapigwa na kitu kzito kichwan...NB:ndege wafananao huruka pamoja.
 
Jiulize KQ wameweza? Shida huwa tunadharau bila kufatilia taarifa za wengine. Kuna mbinu nyingi zinafanyika ili kulimaliza hili shirika. So sad
Hiyo inaitwa kipofu kumuongoza kipofu mwenzio, je mutafika wapi?

Au huwezi kuunganisha vilema wawili ili upate mtu mzima mmoja
 
Chukulia we ndio ATCL unaweza kwenda China au India directly mara tatu kwa week na kujaza ndege kwa abiria wa Tanzania tu.

Hata hayo mashirika makubwa kama KLM ayawezi kujaza ndege kuja popote Afrika kutoka Amsterdam pekee. Ili kujaza kuna vindege vyao vidogo au strategic partners wanao waletea abiria kutoka nchi ambazo ni masaa mawili au limoja mpaka Amsterdam ili kujaza ndege.

Kwa ivyo watu U.K., Germany, France, Ireland na nchi EU. Kuja Africa na KLM watabebwa na videge vya masafa mafupi mpaka Amsterdam halafu mnapakiwa kwenye Dreamliner kama lile alilonunua mwamba Magufuli ndio mnaletwa E.A. Likitua E.A mara nyingi Kenya na kwenyewe Kenya airways inawasambaza Uganda, Tanzania, Rwanda na Burundi that’s how routes maximise number of passengers.

Huo ndio msingi wa strategic alliances ili ATCL iweze beba abiria wa Uganda, Rwanda, Burundi na Kenya; inahitaji shirika la ndege linalo ruka maeneo hayo frequently.

Kwa muungano huo ATCL inaweza chukua abiria wa nchi hizo kutoka nje ya nchi ikitua Kenya abiria wakapata connection ya kwenda nchi zingine za EA kirahisi kwa sababu Kenya airways inaruka frequently nchi hizo.

Kuliko wakija Tanzania na ATCL ambapo inaweza bidi walale siku kadhaa ndio wapate connection za kwenda mwisho wa safari yao. Huko ni kupoteza wateja kwa sababu mashirika mengine yenye strategic partnership na Kenya airways itawabeba.
Mawazo yako ni mazuri na yanaeleweka lakini "Strategic Partner" ndiyo haaminiki. Atatuzamisha kama alivyo grab mali za iliyokuwa East African Airways mwaka 1977.

Waulize wakongwe chanzo cha neno NYANG'AU utaelewa naongea nini.

Tushirikiane na Kenya kwa tahadhari sana
 
nashauri Wakenya tushirikiane nao kwenye chakula pekee tuwe tunapiga pesa kwa kuwapelekea chakula, hiyo ndiyo sekta pekee tunapaswa kushirikiana nao mana kwenye njaa hawana ujanja, ni wavivu kulima na wazembe
Tuwauzie Chakula tu mengine Big NO, alafu msosi wanakufuata shambani
 
Mawazo yako ni mazuri na yanaeleweka lakini "Strategic Partner" ndiyo haaminiki. Atatuzamisha kama alivyo grab mali za iliyokuwa East African Airways mwaka 1977.

Waulize wakongwe chanzo cha neno NYANG'AU utaelewa naongea nini.

Tushirikiane na Kenya kwa tahadhari sana
Hivyo ndivyo airlines zinavyofanya operation zao duniani ili kupata wateja wengi wa kimataifa.

Kufanikisha hilo unahitaji ‘hub and spoke network strategy’ kuna mashirika wana ndege na route za kutosha; na wengine wanahitaji strategic alliance.

Trafsiri tu ya ‘strategic alliance/partnership’ maana yake kila shirika litafaidika kuimarisha operation zao.

Hakuna mtu anachangia chochote kwa mwenzake in physical asset, ni kubebeana abiria tu kimkakati. Na sioni ATCL kuwahitaji wakenya locally, itakuwa kwa safari zao za masafa marefu ili watanue soko la abiria wa nchi za africa mashirika kwenda na kurudi kwa sababu Kenya airways ni frequent regional flier kushinda ATCL.

Hakuna mtu anaweka mali kwenye huo ubia ni kulipana tu ili kubebeana abiria kukuza biashara kwa wote.
 
Kama hiyo ndiyo tafsiri basi haina shida
 
Shida ipo, na inaanza na kueleweshana kisomi kisha wanaishia kusema "yaliyopita si ndwele"

Shirika la ndege limekufa mara ngapi?
Hakuna tulilojifunza? Hakuna mwenye historia yake?

