ATCL Kwenda India ni ukatili kwa Watanzania

Hii nchi haina serikali ina genge la wahuni tu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Na kwann unataka nchi zote zifanane

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hao watu wa India nimewaona kule facebook wakilalamika ,kinachowauma ni kwamba kwanini one way ni dollar 850,ikiwa wakati safari za anga zipo one way ilikuwa 350$
Kilichowazuia wasipande hizo za dola 350 Ni nini? Si wapande
 
Hao watu wa India nimewaona kule facebook wakilalamika ,kinachowauma ni kwamba kwanini one way ni dollar 850,ikiwa wakati safari za anga zipo one way ilikuwa 350$

Mkuu uwanja wa safari za ndege unabadilika, nauli za ndege zitakuwa ghali sana kutokana na huu ugonjwa kwa sababu mashirika mengi yatakufa kifo cha mende. Hizo ni gharama ambazo ATC wamezitoa, hiyo extra cash ulitaka nani alipe? Walipa kodi wa Tanzania hawawezi kulipa gharama hizo hiyo budget itatoka wapi?
 
NO. ATCL ili iwezepeleka ndege anatakiwa mtu wa kugharamia gharama za hiyo ndege; aidha Serikali, Watu binafsi au michango ya CORONA.
Kwenye michango ya Covid-19 hawatokei hao ni wapiga zumari.
 
Sio swali hilo mimi nina majirani waliofariki na kuthibitishwa

Ati una majirani kwani nani hana majirani? Umenisikia nalialia kama wewe? Lazima watu wafe na wengine wazaliwe. ''Kabla hujafa hujaumbika.''
 
Ati una majirani kwani nani hana majirani? Umenisikia nalialia kama wewe? Lazima watu wafe na wengine wazaliwe. ''Kabla hujafa hujaumbika.''
Swali uliloniuliza jingine nikakujibu sasa unataka mabishano tuu yasiyo na tija
 
Huwa hamjui nini mnataka. Tulisema siasa iwekwe kando katika uendeshwaji wa hizi ndege sasa wewe na sinzahome mnataka nini zaidi kama si ugomvi usiyo na tija
Ujamaa umetuharibu kweli mpaka kila kitu tunataka tunafanyiwe bure, mbaya zaidi hata wananchi hawajui nani anapaswa kuombwa msaada na ndio maana wengi wanailaumu ATCL wakati ATCL inatakiwa irudishe gharama za safari na faida pia haijalishi wanaofuatwa wako kwenye matatizo ama la (issue hapa wananchi watambue nani anapaswa kuombwa msaada ambae kimsingi ni serikali na kama itaona inafaa serikali inailipa ATCL fedha za safari, kwahiyo iwe abiria walipe au wasafiri bure ATCL lazima vitabu vyake vya akaunti vionyeshe kuna amount flani imeingia kutokana na safari hiyo
 
Siku hizi vituko vinaongezeka. Yaani kwa kuwa mtu ni mvivu na hawezi kulipia hata nauli ya daladala basi anadhani kuwa kuna wengine itakuwa hawawezi kumudu kulipia ndege. Uvivu kitu kibaya sana. Ndiyo sababu sipendi kuzungukwa na wavivu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…