SoC02 Athari za Matumizi ya Simu barabarani na Sheria

Stories of Change - 2022 Competition

Caesarln

New Member
Joined
Jul 26, 2022
Posts
4
Reaction score
1
Athari za Matumizi ya Simu Barabarani na Sheria

Utangulizi
Kulingana na tafiti za Shirika la Afya Duniani(WHO) za mwaka 2022; ajali za barabarani zinaongoza duniani kwa kusababisha vifo, ambapo takribani watu milioni1.3 hufariki kila mwaka kutokana na ajali za barabarani. Huku madhara makubwa zaidi yakiwa ni kwa watoto na vijana kuanzia miaka 5-29. Asilimia 93% ya ajali zote hutokea kwenye nchi za uchumi wa chini na kati.

Zipo sababu nyingi ambazo zinapelekea ajali za barabarani, lakini nakala hii imejikita zaidi kwenye matumizi ya simu kwa madereva na waenda kwa miguu kama chanzo cha ajali zinazopelekea vifo, majeraha, ukilema na uharibifu wa miundombinu.

Ajali nyingi zinatokea chini na chanzo kimoja wapo na kikubwa ni matumizi ya simu barabarani. Ajali ambazo kwa namna moja ama nyingine zinarudisha nyuma uzalishaji mali kwa mtu mmoja mmoja, familia, jamii na nchi kwa ujumla. Hii inaonesha wazi kwamba matumizi ya simu yanahusiswa na mtumia barabara kutokuwa makini na mazingira yanayomzunguka.​

Dereva
Shiriaka la Afya Duniani (WHO) kwenye chapisho lao la “Road Traffic Injuries, 20 June 2022” linasema kwamba, kuna uwezekano mara 4 kwa dereva anayetumia simu kusababisha au kupata ajali kuliko dereva ambaye hatumii simu. Hii ni sahihi kwa sababu; kundesha gari na kutumia simu kwa wakati mmoja, iwe ni kusoma, kuandika na kutuma ujumbe, kuongea na mtu kwenye simu au kutumia “earphones,” hupunguza uwezo wa dereva kulimudu gari lake akiwa barabarani. Mfano, matumizi ya simu yanaweza kumpelekea dereva yafuatayo:-​
  • kotoshika breki kwa muda sahihi.​
  • kutofuata alama, ishara, taa na michoro ya barabarani.​
  • kutotilia maanani watumiaji wengine waliopo barabarani.​
  • Dereva anaweza asiwe kwenye umbali salama kati ya gari lake na la mbele yake.​
  • kwenda mwendo mdogo na kuwa kizuizi au kero kwa watumiaji wengine wa barabara (hili ni kosa kisheria kwa mjibu wa kifungu namba 56 cha sheria ya usalama barabarani).​
Haya yote hutokea kwa sababu umakini wa dereva utakuwa kwenye simu muda huo. Dereva huyo atasababisha mazingira hatarishi zaidi endapo akishtukizwa au kupata taarifa ya kushtua, au ya kumsababishia mawazo kutoka kweye simu akiwa barabarani. Lakini sio hilo tu, dereva akiwa anaandika na kutuma ujumbe, mikono au mkono wake hautakuwa kwenye usukani. Bado na hilo ni tatizo kubwa sana, chochote kinaweza kutokea na akashidwa kumudu usukani wake vizuri.

Na ijulikane kwamba kuendesha gari kwa kasi ya kilometa 80 kwa saa na zaidi huku unasoma, kuandika na kutuma ujumbe kwenye simu ni sawa na kundesha gari umbali wa uwanja wa mpira na zaidi huku umefungwa kitambaa kwenye macho. Ni jambo la hatari na la kutisha. Baadhi ya watu huiita hali hii “hatari isiyoonekana,” ila kiuhalisia huo ni upotoshaji. Binadamu aliye kamili anajua wazi kwamba kitu chochote kitakachoondoa umakaini wa mtu barabarani ni hatarishi.​

Waenda kwa Miguu
Waenda kwa miguu ni kundi mojwapo kati ya makundi sita(6) ya watumia barabara na ni moja ya kundi ambalo linaathirika sana na mara kwa mara na ajali za barabaran. Ujio na ongezeko la simu janja limefanya ajali ziongezeke sana kwenye kundi hili.

