Athari za Kutohimiza Kiingereza

Athari za Kutohimiza Kiingereza

Wewe umeajiriwa nchi gani kwa kujua kiingereza
Unajua kanda ya ziwa wahaya na wasukuma hawapendi kuongea kiswahili na kwa taarifa yako huko mikoani ambako wewe hukujui kuna watu wengi hawakijui kiswahili.
 
Sasa wewe unajilinganisha na hao uliowataja!?? Hivi kwann ccm mnaogopa kiingereza hivi!??
Usiwe mtumwa wa fikra mkuu Kiingereza sio lugha yako, huo Mfano nimeutoa kukuonesha maendeleo katika yanaeza kuja bila hata watu wake kujua au kutumia Kiingereza kwenye miamala yao
 
Ujerumani na Japan ni nchi zenye teknolojia kubwa duniani na hawatumii kiingereza katika mitaala Yao yote na hata Kama lugha ya Taifa , Taifa imara ni lile linalosimamia misingi yake kuanzia kuwa na lugha yake wenyewe ukisema tuhamasishwe kutumia kiingereza ina maana unaturudisha katika utumwa wa kifikra na kuendelea kujiona dhaifu Kwa kudharau vitu vyetu
Kujilinganisha inabidi tujilinganishe na nchi zilizo na hali ya kama sisi. Ujerumani na Japan ni mataifa makubwa. Hayakupitia ukoloni wa Waingereza kama sisi. Don't compare apples with oranges
 
Serikali wangejenga angalau vyuo ya lugha kadhaa Kwa ajiri kuongea lugha zingine ili watu walio na shauku ya kuwa na uekewa wa kuongea lugha kama kiingereza isiwe tabu

Ingekuwa vzr sana
Nchi kama Kenya ambapo lugha zote mbili zinazungumzwa ni kutokana na kujenga vyuo vya lugha? Hapana. Tanzania pia miaka ya nyuma mhitimu yeyote wa elimu ya kidato cha nne alikuwa anaongea na kuandika vizuri lugha zote mbili.

Tulipoteza mwelekeo kwenye miaka ya sabini tulipofanyia mfumo wetu wa elimu majaribio mengi bila kufikiria vizuri matokeo yake.

Nimetoa mapendekezo namna ya kuanza tena kuturudisha kwenye kudhamini na kumudu Kiingereza.

Tunatakiwa wasomi wetu wawe kama Nyerere na Mkapa. Confident and at home with both English and Kiswahili.

It can be done, it must be done.
 
Usiwe mtumwa wa fikra mkuu Kiingereza sio lugha yako, huo Mfano nimeutoa kukuonesha maendeleo katika yanaeza kuja bila hata watu wake kujua au kutumia Kiingereza kwenye miamala yao
Kiingereza ni lugha ya dunia.Hakuna taifa linaloweza kuzuia watu wasitumie lugha ya Kiingera kwa kudai ni lugha yao pekee!

Jifunze Kiingereza na lugha nyingine za dunia kwa manufaa yoyote unayoweza kutegemea kuyapata nje na ndani ya Tanzania kupitia lugha husika!
 
Angeandika lugha gani isiyo ya Kitumwa?

Kichina?ni ya kitumwa
Kiarabu?ni ya kitumwa
Kiswahili?Ni ya kitumwa maana 80% ni Kiarabu
Kizanaki?Nani asome wakati wajua Kizanaki duniani hawazidi watu 50,000
Kifaransa?ni ya kitumwa
Kijapan?ni yakitumwa
Kihindi?ni ya kitumwa
egtc

hebu tuletee lugha isiyokua ya "kitumwa"?

Ni hivi,lugha zote duniani ni TOOLS za kufanikisha kitu unachokitaka

Kila mtu ana lugha yake,kujua ya mwingine ni TOOL ya wewe kupata chance ya kumu-influence huyo mtu..

Sisi tunaihitaji dunia zaidi kuliko yenyewe inavyotuhitaji,lazima tuiname!

Sijui hii fear mnaitolea wapi aisee?

Wewe kujua lugha ya mtu mwingine sio eti lugha yako ndio imekufa,unajua lugha zote na unazitumia inavyotakiwa!

Kuacha kabisa mother tongue yako hilo ni tatizo lako binafsi na ni kosa..ila kujua lugha ya mtu mwingine ni ujuzi additional!

Stop this nonsense
Umetoa nondo nzito sana. Kuchukua mema kutoka nje sio vibaya. Mbona hata kutumia umeme tumeiga?

