ATCL Kwenda India ni ukatili kwa Watanzania

..serikali ilitakiwa iwachukue hao wagonjwa bila kuwatoza fedha.

..hili ni suala la KIBINADAMU / HUMANITARIAN na UOKOAJI na serikali inatakiwa ibebe mzigo wa gharama.
 
Tembeeni vifua mbereee tumenunua ndegee kwa kashi.

Nauli za Ndege zimekuwa juu kuliko awamu iliyopita. Nakumbuka mwanza to dar nilipanda ndege kwa 90k.

Ndege inatumwa madagascar kuchukua box 13 za dawa ambazo hata sisi tunazo. Yani majani yametuzunguka kila kona. Tulivutiwa na packaging.



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Waingereza wao walitozwa Pauni 1,600/= na nyongeza.
 
Lini serekali ya CCM iliwahu kuuwasaidia wananchi?
 
msemaji wa serikali alisema ndege imekodiwa na mtu mmoja, huyo mtu mmoja yeye atajuana na abiria hao. kwenda kutibiwa nje inamaana unakuwa huelewi utarudi lini nchini kwahiyo unakuwa umejiandaa kikamilifu financially ukiwa huko, imetokea dharula unatakiwa urudi nitashangaa ukishindwa kujilipia nauli hata kama ni mara 3, hiyo kwako ni ndogo mno. Ungekuwa na pesa za wasiwasi ungebakia uhangaike na hospitali za ndani hadi mwisho wa maradhi yako
 
Juzi hapa niliona taarifa moja kwamba Nchi ya Uturuki ilituma ndege yake Sudan kwenda kumchukua raia wake mmoja aliyekuwa anaumwa na corona. Nikafikiri nikasema sisi waafrika tumekosea wapi maana kwa nchi zetu hizi ni ndoto. Hata hilo la kutoa ndege kwenda kuwachukua tushukuru tu.
 
Je sisi ni waingereza? unakijua kipato cha muingereza wa hali ya chini?
Serikali yao imewapa miezi mitano (5) ya kuzilipa baada ya wengi kudai hawana uwezo wa kuzilipa kwa mkupuo. Nadhani nimejibu swali lako.
 
Hao watu wa India nimewaona kule facebook wakilalamika ,kinachowauma ni kwamba kwanini one way ni dollar 850,ikiwa wakati safari za anga zipo one way ilikuwa 350$

Hapo watakuwa hawatendi haki wakilalamika, maana kabla serikali kuamua kutoa ndege kuwafuata gharama zao za kuishi huko zilikuwa kubwa mno, na wasingefuatwa bado gharama za kuishi huko zingeendelea kuwa kubwa sana kuliko wanacho kilalamikia.

Wangeweza kufikria tu kuwa, hapa ndege inaondoka tupu hadi india hailipiwi. Kwahiyo nafikr hiyo bei ni kama imegharamikia to and fro
 
Mkuu asante kwa taarifa ila hakuna jipya hapo. Hapa hapa ndani no body cares sebuse walokuwepo India? Acha kabisa
 
Hii kitu ina harufu kubwa ya rushwa, kama siasa hazitaingizwa tu, basi takukuru wanatakiwa kufuatilia kwa undani. Kwanza ni kweli kuna ruti ya India au ilikufa kimyakimya na hii ruti imekodiwa tu? Nani kakodi? Kwanini iwe gharama maratatu ya ruti za kawaida?
 
Kutokana na janga hili kuna nchi nyingi zimefanya yafuatayo
Kufuta baadhi ya kodi
Kutoa ruzuku kwa raia wake
Kurudisha raia wake wote waliokwama nje ya nchi
Umeme/maji kitolewa bure
Kigawa sanitaiza, pep na baràkoa bure
Kupandisha mishahara ya afya maradufu
Kusitisha shughuli zote za uazalisha zenye mikusanyiko

Lakini sisi Tz tumeruhusu yooote ila tumetoa ndege ifuate watu wetu waliokwama kwasababu ya lockdown tunaanza kulalamika.......hivi nani katuloga lakini?
Mleta mada hana tofauti ya roho mbaya kama aliyonayo mgogo anayeongoza bunge letu
 
Du wabongo bwana! ndo maana hatuendelei, sasa shirika likipata hasara mtoa mada atakuwa wa kwanza kutoa post ya kufurahia huku alisema kwa mbwembwe "tulimwambia" .
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…