ATCL Kwenda India ni ukatili kwa Watanzania

ATCL Kwenda India ni ukatili kwa Watanzania

Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) kutumia ndege yake ya Boeing 787 Dreamliner inataraji kwenda nchini India kuwachukua watanzania 255 waliokuwa wagonjwa wakipatiwa matibabu nchini humo. Suala hili ukiliangalia juu juu unaweza kusema ni upendo wa Serikali ya Tanzania kwa wananchi wake kwa kuwachukua watanzania hao baada ya kunasa huko kwa sakata la LOCKDOWN la Ugonjwa wa CORONA ulioathiri Dunia Nzima.

Lakini laghasha, Watanzania hawa wanaoenda kuchukuliwa wameingia gharama kubwa saaaaaana za kulipia nauli ya ndege na kuwa mara 2 au 3 zaidi ya ile waliotumia awali kwenda India kutibiwa, kiasi ambacho wengi wao walioko huko wenye kipato kidogo kushindwa kulipia nauli hiyo ya kurudi nyumbani. Kama kweli Serikali inania ya dhati ya kuwasaidia wananchi wake kurudi nyumbani wafanye “COST SHARING” kwa hao wagonjwa ili kuwasaidia kurejea nyumbani. Ikumbukwe kwamba hao wagonjwa walikwenda India kutibiwa huko kwa gharama zao wenyewe na walishaingia gharama kubwa za kutibiwa wakiwa huko sasa sidhani kuwasaidia kurudi nyumbani napo waingie gharama nyingine kubwa zaidi.

Hili kwa maoni yangu naona sio kuwasaidia wananchi bali ATCL kuendelea kuingiza mapato licha ya Janga la CORONA kuendelea kuwepo. Hii inaitwa kufa kufaana kuwepo kwa janga la CORONA imekuwa ni manufaa kwa ATCL kuendelea kuingiza mapato na sio kuwasaidia wananchi wake. wakati huo ikumbukwe kuwa ndege hizi zimenunuliwa kwa Kodi za wananchi ambao ni watanzania wenyewe kati yao ndio hao walionasa huko India.

Mkurugenzi Mtendaji wa ATCL Mhandisi Ladislaus Matindi alisema “Sisi ni wafanya biashara, ndege yetu gharama yake ni hizi kwahiyo tunahitaji utupe kiasi hiki, hata wakiwa watu wawili wakiwa na uwezo wa kuichukua ndege tunawapa” Kwa kusema hivi inaonesha kuwa ATCL wako kimaslahi zaidi na sio kuwasaidia watanzania.

ATCL na Serikali kwa ujumla kwa hili hata siwasifu eti mnawajali au kuwasaidia watanzania bali nawapongeza kwa kuendele kuwaumiza wananchi hali ya kuwa ndege hizo ni Kodi zao.
View attachment 1447667
Hii nchi haina serikali ina genge la wahuni tu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nitolee ujinga mimi corona ipo wapi Ndugu zako wamekufa wangapi?
1589275071991.png
 
Mm naungama na ww mkuu. Kwanza hao watu wamelalamika sana mpaka ikabidi waseme kwa gharama yyte ile waende wachukuliwe watalipia. Uone mbele ya pesa....watu wanavyopenda pesa. Mataifa mengne wanachukua watu wao bila masharti yyte tena kwa gharama ya serikali. Lkn serikali ya wanyonge wanalipisha wanyonge mamilion ya shilingi kuwaleta nyumbani.
Na kwann unataka nchi zote zifanane

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hao watu wa India nimewaona kule facebook wakilalamika ,kinachowauma ni kwamba kwanini one way ni dollar 850,ikiwa wakati safari za anga zipo one way ilikuwa 350$
Kilichowazuia wasipande hizo za dola 350 Ni nini? Si wapande
 
Hao watu wa India nimewaona kule facebook wakilalamika ,kinachowauma ni kwamba kwanini one way ni dollar 850,ikiwa wakati safari za anga zipo one way ilikuwa 350$

Mkuu uwanja wa safari za ndege unabadilika, nauli za ndege zitakuwa ghali sana kutokana na huu ugonjwa kwa sababu mashirika mengi yatakufa kifo cha mende. Hizo ni gharama ambazo ATC wamezitoa, hiyo extra cash ulitaka nani alipe? Walipa kodi wa Tanzania hawawezi kulipa gharama hizo hiyo budget itatoka wapi?
 
NO. ATCL ili iwezepeleka ndege anatakiwa mtu wa kugharamia gharama za hiyo ndege; aidha Serikali, Watu binafsi au michango ya CORONA.
Kwenye michango ya Covid-19 hawatokei hao ni wapiga zumari.
 
Sio swali hilo mimi nina majirani waliofariki na kuthibitishwa

Ati una majirani kwani nani hana majirani? Umenisikia nalialia kama wewe? Lazima watu wafe na wengine wazaliwe. ''Kabla hujafa hujaumbika.''
 
Ati una majirani kwani nani hana majirani? Umenisikia nalialia kama wewe? Lazima watu wafe na wengine wazaliwe. ''Kabla hujafa hujaumbika.''
Swali uliloniuliza jingine nikakujibu sasa unataka mabishano tuu yasiyo na tija
 
Huwa hamjui nini mnataka. Tulisema siasa iwekwe kando katika uendeshwaji wa hizi ndege sasa wewe na sinzahome mnataka nini zaidi kama si ugomvi usiyo na tija
Ujamaa umetuharibu kweli mpaka kila kitu tunataka tunafanyiwe bure, mbaya zaidi hata wananchi hawajui nani anapaswa kuombwa msaada na ndio maana wengi wanailaumu ATCL wakati ATCL inatakiwa irudishe gharama za safari na faida pia haijalishi wanaofuatwa wako kwenye matatizo ama la (issue hapa wananchi watambue nani anapaswa kuombwa msaada ambae kimsingi ni serikali na kama itaona inafaa serikali inailipa ATCL fedha za safari, kwahiyo iwe abiria walipe au wasafiri bure ATCL lazima vitabu vyake vya akaunti vionyeshe kuna amount flani imeingia kutokana na safari hiyo
 
Sasa wewe unalalamika vipi wakati wao ndiyo wameomba msaada wa ndege kwa gharama hiyo? Pia wao ndiyo waliamua kwenda huko wakati huduma zote za afya zinapatikana hapa TZ. Kumbuka pia wengine walipeleka watoto wao shule ila wakanasa huko. Hivyo huo ni msaada tosha kabisa la sivyo waendelee kukaa huko mpaka ndege sitakapoanza safari duniani kote. Wapo wamarekani wamekwama hapa TZ mpaka sasa hivi wakisubiri ndege zianze safari.
Siku hizi vituko vinaongezeka. Yaani kwa kuwa mtu ni mvivu na hawezi kulipia hata nauli ya daladala basi anadhani kuwa kuna wengine itakuwa hawawezi kumudu kulipia ndege. Uvivu kitu kibaya sana. Ndiyo sababu sipendi kuzungukwa na wavivu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom