Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Unajua kanda ya ziwa wahaya na wasukuma hawapendi kuongea kiswahili na kwa taarifa yako huko mikoani ambako wewe hukujui kuna watu wengi hawakijui kiswahili.Wewe umeajiriwa nchi gani kwa kujua kiingereza
Usiwe mtumwa wa fikra mkuu Kiingereza sio lugha yako, huo Mfano nimeutoa kukuonesha maendeleo katika yanaeza kuja bila hata watu wake kujua au kutumia Kiingereza kwenye miamala yaoSasa wewe unajilinganisha na hao uliowataja!?? Hivi kwann ccm mnaogopa kiingereza hivi!??
Kujilinganisha inabidi tujilinganishe na nchi zilizo na hali ya kama sisi. Ujerumani na Japan ni mataifa makubwa. Hayakupitia ukoloni wa Waingereza kama sisi. Don't compare apples with orangesUjerumani na Japan ni nchi zenye teknolojia kubwa duniani na hawatumii kiingereza katika mitaala Yao yote na hata Kama lugha ya Taifa , Taifa imara ni lile linalosimamia misingi yake kuanzia kuwa na lugha yake wenyewe ukisema tuhamasishwe kutumia kiingereza ina maana unaturudisha katika utumwa wa kifikra na kuendelea kujiona dhaifu Kwa kudharau vitu vyetu
Nchi kama Kenya ambapo lugha zote mbili zinazungumzwa ni kutokana na kujenga vyuo vya lugha? Hapana. Tanzania pia miaka ya nyuma mhitimu yeyote wa elimu ya kidato cha nne alikuwa anaongea na kuandika vizuri lugha zote mbili.Serikali wangejenga angalau vyuo ya lugha kadhaa Kwa ajiri kuongea lugha zingine ili watu walio na shauku ya kuwa na uekewa wa kuongea lugha kama kiingereza isiwe tabu
Ingekuwa vzr sana
Kiingereza ni lugha ya dunia.Hakuna taifa linaloweza kuzuia watu wasitumie lugha ya Kiingera kwa kudai ni lugha yao pekee!Usiwe mtumwa wa fikra mkuu Kiingereza sio lugha yako, huo Mfano nimeutoa kukuonesha maendeleo katika yanaeza kuja bila hata watu wake kujua au kutumia Kiingereza kwenye miamala yao
Utake usitake yaani!English ni kama maji. Ukigoma kuyanywa utayaoga au utayakuta kwenye msosi. Haikwepeki.
Umetoa nondo nzito sana. Kuchukua mema kutoka nje sio vibaya. Mbona hata kutumia umeme tumeiga?Angeandika lugha gani isiyo ya Kitumwa?
Kichina?ni ya kitumwa
Kiarabu?ni ya kitumwa
Kiswahili?Ni ya kitumwa maana 80% ni Kiarabu
Kizanaki?Nani asome wakati wajua Kizanaki duniani hawazidi watu 50,000
Kifaransa?ni ya kitumwa
Kijapan?ni yakitumwa
Kihindi?ni ya kitumwa
egtc
hebu tuletee lugha isiyokua ya "kitumwa"?
Ni hivi,lugha zote duniani ni TOOLS za kufanikisha kitu unachokitaka
Kila mtu ana lugha yake,kujua ya mwingine ni TOOL ya wewe kupata chance ya kumu-influence huyo mtu..
Sisi tunaihitaji dunia zaidi kuliko yenyewe inavyotuhitaji,lazima tuiname!
Sijui hii fear mnaitolea wapi aisee?
Wewe kujua lugha ya mtu mwingine sio eti lugha yako ndio imekufa,unajua lugha zote na unazitumia inavyotakiwa!
Kuacha kabisa mother tongue yako hilo ni tatizo lako binafsi na ni kosa..ila kujua lugha ya mtu mwingine ni ujuzi additional!