Kama ulivyosema lugha ni nyenzo. Wenye uelewa mzuri wa nchi zingine wameanza kujifunza lugha yetu pia.

Dunia imekuwa kijiji kidogo. Kutomudu lugha inayotumiwa kuliko zote kwa elimu na biashara ni kujimaliza wenyewe.
 
Kwani Prof. Ndalichako au rire jiwe renyewe ririkuwa rinasemaje kuhusu hili la lugha za mabeberu?
Professor Ndalichako anamudu Kiingereza vizuri. Kosa moja hapa na pale havimwondolei sifa ya kumudu Kiingereza. Jiwe alikuwa na akili tambuzi sana na memory kali kabisa. Kumbuka alikuwa na mkichwa unaofahamu hadi urefu wa kila barabara kuu ya Tanzania. Lakini Kiingereza kikawa hakipandi. Hii ilitokana na dharau zake za kudhani hatuhitaji lugha zaidi ya Kiswahili. He was dead wrong on that score.
 
Hivi JF wakisema kitumike kiingereza tu, mijadala na maarifa yaliyomo humu tungepata? Kiingereza ni moja ya mambo yanayofanya tusiendelee
Hatupendekezi mitaani au JF kitumike Kiingereza pekee. Ni shule tu ndiyo kitumike Kiingereza peke yake. Tunapenda wahitimu wa elimu ya sekondari wawe na uwezo wa kuongea na kuandika lugha zote mbili. JF ni nje ya shule.

Wapendekeza tufanikisheje hiyo KPI? Mimi nimetoa pendekezo langu. I think it is a feasible way of achieving the required competency.
 
Siku hizi watu Hadi majina Yao wanakosea kuandika..Loda Saloon..Rozi Saloon...aibu sana
 
Madhara ya Kutokipa Kiingereza Umuhimu

Siku hizi nchi yetu ina tatizo la wananchi wengi kutoweza kuandika na kuzungumza kwa lugha ya Kiingereza. Kiuchumi, TAZIZO HILI SIYO HIMILIVU.

Adhari zake ni pamoja na zifuatazo:

1. Kukosa ajira za kimataifa. Nchi kama Uingereza inakuwa na upungufu wa manesi mara kwa mara. Wanaajiri toka Malawi, Kenya na nchi nyingine ambazo raia wake wanamudu lugha ya Kiingereza.

Mashirika kama Emirates huwa yanahitaji waajiriwa wachache wanaoweza kuongea Kiswahili na Kiingereza. Huwa wanaajiri Wakenya kwani wana hiyo sifa.

2. Kukosa ajira nchini. Nyumbani kwenyewe mashirika binafsi wanapenda zaidi wahitimu waliosoma nje kwani wao humudu lugha zote mbili.

3. Kukosa fursa za kusikika ulimwenguni. Mashirika ya habari kama Aljazeera na BBC World service wanapotaka kuongea na mtu wa Afrika Mashariki, kwa Kiingereza, huwa hawachagui Mtanzania. Wataongea na mwalimu wa chuo kikuu Mkenya au Mganda. Hii inafifisha umaarufu wa vyuo vyetu. Vinashuka kwenye viwango rasmi vya ubora duniani.

Ukiweka YouTube kitu kwa Kiswahili maana yake unakilenga kwa watu milioni 200. Ukiweka kwa Kiingereza basi umekielekeza kwa watu zaidi ya mara tano ya hao.

4. Kudumaza elimu. Reading materials mtandaoni sehemu kubwa ni za Kiingereza. Mtu asiyeelewa vizuri Kiingereza tayari anajinyima asilimia kubwa ya maarifa yaliyopo duniani.

5. Kudumaza utalii. Kutosikika kimataifa kunatunyima watalii wengi. Pia wachache wanaokuja wanajikuta hata watu wa uhamiaji na polisi hawawezi kuzungumza nao kwa Kiingereza.

Miaka ya sitini tulikuwa vizuri tu kwenye Kiingereza. Mhitimu wa shule ya sekondari alikuwa anabidika kufaulu Oral and written English.

Napendekeza kwamba:
1. Interview za ajira serikalini zizingatie uwezo wa kusema na kuandika Kiswahili na Kiingereza. Kumudu Kiingereza iwe a condition for employment of ALL civil servants.

2. Kuwe na sera ya wanafunzi shule za sekondari kuongea tu Kiingereza wawapo shuleni. Hii haitadhoofisha Kiswahili kwani watakiongea sana nyumbani na mitaani.