Ukiingia YouTube utakutana na video nyingi zikionesha watu wanaogongwa, wanaojigonga kwenye vyombo vya moto, miundo mbinu ya barabarani, mtu na mtu, kuanguka au kutumbukia kwenye mashimo na yote hii ni sababu ya matumizi ya simu. Haya yote yanatokea kwa sababu; mtu akiwa kwenye simu ni vigumu kuona, kusikia au kutambua kinachoendelea kwenye mazingira yanayomzunguka kwa sababu akili au umakini mwingi kama sio wote utakuwa kwenye simu.

Kutumia simu kunaweza kumfanya mtu akajisahahu kwamba yupo barabarani na akashindwa kufauata kanuni na taratibu za barabarani ambazo zipo kwa ajili ya usalama wake na wa watumiaji wengine wa barabara. Mtu anayesoma, kuandika na kutuma ujumbe kwenye simu, yupo kwenye hatari zaidi ya kusabisha au kupata ajali kuliko anayeongea na simu au kusikiliza mziki. Hii sio kwa waenda kwa miguu tu, hata dereva.

Sheria Inasemaje
Kwa mjibu wa sheria ya usalama barabarani ya mwaka 1973, kama ilivyofanyiwa marekebisho mwaka 2002, sura ya 168, kifungu namba 42. Kinazungumzia uendeshaji hatarishi. Kwamba uendeshaji wowote wa chombo cha moto ambao ni hatarishi ni kosa kisheria. Ijulikane kwamba, kuendesha gari huku unatumia simu ni hatarishi.

Lakini kwa upande wa mwenda kwa miguu, sheria imemtaka kuwa makini awapo barabarani ikiwa ni kutembea upande wa kulia pembezoni kabisa mwa barabara, kuvuka barabara kwa uangalifu, asiwe kwenye namna au hali ambayo ni hatarishi kwake na watumiaji wengine wa barabara na kufuata sheria kanuni na taratibu kama ilivyobainishwa kwenye kifungu namba 65(1-14) cha sheria tajwa. Ifahamike kuwa, mwenda kwa miguu kuwa kwenye hali au namna ambayo ni hatrishi ni pamoja na matumizi ya simu barabarani. Pamoja na hayo, bado sheria ya usalama brabarani inahitaji marekebisho au mboresho hasa kwenye kipengele cha matumizi ya simu barabarani. (angalia aya ifuatayo kwa maelezo zaidi).​

Ushauri
Tekinolojia ya aina yeyeote haiji na faida peke yake kwenye jamii, bali hubeba na madhara vile vile, na ndio maana sheria itahitajika kwa ajili ya kuifanya technolojia hiyo iishi vizuri kwenye jamii. Kuna uhitaji mkubwa wa kudhibiti matumizi ya simu barabarani kisheria pamoja na usimamizi wake na mabadiliko kisheria ndiyo itakuwa ngazi ya kufanikisha hilo. Hivyo basi, matumizi ya simu ni muhimu kujumuishwa kwenye sheria kama kipengele au kifungu cha aina yake na sio cha jumla kama sheria ya Tanzania ilivyo. Vile vile adhabu isiwe ya mazoea bali iendane na kosa husika. Zipo zaidi ya nchi 30 za mfano ambazo zimefanikisha hilo na Uingereza ni miongoni mwa nchi hizo ambapo sheria na usimamizi wake ni madhubuti sana katika hilo.​

Hiarika kwa Ajili ya Usalama Wako
  • Jiulize, je unaweza kuweka simu pembeni mpaka utoke barabarani? Jibu ni diyo inawezekana baada ya kulinganisha simu au matumizi yake na uhai wako na wa watu wengine.​
  • Kama unataka kutumia simu tafta eneo salama pembeni mwa barabara tumia simu yako vyovyote vile na baada ya kumaliza endelea na safari yako.​
  • Jifunze udereva wa kujihami.​
  • Pata Elimu ya usalama barabarani. Elimu hii ni muhimu kwa jamii ya kitanzania. Mabadiliko yanaanza na uelewa na uelewa tunaupata kupitia elimu. Elimu hii unaweza kuipata kupitia mashirika yaliyo jikita kwenye usalama barabarani kama PESACO, AMEND n.k lakini vile vile kupitia jeshi la polisi kitengo husika.​
Zuia ajali kabla haijakuzuia”
 
Upvote 3
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…