Stop this nonsense
Professor Ndalichako anamudu Kiingereza vizuri. Kosa moja hapa na pale havimwondolei sifa ya kumudu Kiingereza. Jiwe alikuwa na akili tambuzi sana na memory kali kabisa. Kumbuka alikuwa na mkichwa unaofahamu hadi urefu wa kila barabara kuu ya Tanzania. Lakini Kiingereza kikawa hakipandi. Hii ilitokana na dharau zake za kudhani hatuhitaji lugha zaidi ya Kiswahili. He was dead wrong on that score.Kwani Prof. Ndalichako au rire jiwe renyewe ririkuwa rinasemaje kuhusu hili la lugha za mabeberu?
Hatupendekezi mitaani au JF kitumike Kiingereza pekee. Ni shule tu ndiyo kitumike Kiingereza peke yake. Tunapenda wahitimu wa elimu ya sekondari wawe na uwezo wa kuongea na kuandika lugha zote mbili. JF ni nje ya shule.Hivi JF wakisema kitumike kiingereza tu, mijadala na maarifa yaliyomo humu tungepata? Kiingereza ni moja ya mambo yanayofanya tusiendelee
Je wajua katika Marais sita wa Tanzania, waliokuwa na uwezo wa kuongea Kiingereza kwa ufasaha ni Mwl Nyerere, Mzee Mwinyi na Mzee Mkapa, the rest hawana fluency kwenye kuongea zaidi wanaokoteza kulalMadhara ya Kutokipa Kiingereza Umuhimu
Siku hizi nchi yetu ina tatizo la wananchi wengi kutoweza kuandika na kuzungumza kwa lugha ya Kiingereza. Kiuchumi, TAZIZO HILI SIYO HIMILIVU.
Adhari zake ni pamoja na zifuatazo:
1. Kukosa ajira za kimataifa. Nchi kama Uingereza inakuwa na upungufu wa manesi mara kwa mara. Wanaajiri toka Malawi, Kenya na nchi nyingine ambazo raia wake wanamudu lugha ya Kiingereza.
Mashirika kama Emirates huwa yanahitaji waajiriwa wachache wanaoweza kuongea Kiswahili na Kiingereza. Huwa wanaajiri Wakenya kwani wana hiyo sifa.
2. Kukosa ajira nchini. Nyumbani kwenyewe mashirika binafsi wanapenda zaidi wahitimu waliosoma nje kwani wao humudu lugha zote mbili.
3. Kukosa fursa za kusikika ulimwenguni. Mashirika ya habari kama Aljazeera na BBC World service wanapotaka kuongea na mtu wa Afrika Mashariki, kwa Kiingereza, huwa hawachagui Mtanzania. Wataongea na mwalimu wa chuo kikuu Mkenya au Mganda. Hii inafifisha umaarufu wa vyuo vyetu. Vinashuka kwenye viwango rasmi vya ubora duniani.
Ukiweka YouTube kitu kwa Kiswahili maana yake unakilenga kwa watu milioni 200. Ukiweka kwa Kiingereza basi umekielekeza kwa watu zaidi ya mara tano ya hao.
4. Kudumaza elimu. Reading materials mtandaoni sehemu kubwa ni za Kiingereza. Mtu asiyeelewa vizuri Kiingereza tayari anajinyima asilimia kubwa ya maarifa yaliyopo duniani.
5. Kudumaza utalii. Kutosikika kimataifa kunatunyima watalii wengi. Pia wachache wanaokuja wanajikuta hata watu wa uhamiaji na polisi hawawezi kuzungumza nao kwa Kiingereza.
Miaka ya sitini tulikuwa vizuri tu kwenye Kiingereza. Mhitimu wa shule ya sekondari alikuwa anabidika kufaulu Oral and written English.
Napendekeza kwamba:
1. Interview za ajira serikalini zizingatie uwezo wa kusema na kuandika Kiswahili na Kiingereza. Kumudu Kiingereza iwe a condition for employment of ALL civil servants.
2. Kuwe na sera ya wanafunzi shule za sekondari kuongea tu Kiingereza wawapo shuleni. Hii haitadhoofisha Kiswahili kwani watakiongea sana nyumbani na mitaani.
3. Kufaulu kidato cha nne iwe ni pamoja na kufaulu Oral English. Mitihani yake itasimamiwa na shule kama ilivyokuwa miaka ya sitini.