Ni kweli tunahitaji ubia kusonga mbele? Hatujawahi kuingia ubia? Ikawaje?

Sukuma gang, ulimaanisha nini?

PW inakufa, TRC, TAZARA, Tanesco, NIC, yote yako taabani, na sio leo, ni tangu enzi na enzi! Staff wanang'aa na ukwasi wa kufuru, shirika linakufa, ndio mtindo uliokuwepo na sasa umerudi.
 
Kwenye habari za Channel 10 ya Saa 1:00 jioni leo tarehe 19/ 04/ 23, kuna habari inayosema ATCL ina mpango wa kushirikiana na Shirika la Ndege la Kenya maarufu kama KQ.

Kama habari hii ni ya kweli, nashauri Watanzania tukemee mipango hii kwa vile uzoefu unaonyesha ushirikiano hauna tija Kama ifuatavyo;

1. Alliance Air ikihusisha SAA na Uganda Airways ilishirikiana na Air Tanzania kwenye 1994 hadi 2002 na matokeo yake tulifilisika vibaya

2. Kenya Airways ilishirikiana na Precision Air kwenye miaka ya 2000, na baada ya hapo Precison ilidhoofu vibaya

3. Kwenye miaka ya 2001 hadi 2006 ATC ikawa washirika wa SAA na tukafa moja kwa moja

Nashauri tukatae ubia wowote na mashirika ya Africa. Labda kama kuna haja tutafute ushirika na mashirika ya Ulaya au Middle EastView attachment 2593219
Wajanja kama Kenya wakikuomba ushirikiano ujue wanataka kukuua. Ni mkakati wa kukuondoa sokoni. ATCL wakae mbani na Kenya. Wapambane tu au kua makini inapobidi kushirikiana. Wenzetu ni nyang'au hawanaga mzaha kwenye biashara.
 
Kwenye habari za Channel 10 ya Saa 1:00 jioni leo tarehe 19/ 04/ 23, kuna habari inayosema ATCL ina mpango wa kushirikiana na Shirika la Ndege la Kenya maarufu kama KQ.

Kama habari hii ni ya kweli, nashauri Watanzania tukemee mipango hii kwa vile uzoefu unaonyesha ushirikiano hauna tija Kama ifuatavyo;

1. Alliance Air ikihusisha SAA na Uganda Airways ilishirikiana na Air Tanzania kwenye 1994 hadi 2002 na matokeo yake tulifilisika vibaya

2. Kenya Airways ilishirikiana na Precision Air kwenye miaka ya 2000, na baada ya hapo Precison ilidhoofu vibaya

3. Kwenye miaka ya 2001 hadi 2006 ATC ikawa washirika wa SAA na tukafa moja kwa moja

Nashauri tukatae ubia wowote na mashirika ya Africa. Labda kama kuna haja tutafute ushirika na mashirika ya Ulaya au Middle EastView attachment 2593219
Wenzetu wana uzalendo sisi maslahi binafsi kwanza hivyo lazima tulizwe.
 
ATCL imeshindwa tayari acha washirikiane na KQ.watanzania tunawaogopa sana wakenya hasa kwenye swala la mambo ya uchumi!
Washirikiane kutafuta nini sasa? Maana KQ yenyewe inapata hasara, na kuna ndege kibao zimekpdiwa - ambazo zinamilikiwa na "Vigogo" wao. Unataka shirika letu la Ndege likauawe huko?? Labda washirikiane kwenye "CODE" sharing.
 
maeneo ya kushirikiana yapo mengi,mbona Precicion wanashirikiana na KQ baadhi ya maeneo kwenye shirika!
 
Wajanja kama Kenya wskikuomba ushirikiano ujue wanataka kukuua. Ni mkakati wa kukuondoa sokoni. ATCL wakae mbani na Kenya. Wapambane tu au kua makini inapobidi kushirikiana. Wenzetu ni nyang'au hawanaga mzaha kwenye biashara.
Umeliweka vizuri sana. Wakenya ni wa kiwaangalia kwa jicho la tahadhari
 
Wenzetu wana uzalendo sisi maslahi binafsi kwanza hivyo lazima tulizwe.
Uzalendo kwa Wakenya? Hapana, wale ndiyo wanaongoza kwa UFISADI. Hata neno fisadi kumaanisha mhujumu uchumi limetokea Kenya
 
Hilo ni neno tu la kiswahili.
Unakumbuka issue ya vifaranga kuchomwax au mahindi kuzuiwa mpakani? Serikali na wapinzani kenya wote walitetea maslahi ya kenya.

Kwetu uzalendo haupo kabisa.
 
Back
Top Bottom