Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mbona wao hawakutosheka wakakimbilia kwenye siasa?!ukithubutu kula rushwa au hela ya serikali utaitapika kwa pua sio mdomo.
usicheze na rushwa au hela ya serikali, kama unabisha jaribu uone
Kwa kweli, hali isije kuwa mbaya zaidi ikafikia kipindi nikatoa talaka kwa wake zangu wanne nilionao sio kwa mapenzi yangu bali sababu za kiuchumi.😭😭Hili lisitokee tafadhali 10 inatosha.
bora na wewe ukimbilie huko huko angalu utasalimika kuliko kujaribu kula rushwa au kuchezea hela ya serikali utaumia bure uache watoto wako wanakulilia.Mbona wao hawakutosheka wakakimbilia kwenye siasa?!
Mbona una hasira sana? Kuna nongwa gani mtu kutoa maoni yake. Unamuambia akae kimya kama nani?Hiyo mishahara ni shs ngapi
Weka Salary slip hapa za wafanyakazi..
Na huu ndiyo ukweli mchungu. Kwa sasa kazi inafanyika kwa kulazimishana na pia kwa kutishana! Maana wanafahamu fika upuuzi wanao ufanya kwa wafanyakazi.Kingine ni mishahara midogo husababisha motisha ndogo ya kufanya kazi.
Wafanyakazi wanasema serikali ina pretend kuwalipa mishahara, na wao wafanyakazi wana pretend kufanya kazi.
We acha upoyoyo, wewe kila siku hapa Salary scale za waalimu na manesi TGTS na TGHS respectively zinawekwa hapa utanaka ref. ipi zaidi?Hiyo mishahara ni shs ngapi
Weka Salary slip hapa za wafanyakazi
Ukubwa wa hela kwako unaanzia shs ngapi?...
TV ya 500,000/= hadi akakope.Mishahara duni ina athari kubwa sana kwa watumishi wa umma na Taifa kwa ujumla na hizi ni baadhi ya athari hizo kwa watumishi na Taifa letu....
Atujamkosea Mungu kupita kiasi hicho Hadi atususe hivyoUnaweza kuambiwa hiyo mi nne ikiisha, inaanza mingine kumi ya kulia na kusaga meno.
watakuwa wamekusikia mkuuMishahara duni ina athari kubwa sana kwa watumishi wa umma na Taifa kwa ujumla na hizi ni baadhi ya athari hizo kwa watumishi na Taifa letu.
1. Low purchasing power
Mishahara duni inapunguza uwezo wa mtumishi kufanya manunuzi na hivyo wakati mwingine humlazimisha mtumishi kukimu mahitaji yake kwa kukopa kugharamia basic needs na sio kukopa ili afanye biashara au kuongeza mtaji wa biashara yake.
Mtumishi wa nchi hii hata kununua tv ya shilingi 500,000/=, inabidi akakope Benki au katika vicoba, n.k vinginevyo atalaza watoto njaa.
2. Stress
Mishahara duni ni moja ya chanzo kikubwa cha stress kwa watumishi wa umma kwani hela anayopata mwisho wa mwezi haitoshi kumfikisha mwezi unaofuata kwa sehemu kubwa ya mshahara huo mdogo inatumika kulipa madeni na hivyo kumuacha mtumishi akiwa na mawazo(stress) ya namna ya kumaliza mwezi.
3. Uwezo mdogo wa kujiwekea akiba
Mishahara duni inafanya kuwa ni vigumu kwa mtumishi wa umma kuweka akiba katika Maisha yake na matokeo yake akipata dharau solution yake ni kwenda kutafuta mkopo.
4. Uwezo mdogo wa kukopesheka
Moja ya athari ya mishahara duni ni mtumishi kuwa na nafasi ndogo ya kupata mikopo inayokidhi mahitaji yake kwani wakopeshaji hutoa mikopo kulingana na mshahara (take home) ya mtumishi husika.
Matokeo ya hali ni kuwaweka watumishi katika mazingira magumu ya kujilwamua kimaisha iwe ni katika kutafuta mitaji,kugharamia ujenzi, n.k.
5. Mishahara duni ni chanzo watumishi kuwa na mikopo mingi mitaani (multiple loans)
Mtumishi mwenye mshahara mdogo hulazimika kukopa sehemu tofauti tofauti ili kukidhi mahitaji yake kwani taasisi nyingi za mikopo hukwepa kuwa mikopo mikubwa kwa hofu ya kushindwa kurejesha hivyo watumishi hulazimika kukopa katika taasisi zaidi ya moja na hata kwa watu binafsi mitaani.
6. Chanzo cha watumishi kujiingiza katika rushwa, ufisadi na ubadhirifu wa mali za umma
Pamoja na ukweli kwamba siku zote binadamu hatishiki na mshahara hua hautoshi, lakini ni kweli pia mishahara duni isiyokidhi mahitaji ya msingi ya mtumishi na familiar yake, humsukuma mtumishi kutumia nafasi yake katika Utumishi wa umma kupata fedha za ziada hata kwa njia zisizo halali ili aweze kumudu maisha tofauti na wale wanaotumia madaraka yao kujilimbikiza mali.
7. Chanzo cha mafao madogo ya uzeeni
Wote tunajua kuwa mafao ya kustaafu anayolipwa mtumishi baada ya kustaafu hutegemea na mshahara wake wakati anastaafu.Hivyo, watumishi wenye mishahara midogo hata mafao ya huwa madogo.