Huu uzi nimeuleta kama hatua ya kupambana na hali yangu. Ni hali ya kukosa furaha kutokana na kuona mwelekeo usio sahihi wa taifa langu. Siishi mwenyewe naishi na wananchi milioni 60. Their loss is my loss. And we have been losing a lot on account that we have not given due emphasis to competency in English.Pambania hali yako
Kenya wako kwenye take off stage. Natumaini unaelewa take off stage ina maana gani kiuchumi.Zambia,Malawi,Kenya,Ghana wanaongea kingereza sana tu. Je wametupita nini katika maendelea ya kiuchum,sayansi na teknolojia?
Kinachowasumbua ni utimwa wa kifikra, huu ugonjwa kumtoka mwafrika ni kazi sana.
Wkati wewe unawaza kingereza kuna waafrika wenzio wanawaza kifaransa kifundishwe vizuri lakini kuna wengine wanawaza kireno bila kusahau kiarabu.
Ni ukoloni tu unaowasumbua watu weusi hakuna kingine.
Masomo mpaka chuo kikuu yawe kwa kiswahili. Kiingereza kifundishwe kama somo.Hatupendekezi mitaani au JF kitumike Kiingereza pekee. Ni shule tu ndiyo kitumike Kiingereza peke yake. Tunapenda wahitimu wa elimu ya sekondari wawe na uwezo wa kuongea na kuandika lugha zote mbili. JF ni nje ya shule.
Wapendekeza tufanikisheje hiyo KPI? Mimi nimetoa pendekezo langu. I think it is a feasible way of achieving the required competency.
Resources (vitabu, research journals, etc.) za kufundisha ngazi zote kwa Kiswahili ziko tayari?Masomo mpaka chuo kikuu yawe kwa kiswahili. Kiingereza kifundishwe kama somo.
Unaweza kuonyesha hio udadi ya hao manesi wanaopata sana ajira .Kenya wako kwenye take off stage. Natumaini unaelewa take off stage ina maana gani kiuchumi.
Ghana pia wametupita sana miaka hii. Huko nyuma, tulikuwa tunasikika sana na UDSM was ranked, by Webometrics, well ahead of all universities in Ghana and Kenya. Sasa kimeshuka sana. There are economic consequences to this.
Malawi na Zambia hawajatupita kwa sasa. Ila manesi wa Malawi wanapata sana ajira Uingereza. Wakwetu wanakwama lugha.
But to find a country that speaks English and is not better off than us doesn't prove that English is unimportant.
Kutambua kwamba tunahitaji kujua Kiingereza sio mawazo ya kitumwa. Utumwa wa kitu gani? Ni ukweli kwamba bila Kiingereza kuna makala nyingi duniani ambazo hutaweza kuzisoma.
We jamaa serikali ya Tanzania haipeleki wvijsna kwenda kusoma huko ulaya na America?Tatizo ni jinsi tunavyofikiria. Je ni "kingereza na kiswahili" au ni " kingereza au kiswahili"? Kwa elimu na biashara / uwekezaji kingereza ni muhimu na huwezi kukikwepa. Vyuo vingi duniani vina programu na kozi zinazofundishwa kwa kiingereza ( mfano ni China, Urusi, Japan, Ufaransa, etc). Nchi hizo pia huwafundisha wanafunzi wao kingereza hata kama masomo mengine yanafundishwa kwa lugha zao. Mimi modeli yangu ni "kingereza na kiswahili " lakini tutahitaji uwekezaji mkubwa kwa lugha zote mbili. Kwa sasa wengi wetu tu wabovu kwenye kingereza na kiswahili pia. Rasili mali kubwa ya nchi yeyote ni watu wake na elimu yao ni kitu muhimu. Mafanikio ya China hapa jf hutolewa kama mfano wa maendeleo bila kingereza, ukweli ni tofauti kabisa kwani uchina pamoja na mambo mengine ilipeleka vijana kwa maelfu kwenda kusoma uingereza na america wengine wakifanya ujasusi wa technologia. Hawa wana mchango mkubwa kwenye kuipaisha nchi yao. Tuwekeze kwenye ufundishaji wa hizi lugha tutafika mbali.