Kuna uwepo mdogo wa mwingiliano wa kibiashara na kijamii kati ya Russia na Tanzania kwa sasa.
Hapa ninachokiona ni serikali inatafuta washirika mbadala kufuatia mivutano ya kidiplomasia na mataifa ya Magharibi , EU, kuhusu misingi ya utawala bora na haki za binadamu... ipo wazi EU wapo tofauti na Russia. Hivyo huu mradi upo kisiasa zaidi na si kwa maslahi mapana ya kiuchumi kwa wananchi.
kiuchumi huu mradi utazalisha hasara tokana na kwamba hakutokuwepona soko endelevu la wasafiri..
Lakini yote na yote naona ni kama mbuzi inayofurukuta ikikata roho baada ya kisu kupita shingoni...
Kuingiza masuala ya diplomasia ya kisiasa kwenye masuala ya kiuchumi inaonyesha jinsi gani hii serikali ina vilaza, inasikitisha sana.
Hapo ni watu wanaanza kujiandaa mapema, maana EU wakikaza mahala pa kukimbilia ni Russia.