8. Maisha magumu ya uzeeni
Mtumishi ambae kwa bahati mbaya mpaka anastaafu ameshindwa kuwekeza, mtumishi huyu ataishia kuishi maisha magumu bada ya kustaafu hasa ikitokea anastaafu huku bado ana watoto wanaomtegemea.
9.Mifuko ya hifadhi ya Jamii kuathirika kiuchumi
Kama mishahara ni duni na haiongezeki, tafsiri take ni kuwa hata makato yanayoingia katika mifumo hii yanakuwa madogo na pia hayaongezeki kwani makato hukatwa kwa asilimia ya basic salary ya mtumishi. Hivyo, mama mshahara hauongezeki, maana yake hata pato la mifumo hii nalo haliongezeki.
10. Uwezo wa Mifumo ya Hifadhi ya Jamii kuchangia maendeleo ya nchi kushuka
Wote ni mashahidi wa jinsi mifumo hii inavyotumia fedha za wanachama kujenga vitega uchumi kama kujenga malengo,n.k pamoja na kuiokpesha serikali.
Hivyo, vipato vya hii mifuko vinapkuwa haviongezeki, maana yake ni mchango wa mifuko hii katika shughuli za kiuchumi za nchi hushuka pia.
11. Mishahara kutoongezewa kunaathiri mzunguko wa fedha
Ukiwalipa vizuri watumishi, maana yake ni kuwa umeongeza uwezo wao wa kufanya manunuzi mitaani na hivyo kuongeza mzunguko wa fedha mitaani.
12.Kunaathiri utoaji wa mikopo katika mabenki na taasisi nyingine za kifedha
Ukiongeza mishahara, maana yake pia umeongeza uwezo wa mtumishi kukopesheka, na hivyo ku-boost biashara ya mabenki katika kukopesha na kwahiyo kuongeza faida ya mabenki na automatically kodi ya serikali kutoka katika mabenki na taasisi zingine za kifedha inaongezeka.
13. PAYE kutoongezeka na serikali kukosa mapato
Kwasababu PAYE hutegemea mshahara mtumishi anaolipwa, mshahara inapokuwa mdogo au kutoongezeka, maana yake ni mchango wa PAYE katika mapato ya nchi unafubaa na matokeo yake kuipunguzia serikali mapato.
14. Kushusha ana kuondoa morali ya kazi miongoni mwa watumishi
Mishahara inapokuwa midogo au kutoongezeka kwa muda mrefu, hali hiyo kushusha morali ya kazi miongoni mwa watumishi na hivyo kupunguza ufanisi wa kazi na madhara ni kwa nchi na wananchi wanaotafuta huduma katika ofisi za umma
15. serikali na chama tawala kuchukiwa
Hii ndio athari ya kisiasa kwa chama tawala na serikali iliyoko madarakani na ni advantage kwa vyama vya upinzani.
Unafika katika hospitali ya umma unakutana na Daktari au Nesi mwenye stress zake(anawaza ada ya mwanae,madeni mtaani n.k) unaishia kupata huduma mbovu inayotishia afya na hata uhai wa mgonjwa kisa kikiwa kipato kidogo kinachowaweka watumishi hawa katika mazingira magumu kimaisha.
16. Nchi kuendelea kushuka nafasi za juu miongoni mwa nchi ambazo raia wake hawana furaha
Kutoka na stress na ugumu wa maisha unaotokana na mishahara duni,watu watakosa furaha ya maisha na hivyo kuchangia nchi yetu kuwa ni miongoni mwa nchi ambazo raia wake hawana furaha kama ilivyo sasa na kama ambavyo itaendelea kuwa unless hatua zinachukuliwa kuboresha standard of living ya watu wetu.
Hizi ni baadhi ya athari ambazo, kwa mtazamo wangu, zinatokana na mishahara duni na pia kutoongeza kabisa mishahara ya watumishi wa umma kwa miaka sita sasa.
CC: Waziri wa Fedha na Waziri wa Utumishi
Ndio ukweli wenyewe huo vinginevyo watoto wanalala njaa.TV ya 500,000/= hadi akakope.
Hahahaaaa
Magufuli mwenyewe anajua yanayo endelea maofisini.ukithubutu kula rushwa au hela ya serikali utaitapika kwa pua sio mdomo.
usicheze na rushwa au hela ya serikali, kama unabisha jaribu uone
Kipindi cha JK kuna time tulikaa na washkaji, tukawa tunaponda utawala wake ulivyokuwa wa ovyo.Atujamkosea Mungu kupita kiasi hicho Hadi atususe hivyo
Mwanaume gani wewe??una gubuHiyo mishahara ni shs ngapi
Weka Salary slip hapa za wafanyakazi
Ukubwa wa hela kwako unaanzia shs ngapi?
Unapiga kelele sana hapa JF bila takwimu za mishahara
Wewe hujui kupanga matumizi, Ukiweka salary slip hapa, Ficha details zingine
Wewe umekosa elimu ya Finance na Economics
Tangu lini mahitaji ya mtu yakatimizwa, Ukinunua helcopter utahitaji Dreamliner
Furaha ni wewe binafsi na sio pesa
Kuna watu wanafuraha na hata hawajawahi kuajiriwa na wala hawajajiajiri ni wakulima wa kawaida tu wasiotambulika
Kaa kimya wewe Mwanaume, Mkeo itakuwaje sasa?
Mkuu Wewe endelea kufaidi dunia huko uliko. Waachie kilio wenye msiba wao. Usiwakatishe tamaa zaidi.Unaweza kuambiwa hiyo mi nne ikiisha, inaanza mingine kumi ya kulia na kusaga meno.