3. Kufaulu kidato cha nne iwe ni pamoja na kufaulu Oral English. Mitihani yake itasimamiwa na shule kama ilivyokuwa miaka ya sitini.
Je wajua katika Marais sita wa Tanzania, waliokuwa na uwezo wa kuongea Kiingereza kwa ufasaha ni Mwl Nyerere, Mzee Mwinyi na Mzee Mkapa, the rest hawana fluency kwenye kuongea zaidi wanaokoteza kulal
 
Pambania hali yako
Huu uzi nimeuleta kama hatua ya kupambana na hali yangu. Ni hali ya kukosa furaha kutokana na kuona mwelekeo usio sahihi wa taifa langu. Siishi mwenyewe naishi na wananchi milioni 60. Their loss is my loss. And we have been losing a lot on account that we have not given due emphasis to competency in English.
 
Zambia,Malawi,Kenya,Ghana wanaongea kingereza sana tu. Je wametupita nini katika maendelea ya kiuchum,sayansi na teknolojia?
Kinachowasumbua ni utimwa wa kifikra, huu ugonjwa kumtoka mwafrika ni kazi sana.
Wkati wewe unawaza kingereza kuna waafrika wenzio wanawaza kifaransa kifundishwe vizuri lakini kuna wengine wanawaza kireno bila kusahau kiarabu.
Ni ukoloni tu unaowasumbua watu weusi hakuna kingine.
Kenya wako kwenye take off stage. Natumaini unaelewa take off stage ina maana gani kiuchumi.

Ghana pia wametupita sana miaka hii. Huko nyuma, tulikuwa tunasikika sana na UDSM was ranked, by Webometrics, well ahead of all universities in Ghana and Kenya. Sasa kimeshuka sana. There are economic consequences to this.

Malawi na Zambia hawajatupita kwa sasa. Ila manesi wa Malawi wanapata sana ajira Uingereza. Wakwetu wanakwama lugha.

But to find a country that speaks English and is not better off than us doesn't prove that English is unimportant.

Kutambua kwamba tunahitaji kujua Kiingereza sio mawazo ya kitumwa. Utumwa wa kitu gani? Ni ukweli kwamba bila Kiingereza kuna makala nyingi duniani ambazo hutaweza kuzisoma.
 
Hatupendekezi mitaani au JF kitumike Kiingereza pekee. Ni shule tu ndiyo kitumike Kiingereza peke yake. Tunapenda wahitimu wa elimu ya sekondari wawe na uwezo wa kuongea na kuandika lugha zote mbili. JF ni nje ya shule.

Wapendekeza tufanikisheje hiyo KPI? Mimi nimetoa pendekezo langu. I think it is a feasible way of achieving the required competency.
Masomo mpaka chuo kikuu yawe kwa kiswahili. Kiingereza kifundishwe kama somo.
 
Masomo mpaka chuo kikuu yawe kwa kiswahili. Kiingereza kifundishwe kama somo.
Resources (vitabu, research journals, etc.) za kufundisha ngazi zote kwa Kiswahili ziko tayari?

Zamani (until 1965 or so) tulikuwa tuanafundisha kwa Kiswahili hadi darasa la tatu kisha ni Kiingereza mpaka mwisho. Watoto walihitimu shule za msingi, sekondari na vyuo vikuu wakiwa na uwezo wa kuandika na kusoma Kiswahili na Kiingereza kwa ufasaha. Kulikuwa na faida gani kubadilisha? Kimeleta matokeo hasi.

We fixed it while it was not broken. Let's swallow our pride and go back to doing what we used to do.
 
Tatizo ni jinsi tunavyofikiria. Je ni "kingereza na kiswahili" au ni " kingereza au kiswahili"? Kwa elimu na biashara / uwekezaji kingereza ni muhimu na huwezi kukikwepa. Vyuo vingi duniani vina programu na kozi zinazofundishwa kwa kiingereza ( mfano ni China, Urusi, Japan, Ufaransa, etc). Nchi hizo pia huwafundisha wanafunzi wao kingereza hata kama masomo mengine yanafundishwa kwa lugha zao. Mimi modeli yangu ni "kingereza na kiswahili " lakini tutahitaji uwekezaji mkubwa kwa lugha zote mbili. Kwa sasa wengi wetu tu wabovu kwenye kingereza na kiswahili pia. Rasili mali kubwa ya nchi yeyote ni watu wake na elimu yao ni kitu muhimu. Mafanikio ya China hapa jf hutolewa kama mfano wa maendeleo bila kingereza, ukweli ni tofauti kabisa kwani uchina pamoja na mambo mengine ilipeleka vijana kwa maelfu kwenda kusoma uingereza na america wengine wakifanya ujasusi wa technologia. Hawa wana mchango mkubwa kwenye kuipaisha nchi yao. Tuwekeze kwenye ufundishaji wa hizi lugha tutafika mbali.
 
