Athari za kutoa mimba

Athari za kutoa mimba

WLF Tanzania

Member
Joined
Oct 9, 2014
Posts
38
Reaction score
22
Wakuu,

Utoaji mimba ni jambo hatari. Kuna wakati inabidi, lakini asilimia kubwa ya watoaji mimba ni wasichana wadogo, hasa walioko shule ambao wamejiingiza katika vitendo vya ngono mapema.

Utoaji mimba unaweza kuleta madhara mengi, yakiwemo:

  • Kuhatarisha maisha
  • Kuharibu kizazi
  • Kuwa katika hatari zaidi ya kupata maradhi kama Saratani ya Shingo ya Kizazi
  • Kushitakiwa na nchi kwa kosa la kuua
  • Kwa mtu anayemuamini Mungu, kitendo hiki kinaharibu uhusiano wake na Mungu.

Kumbuka, kinga ni bora kuliko tiba. Usijiweke katika hatari ya kupata mimba kama hutaki mtoto.

Nawatakia siku njema.
 
Ni jambo baya sana. Athari ni nyingi na za muda mrefu kuliko aibu unayoepuka au faida unayopata kwa muda mfupi
 
Ni jambo baya sana. Athari ni nyingi na za muda mrefu kuliko aibu unayoepuka au faida unayopata kwa muda mfupi

Ni kweli kabisa. Ndio maana wasichana wanashauriwa kuepuka ngono isiyo salama ili kutoishia kuwa na mimba zisizotarajiwa ambazo nyingi huishia kutolewa.
 
Ujumbe mzuri sana Hongera mtoa mada kwa Somo zuri.
 
Back
Top Bottom