ATCL Kuanza Safari za Moja kwa Moja Tanzania-Moscow 2026

ATCL Kuanza Safari za Moja kwa Moja Tanzania-Moscow 2026

Zack Abdul

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2026
Posts
1,194
Reaction score
911
Ndege ya Air Tanzania ya abiria na mizigo, sasa rasmi, kuanza safari ya moja kwa moja kutoka Tanzania kwenda jijini Moscow, nchini Urusi kuanzia mwishoni mwa mwezi Juni, 2026


IMG-20260515-WA0038.jpg
 
Ah kumbe kwa familia?... Anyway hivi niulize maafisa wa special branch bado wanapata mafunzo yao huko ? 😎
 
Safi sana.
Uamuzi sahihi.
Zanzibar inapokea watalii wengi sana toka Russia.
 
Mimi nafikiri tungejikita kwanza South Africa, China na India
Tukishakuwa vizuri hapo bila kubadilisha badilisha safari, ndio tufungue route nyingine.....
Tukifungua route nyingi huku hatuna uzoefu wa kutosha, naona kama ni risk
Sijui kama Urusi kuna abiria wa kujaza ndege....
Ningekuwa na uwezo ningenunua/kodisha ndege moja ya abiria 175... nauli yake iwe $50 tu route yoyote Tanzania.
 
HIvi kuna abiria wengi wa kwenda au kutoka Russia? Naona ATCL wanajitahidi kuongeza hasara, wanayoipata haijwatosha.
 
Kuna uwepo mdogo wa mwingiliano wa kibiashara na kijamii kati ya Russia na Tanzania kwa sasa.

Hapa ninachokiona ni serikali inatafuta washirika mbadala kufuatia mivutano ya kidiplomasia na mataifa ya Magharibi , EU, kuhusu misingi ya utawala bora na haki za binadamu... ipo wazi EU wapo tofauti na Russia. Hivyo huu mradi upo kisiasa zaidi na si kwa maslahi mapana ya kiuchumi kwa wananchi.

kiuchumi huu mradi utazalisha hasara tokana na kwamba hakutokuwepona soko endelevu la wasafiri..

Lakini yote na yote naona ni kama mbuzi inayofurukuta ikikata roho baada ya kisu kupita shingoni...

Kuingiza masuala ya diplomasia ya kisiasa kwenye masuala ya kiuchumi inaonyesha jinsi gani hii serikali ina vilaza, inasikitisha sana.

Hapo ni watu wanaanza kujiandaa mapema, maana EU wakikaza mahala pa kukimbilia ni Russia.
 
Je imejipanga vipi kuhakikisha seat zinajaa angalau 3/4 Kwenda Na Kurudi?

Russia iko kwenye vikwazo hivo hakuna VISA, MASTERCARD, Euro na Dollar kwa watalii Rubles watazipata hapa Tanzania kwenda nazo?

VISA za kwenda Russia vigezo vyake vikoje?
Huko Russia advertisements za kuvutuia Russians waje bongo zimefanywa za kutosha?
 
Nilikuwa najiuliza nitaendaje Urusi kujiunga na jeshi sasa nimepata ufumbuzi - kama mtalii
 
Back
Top Bottom