Kenya wako kwenye take off stage. Natumaini unaelewa take off stage ina maana gani kiuchumi.

Ghana pia wametupita sana miaka hii. Huko nyuma, tulikuwa tunasikika sana na UDSM was ranked, by Webometrics, well ahead of all universities in Ghana and Kenya. Sasa kimeshuka sana. There are economic consequences to this.

Malawi na Zambia hawajatupita kwa sasa. Ila manesi wa Malawi wanapata sana ajira Uingereza. Wakwetu wanakwama lugha.

But to find a country that speaks English and is not better off than us doesn't prove that English is unimportant.

Kutambua kwamba tunahitaji kujua Kiingereza sio mawazo ya kitumwa. Utumwa wa kitu gani? Ni ukweli kwamba bila Kiingereza kuna makala nyingi duniani ambazo hutaweza kuzisoma.
Unaweza kuonyesha hio udadi ya hao manesi wanaopata sana ajira .
Kenya imefika hio take off stage kwa sababu ya kingereza, je unaushahidi?
Kwa nini zambia na malawi wasitupite mbona wanajua sana kingereza.
Unataka kuniaminisha kwamba tukijua kingereza basi tutapata sana ajira huko ulaya, unaweza thibitisha?
Je unaweza weka data Ghana wametupita kwenye jambo gani?
Je akili ya kuamini ajira zipo ulaya na Africa hazipo unadhani ni akili nzuri? Kwa nini wewe usishiriki kutatua tatizo la ajira na ukimbilie kuwa nesi ulaya! Huoni kuwa unaudhaifu wa kufikiri ?
Je unajua idadi ta watanzania wanaojua kingereza na wasiojua kingereza, kama hujui kwa nini utoe conclution ikiwa huna data!
Je upo ushahidi unaothibitisha kuwa kujua kingereza ndio ustawi bora wa jamii, je jamii zilizostawi vyema duniani zililazimika kufanya lugha ya kingereza kama msingi wa ustawi bora wa maisha?
Amini usiamini fikra za utumwa zinawasumbua ila kujua kama mmeathiriwa kisaikolojia ni ngumu sana.
Siku hizi hakuna utumwa wa nguvu bali akili na ndio tatizo kubwa la waafrika. Utumwa unawasumbua na hawajiangaishi kujitoa kwenye hilo dimbwi la kitumwa. Watanzania ndio tunaongoza kuamini katika fikra za kitumwa tukufuatiwa na Kongo DRC.
 
Tatizo ni jinsi tunavyofikiria. Je ni "kingereza na kiswahili" au ni " kingereza au kiswahili"? Kwa elimu na biashara / uwekezaji kingereza ni muhimu na huwezi kukikwepa. Vyuo vingi duniani vina programu na kozi zinazofundishwa kwa kiingereza ( mfano ni China, Urusi, Japan, Ufaransa, etc). Nchi hizo pia huwafundisha wanafunzi wao kingereza hata kama masomo mengine yanafundishwa kwa lugha zao. Mimi modeli yangu ni "kingereza na kiswahili " lakini tutahitaji uwekezaji mkubwa kwa lugha zote mbili. Kwa sasa wengi wetu tu wabovu kwenye kingereza na kiswahili pia. Rasili mali kubwa ya nchi yeyote ni watu wake na elimu yao ni kitu muhimu. Mafanikio ya China hapa jf hutolewa kama mfano wa maendeleo bila kingereza, ukweli ni tofauti kabisa kwani uchina pamoja na mambo mengine ilipeleka vijana kwa maelfu kwenda kusoma uingereza na america wengine wakifanya ujasusi wa technologia. Hawa wana mchango mkubwa kwenye kuipaisha nchi yao. Tuwekeze kwenye ufundishaji wa hizi lugha tutafika mbali.
We jamaa serikali ya Tanzania haipeleki wvijsna kwenda kusoma huko ulaya na America?
Wachina na sisi nani syllbus yao imebebwa na kingereza zaidi?
Mnatafuta mchawi kila uchwao, tatizo la maendeleo ya Africa si lugha bali ni zaidi ya lugha.
 
Back
Top Bottom