ATCL yatolea ufafanuzi kuhusu simtofahamu ya msanii Diamond Platnumz

ATCL yatolea ufafanuzi kuhusu simtofahamu ya msanii Diamond Platnumz

Nadhani mamlaka zilikuwa sahihi kumzuia Diamond baada ya kufika airport kwa kuchelewa
 
Atcl jirekebisheni hiyo taarifa yenu ni sawa na mtu akijamba watu wazima wenzake hatusemi kajamba bali tunasema mtu mzima kapumua. Sasa na nyie kwa kweli mmepumua ila ndo mshafanya iwe kwa hila ama bahati mbaya, msiharibu kazi nzuri inayofanywa na serikali hii kwa upuuzi tu.
 
Kaunta inafungwa saa 20h00 Mondi kafika dk 15 baada ya check in kaunta kufungwa hoja yako nini zaidi ya kumwambia dogo asifikiri usafiri wa anga kama daladala ukiliona limesimama unaingia tu!
Je ndege ilikuwa imeshaondoka?
Hiyo kaunta huwa inafungwa haraka haraka hasa nyakati za jioni na kuingia mpaka utoe kiingilio. Hapo getini pameshageuzwa kuwa pango la wanyang'anyi. Inabidi wasafishwe wooote! Tuanze upya.
 
Huyo dogo anatoa wapi uthubutu wa kulichafua shirika letu la ndege kwa uzembe wake mwenyewe wa kuchelewa mda?!

Kuna nani nyuma yake hadi anakuwa na UTHUBUTU WA KIWANGO KILE KULITUHUMU /KULICHAFUA SHIRIKA ILHALI POPOTE DUNIANI MTU ANAYE CHELEWA NDEGE huwa haimusubiri?!

Huyo dogo/jipu lileeni tu.Ipo siku kwa PAPARA zale na MAJIVUNO yake atakuja kuichafua zaidi nchi kwa matamanio ya KIJINGA!

Kwa kitendo kile SHIRIKA LA NDEGE WAMPELEKE MAHAKAMANI HARAKA KWA KULICHAFUA SHIRIKA KWA UZEMBE WAKE!
Ndugu mbona kama umejawa na jazba,una uhakika hauna chuki na jamaa?
 
Maneno ya Diamond mwenyewe
"
  • Naomba nisisitize kuwa Siku ya jana tareh 16 | 12 Mimi Nasibu Abdul Juma Issaack, na nilokuwa Nasafiri nao Tokea Mwanza Sikuchelewa ndege Kabisa..Nilifika Muda Sawia kama Usafiri wa ndege za ndani unavyotaka, na kulidhihirisha hilo.. nikiwa niko pale kuna hata Abiria wengine waliingia nusu saa baadae, tena nikiwepo nimesimama palepale... na mmoja ya watu waloingia nikiwepo nimesimama ni @Harmonize_tz ... kilichotokea ni kuwa Mmoja ya watu wenye dhamana pale, siti zetu aliziuza kwa abilia wa fastjet...kwa Abiria watalii wazungu, na Walichokuwa hawajajua pia waliwauzia na baadhi ya Watu ambao ni wafanyakazi wetu wa Wasafi Media...Na Kuthibitisha tena kuwa hatukuchelewa, alikuja tena Mtu wa Air Tanzania na Kutuambia kuwa Siti zimebaki Mbili...Hivyo Tuchague watu wawili tu wasafiri.... kama kweli tulichelewa, sasa Hao wawili, sasa wangewezaje ingia??? tukasema hatuwezi safiri wawili lazima tuwe wote kama tulivyokata... hivyo ni dhahiri kuwa hatukuchelewa....ila kutokana na Ndege nyingi za kuja mwanza zilicancel Trip zao, ikiwepo Fastjet hivyo Tickets zikawa ni Dili sana na ndio yote kutokea....
    USHAURI tu kwa Ndugu zetu walopewa dhamana ya Kuliendesha shirika letu la Air Tanzania....tutambue kuwa Mh Rais, Pamoja na Serikali nzima kwa Ujumla imepambana Usiku na Mchana, imeamua kujinyima na kujitoa kwa hali na mali ili kuhakikisha Watanzania nasi tunakuwa na Ndege zetu, kwa kuamini kuwa Licha tu ya kuingiza kipato, lakini Uwepo wa Air Tanzania ni Heshima na fahari kwenye nchi Yetu....Hivyo tunaomba Mzisimamie Vizuri....na nikiwa kama Mtanzania Mzalendo Mwenye akili Timamu, siwezi tu kukurupuka kusema jambo kwani ni jukumu langu kuhakikisha nalilinda shirika

    hili, nalitangaza na kuwasifia wanapopatia lakini pia ni jukumu langu kuwaambia Mnapokosea ili mfanye marekebisho na AirTanzania kuwa shirika bora Duniani na kuipa sifa Nchi yetu... hivyo nikiwa kama Mtanzania mwenye uchungu siwezi kuona mtu alopewa dhamana ya Kuzisimamia ndege hizo anafanya vitu tofauti halaf eti nikakaa kimya...Ni sawa na Kumvunja moyo Mh Raisi na Serikali nzima kwa juhudi zake hizi... hivyo Mlopewa Dhamana tunaomba Muwe Makini, na kusimamia vyema ili tusitie doa kwenye ndege zetu.."
    .

    Nasubiria kauli ya AirTanzania .




Maelezo yanajieleza, kawekwa pending wengine wamepewa ticket na wakaingia ndani, so sio kwamba kachelewa, bali kapigwa chini watalii wakasafiri...sio fair
 
Na wametoa ufafanuzi kwa kuwa wanajua kimsingi Diamond ndio kachemka .
Check in mwisho saa 20h00 wewe unakuja 20h15 kwa kuwa tu unajua ndege inaondoka 20h45?
Na baadhi ya watu wa viwanja vya ndege wanadai kijana mara nyingi huwa anaenjoy kuwa wa mwisho anaposafiri locally ,wacha afunzwe ustaarab wa safar
Hayo mengine sizungumzii but hili la kufika wa mwisho nimewahi kumshuhudia JKNIA. Abiria wa Emirates wote walisha check in, bado dakika chache wafunge counter ndio katokea na team yake.
 
Back
Top Bottom