Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Waingereza wao walitozwa Pauni 1,600/= na nyongeza.Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) kutumia ndege yake ya Boeing 787 Dreamliner inataraji kwenda nchini India kuwachukua watanzania 255 waliokuwa wagonjwa wakipatiwa matibabu nchini humo. Suala hili ukiliangalia juu juu unaweza kusema ni upendo wa Serikali ya Tanzania kwa wananchi wake kwa kuwachukua watanzania hao baada ya kunasa huko kwa sakata la LOCKDOWN la Ugonjwa wa CORONA ulioathiri Dunia Nzima.
Lakini laghasha, Watanzania hawa wanaoenda kuchukuliwa wameingia gharama kubwa saaaaaana za kulipia nauli ya ndege na kuwa mara 2 au 3 zaidi ya ile waliotumia awali kwenda India kutibiwa, kiasi ambacho wengi wao walioko huko wenye kipato kidogo kushindwa kulipia nauli hiyo ya kurudi nyumbani. Kama kweli Serikali inania ya dhati ya kuwasaidia wananchi wake kurudi nyumbani wafanye “COST SHARING” kwa hao wagonjwa ili kuwasaidia kurejea nyumbani. Ikumbukwe kwamba hao wagonjwa walikwenda India kutibiwa huko kwa gharama zao wenyewe na walishaingia gharama kubwa za kutibiwa wakiwa huko sasa sidhani kuwasaidia kurudi nyumbani napo waingie gharama nyingine kubwa zaidi.
Hili kwa maoni yangu naona sio kuwasaidia wananchi bali ATCL kuendelea kuingiza mapato licha ya Janga la CORONA kuendelea kuwepo. Hii inaitwa kufa kufaana kuwepo kwa janga la CORONA imekuwa ni manufaa kwa ATCL kuendelea kuingiza mapato na sio kuwasaidia wananchi wake. wakati huo ikumbukwe kuwa ndege hizi zimenunuliwa kwa Kodi za wananchi ambao ni watanzania wenyewe kati yao ndio hao walionasa huko India.
Mkurugenzi Mtendaji wa ATCL Mhandisi Ladislaus Matindi alisema “Sisi ni wafanya biashara, ndege yetu gharama yake ni hizi kwahiyo tunahitaji utupe kiasi hiki, hata wakiwa watu wawili wakiwa na uwezo wa kuichukua ndege tunawapa” Kwa kusema hivi inaonesha kuwa ATCL wako kimaslahi zaidi na sio kuwasaidia watanzania.
ATCL na Serikali kwa ujumla kwa hili hata siwasifu eti mnawajali au kuwasaidia watanzania bali nawapongeza kwa kuendele kuwaumiza wananchi hali ya kuwa ndege hizo ni Kodi zao.
View attachment 1447667
Waingereza wao walitozwa Pauni 1,600/= na nyongeza.
Serikali yao imewapa miezi mitano (5) ya kuzilipa baada ya wengi kudai hawana uwezo wa kuzilipa kwa mkupuo. Nadhani nimejibu swali lako.Je sisi ni waingereza? unakijua kipato cha muingereza wa hali ya chini?
Hao watu wa India nimewaona kule facebook wakilalamika ,kinachowauma ni kwamba kwanini one way ni dollar 850,ikiwa wakati safari za anga zipo one way ilikuwa 350$
Ila wewe mbibi ni rahisi sana kuongopewa, ujana wako ulipata tabu sana. Kabla ya kurusha taarifa za hovyo, uwe unajaribu kupata uhakika wa taarifa zako.
Haujaelewa kinachozungumzwaKama wagonjwa wameomba warudishwe nyumbani Tatizo liko wapi?
Km mtu amepona unataka aendelee kukaa wodini?