ATCL kuanza safari za China tarehe 20/03/2021, wasafiri kupimwa Corona mara mbili ndani ya saa 48 kabla ya safari

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
97,869
Reaction score
171,716
Hii ni habari njema kabisa kwa shirika letu la ndege.

Mkurugenzi mkuu wa ATCL amesema shirika lake litaanza safari za China tarehe 20 mwezi huu.

Bwana Matindi amesema wasafiri watalazimika kupima Corona mara mbili katika muda wa saa 48 kabla ya kuanza safari.

Chanzo: ITV habari

Maendeleo hayana vyama!
 
Nawapongeza kwa hatua hii, ushauri wangu ni kuwa wawenacho kipimo cha korona wasitegemee cha maabara ya taifa, Mchina kila mara anatoa adhabu kwa mashirika ya ndege kila abiria wakipatikana na korona, wakipatikana wanne tu suspension ya wiki moja na kuna idadi ikifika unapigwa mwezi mzima. Ni bora waanzishe utaratibu wa quarantine angalau siku 7 kabla ya safari, abiria wapimwe siku 7 kabla wakae quarantine kisha ndani ya saa 48 wapimwe tena kabla ya safari
 
Kuna mada iliwekwa hapa ikafutwa et tumekubali kile kipimo chao kipya....
 
China ndo wanatumia hicho kipimo kipya,bila kupimwa huingii nchini kwao maana wameona kina matokeo mazuri.
 
Watatumia kipimo gani?

Kile kile kilichopima mapapai na grisi au?
 
Corona haijapoa ndege inaenda China sijui mnataka nini muda mwingine hela inabidi mziangalie tuu Kama zimefungwa kwenye mkia wa chui...
 
Nawapongeza kwa hatua hii, ushauri wangu ni kuwa wawenacho kipimo cha korona wasitegemee cha maabara ya taifa, Mchina kila mara anatoa adhabu kwa mashirika ya ndege kila abiria wakipatikana na korona, wakipatikana wanne tu suspension ya wiki moja na kuna idadi ikifika unapigwa mwezi mzima. Ni bora waanzishe utaratibu wa quarantine angalau siku 7 kabla ya safari, abiria wapimwe siku 7 kabla wakae quarantine kisha ndani ya saa 48 wapimwe tena kabla ya safari
Siku 7 nikae tu bila kua productive. Duh.
 
Back
Top Bottom